Wito kwa Wanazuoni na Wanafikra: Kwa hakika ninawaita wanazuoni, wanafikra, watu wa utamaduni na waandishi warudi kuyahuisha tafiti na masomo ya kijamii na kuyangalia kwa kina na kunufaika nayo, ili tuinuwe kiwango cha jamii yetu na kuifanya iwe tayari kupokea dola ya Imamu aliyeahidiwa (a.s) na uongozi wake wenyebaraka utakaoanzia kwenye ardhii tukufu. Tafiti hizo zinapaswa ziwe wazi na zenye nia dhabiti ili ziwe ndio msingi wakuanzia, na hapo ndipo mambo mengi yaonekanayo kuwa ni sahihi utayaona yako kinyume kabisa: “Na ...
Sababu za Kuendelea Umma: Hakika uhai wa Umma na utukufu na maendeleo yake ni kusoma na kujifunza, wakati ambao jamii ya kijahilia na uliyobaki nyumba matendo yake hayatofautiani na maisha ya wanyama. Anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: “Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita kwenye lile litakalowapa uhai” Surat Al-Anfaal: 24. ...
Umma wa Kusoma: Ni haki yetu Sisi Umma wa Kiislamu kujifakharisha kwakuwa Sisi ni Umma Kusoma na kutafuta elimu, na kwamba neno la kwanza kuteremka kwa Mtume (s.a.w.w) pindi alipopewa ujumbe wa kiislamu lilikuwa ni (Soma), yaani amri ya kusoma, hali kadhalika kwamba muujiza wa kudumu wa Uislamu, yaani Qur’ani ni kitabu chenyekusomwa, ambacho kimetokana na neno ‘qiraatu, yaani: kusoma. ...
Kurejesha Heshima ya Umma wa Kusoma na Kalamu: Ni wajibu wetu tuirejeshe heshima yetu na tuwe kweli ni Umma wa Kusoma na Kitabu. Tuliongoze gurudumu la mwamko wa kitamaduni kwa wote na tuhimize kusoma vitabu kwa namna mbalimbali na kuvipa umuhimu. Tusambaze vitabu, tuwashawishi watu kusoma na kubuni njia tofauti zitakazoinua kiwango cha utamaduni kwa watu kupitia kueneza maonyesho ya vitabu, kuvifanya vipatikane kwa bei nafuu, kuvichapisha katika maumbile yenye kuwavutia wasomaji, kurahisisha uandishi wake na kutofautisha maudhui zake. Tuvifanye kuwa ...
Mwanzo wa Mwaka wa Kimaanawi: Mwaka wa kimaanawi kwa watafuta ukamilifu na wenye shauku ya radhi ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka, huanza mwanzoni mwa mwezi wa Rajabu. Mwanzo: maana yake ni kupiga hatua, kuiandaa azma, kuzidisha uchangamfu, kupitia kurasa za matendo yaliyopita, na kuweka matarajio ya kufungua kurasa mpya nyeupe. ...
