IMAM HUSSEINI (A.S) NI HARAKATI UFAHAMU (MWAMKO) MABORESHO
MARJII YAQOOBI: IMAM HUSSEINI (A.S) NI HARAKATI UFAHAMU (MWAMKO) MABORESHO
Kwa Jina la Allah
Imam Husseini ni Harakati ya Mwamko wa fikra na Maboresho (Islahi)
Tunatumia fursa ya kukaribia mwandamo wa mwezi mtukufu wa Muharam kusisitiza ujumbe huu kwa wapenzi wa kazi kizazi cha mtume (w.a.w.w) miongoni mwa makhatibu, washairi, watu wa mawakibu na vituo vya kuwahudumia wapenzi wa Imam Husseini (a.s) na waumini wote kwa ujumla, juu ya
Mwamko na Urekebishaji, vitu ambavyo ndivyo alivyovikusudia Imam Husseini (a.s) katika mapinduzi yake matukufu kama ilivyokuja katika ziyara ya Arobaini yake kutoka kwa Imam Swadiq (a.s):
(وَبَذَلَ مُهْجَتَهُ فيكَ لِيَسْتَنْقِذَ عِبادَكَ مِنَ الْجَهالَةِ وَحَيْرَةِ الضَّلالَةِ)
(Na akamwaka damu yake kwa ajili yako; ili awaokoe waja wako kutokana na ujinga na tayari ya upotevu). 1.
Kama ambavyo aliweka wazi malengo yake katika hotuba zake nyingi, miongoni mwa maneno yake (a.s) ni pale aliposema:
(وإنما خرجت لطلب الإصلاح في أُمّة جدّي مـحمد (ص) أُريد أن آمر بالمعروف، وأنهى عن المنكر، وأسير بسيرة جدُي مـحمد (ص) وسيرة أبي علي بن أبي طالب (ع).
(Na kwa hakika nimetoka ili kutafuta maboresho katika uma wa babu yake Muhammad (s.a.w.w), ninataka kuamrisha mema, na kukataza mabaya, na nifuate mwenendo wa babu yangu Muhammad (s.a.w.w) na mwenendo wa baba yangu Ali bin Abi Twalib (a.s)2.
Na kama ilivyo wazi, kwamba yote haya yanaingia katika lengo tukufu la Mwenyezi Mungu la kuteremshwa sheria za mbinguni, ambalo ni kusimamishwa dini katika maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii, ikiwa ni pamoja na kuwakusanya watu kwenye msingi wa haki na uadilifu. Amesema Mwenyezi Mungu:
( شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ).
(Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo). Surat Shura: 13.
Hivyo, tunatoa wito mpya tukitarajia wito huu iwe ni miongoni mwa alama tukufu za Imam Husseini (a.s). Wito huu ni kueneza vitabu na majarida ambayo yanabainisha ufahamu huu wa mwamko na mapinduzi ya Imam Husseini (a.s), ikiwa ni pamoja na kuasisi maktaba miskitini na katika huseinia, mawakibu na vikundi mbalimbali. Mfano wa vitabu huu hivi vitolewe ili kutoa fursa kubwa ya kunufaika navyo. Na lau kila mtu mmoja atajitolea walau kitabu kimoja tu, bila shaka ndani ya mwezi huu wa Muharam kungelipatikana maelefu ya maktaba na mamilioni ya vitabu ambavyo vingeliendeleza mapinduzi haya ya Imam Husseini (a.s) na hoi ingelikuwa ni mafanikio makubwa ya kitamaduni ambayo yanahifadhi ubinadamu wa watu baada ya ujumbe na ufunuo wa mbinguni.
Kwa hakika mwamko wa (Husseini (a.s) kama mwanafunzi) tulioutoa miaka kadhaa na ukapokelewa na waumini, ulikuwa ni wenye mafanikio na matunda kwa pande zake zote na uliacha athari njema na zenye baraka, kiasi kwamba maelfu ya wanafunzi walipata mitaala na silabasi za masomo, na mashule yakapata idadi kubwa ya madawati na vifaa vingine kwa baraka za mwamko huo. Hali kadhalika, shule nyingi zilifanyiwa ukarabati na maboresho, shule ambazo wizara ya elimu na malezi ilikuwa imeshindwa kuzifanyia mambo hayo. Na kiukweli, harakati hiyo ilitoa sura mpya ya mwamko na ufahamu mpya wa marasimu na shaairi za Imam Husseini (a.s), ufahamu ambao ulibainisha sura ya kitamaduni ya mapinduzi matukufu ya Imam Husseini (a.s). Na matarajio ni kuwa harakati na mwamko huu pia uwe kama ule uliotangulia.
Jambo jingine, ni kuwa wito huu si maalum kwa ajili ya nchi yetu pendwa ya Iraq, bali ni wito unaoelezwa kwa waumini wa kila nchi ya ulimwengu huu. Hata tunaweza kusema kuwa, huwenda nchi hizo zikawa ndio zenye haja zaidi ya harakati. Na ni vyema harakati hizi ikaambatana na mambo yanayowahimiza na kuwasukuma watu na hasa vijana kujisomea, kama ile ya (Soma dakika 10 na ukimiliki kitabu) au kufanyia mashindano baadhi ya maarifa yalimo ndani ya vitabu hivyo, au kuandaa zawadi kwa atakae atakayesoma kitabu na kukimaliza na mfano wa hayo.
Na hakika Mwenyezi Mungu ametuwafikisha kutoa hotuba nyingi katika uga huu, nyingi zimekusanywa katika cha (Fii Thaqafatir Radhi wa Isw'lahil Mujtamai'), kama ambavyo kuna vitabu vingi vinavyotoa mtazamo wa kisasa juu ya kadhia ya Imam Husseini (a.s). Hivyo, ni matarajio yetu vitabu hivyo vichapwe upya na visambazwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka.
(إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُم)
(Mkimnusuru Mwenyezi Mungu, naye Mwenyezi Mungu atakunusuruni na kuzithibitisha nyayo zenu.) Surat Muhammad: 7.
Muhammad Yaqoobi- Najaf Ashraf
24/Dhul-Hijjah/1442H
sawa na 04/08/2021
____________________________________
1. Mafaatihul Jinan: UK: 468.
2. Kitaabl Futouh: Juzi:5, UK: 33.