Mwanzo | | Maneno ya maadili | Mila na desturi za jamii
Mila na desturi za jamii

Shiriki swali

Uvutaji wa Sigara hauleti picha nzuri

“...Uvutaji wa sigara hauleti picha nzuri, na ni wenye kudhuru katika kila sekta, kiuchumi, kiafya, kijamii, na hata kitabia.

Saa kuna haja gani ya kuendelea kuitumia, achilia mbali kuzama kabisa katika uvutaji?!....”.

Shiriki swali

Naomba sana nisikutane na….

“...Naomba sana nisikutane na kijana wa Kiislamu  ambaye anaweka nywele zake kama mwigizaji wa filamu ya Titanic. Au binti wa Kiislamu hana hijabu, au hata kama anayo basi ni kama vile wanawake wa Kifaransa au Kimarekani  .

Au unakutana na mwingine mwenye kuvaa cheni tena hata msalaba wakati mwingine, au kuweka bangili katika mikono yake huku akiongea kama binti na hakuna ishara yeyote ya kuonyesha kama ni mvulana...”

Shiriki swali

Miongoni mwa mambo yenye kuchekesha....

“...Miongoni mwa mambo yenye kuchekesha na kuleta mizaha ni haya ambayo wanayaita maandamano yenye kupinga uadui wa Marekani na Israel hali ya kuwa watu wamevaa mavazi yao, wanatumia bidhaa zao, wanawaiga katika ada zao na mienendo yao katika filamu zao, na wanaishi maisha yao kwa misingi yao, na hata kuwaita watoto wao majina yao. Kwa hakika hii ni yenye kuchekesha lakini inaliza....”.

Shiriki swali

Inanisikitisha kuona vijana....

“...Inanisikitisha sana kuona vijana wakiwaiga wamagharibi katika uvaaji wao, ulaji wao, utembeaji wao, namna ya kuishi kwao, kana kwamba hawana historia yao mpaka waishie kunakili kutoka kwao...”

Shiriki swali

Haifai kufanya kitu.....

“...Haifai kufanya kitu chochote cha kijinga na ambachi hakina akili ndani yake, kwa maana hisia ni lazima zihukumiwe na akili na wala si kinyume chake, kama ambavyo haifai kuwa chini ya ada na kufuata bila kuangalia nafasi ya sheria na misimamo yake, kwa maana yenye kukubalika yafanywe na yenye kukataliwa basi yaachwe.

Na ikiwa kuachana na jambo hilo ni aibu basi ni bora aibu kuliko kujiingiza motoni.

Imamu Hassana as anasema “...Mwenye kuabudu asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi huwa amefanya shirki, kwa maana ibada ni kutii hivyo ni lazima iwe kwa Mwenyezi Mungu tu...”

total: 5 | displaying: 1 - 5

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf