Mwanzo | | Maswali ya Kisheria
Maswali ya Kisheria

Shiriki swali

Ayatollah Yaaqobiy akemea kila lenye kusababisha tofauti na mifarakano.

Swali:

             Assalamu Alaykum

Kumekuwa na kudhihiri baadhi ya wakati mambo ya kusema vibaya viashiria vya itikadi fulani za kidini kwa namna moja au nyingine, ni upi msimamo wenu katika kuelekea jambo kama hili?.

 

Jawabu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako pia.

Msimamo wetu katika jambo hili upo wazi mno, kwani katika maelezo yetu mbalimbali tumekataza jambo hili, kutokana na kuwa ni kinyume na mienendo ya maimamu wetu watukufu na maelekezo yao kwa wafuasi wake.

Bila shaka jambo hili husababisha mizozo na mifarakano, hali yakuwa Mwenyezi Mungu ameshasema kuwa “.....Wala msigombane kwani itapelekea kushindwa kwenu....” Surat Anfal aya 46.

Na kila ambapo kutakuwa kuna mambo mengi ambayo makundi mawili wanashirikiana (Suni na Shia), basi jambo hili lichungwe maradufu, na kama tutashindwa kuunganishwa na haya tunayoshirikiana basi tuungane kwa kumuangalia adui yetu ambaye hachagui wa kumuangamiza katika sisi, na wala kwake si aibu kuangamiza chochote kile hata kama kitakuwa kitukufu katika matukufu yetu.

Inshallah Mwenyezi Mungu ndio msaidizi wa yote.

Ayatollah Yaaqubiy

15/2/1436

5/4/2015

Shiriki swali

 

Hukumu ya kuvaa soksi kwa mwanamke

Swali:

   Je, mwanamke kuvaa soksi mbele ya ndugu wa mume ni katika hijabu ya kisheria, hasa ikiwa wanaishi katika nyumba moja?.

 

Jawabu:

               Kwa jina la Mwenyezi Mungu.

Katika kufanya hivyo ni ihtiyat na tahadhari tu, ili kuweza kuhakikisha kwamba vile viungo zaidi ya  vinavyotakiwa kuonekana, havionekani.

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy.

Shiriki swali

 

Mafiko ya maiti watoto

Swali:

Je, ni ipi hukumu ya mimba na vichanga ambavyo ndio kwanza vinapata roho na kisha kufariki bila hata ya kutenda dhambi?, wana nafasi gani siku ya kiyama, jeni kweli watapelekwa moja kwa moja peponi kama tunavyosikia?.

 

Jawabu:

               Kwa jina la Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa riwaya ni kwamba hao watapelekwa moja kwa moja peponi, na hawataingia humo mpaka pale ambapo watawaombea wazazi wao waumini na wenye subira kwa amri na matakwa ya Mwenyezi Mungu (swt).

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy.

Shiriki swali

Hukumu ya usomaji wa Quran ndani ya mwezi wa Ramadhani

Swali:

    Katika moja ya ftwa zenu mlisema kwamba inawezekana kumfuata Ayotollah Shahid Thani, ila tu tuwarejee nyie katika mambo ambayo yanatofauti baina yenu, na moja ya maswala hayo ni swala zima la usomaji wa Quran na dua kwa makosa, sasa ni upi mtazamo wenu katika hilo?.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Cha muhimu ni kujitahidi mtu huyu asome kisomo sahihi, na hakuna cha muhimu zaidi ya hicho. Kwani kila kitu kina msimu, na msimu wa Quran ni mwezi wa Ramadhani. Na tumeelezea kwa upana zaidi jambo hili katika kitabu chetu cha (Fiqhul Khilaf).

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Baadhi ya sura zenye kuchafua jamii

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na kurehemu.

Kwa hakika jamii yetu imefikiwa na baadhi ya sura chafu zenye kupingana kabisa na mafundisho ya dini yetu tukufu, bali hata kupingana na adabu za watu wenye tabia za kibinadamu zilizokuwa bora.

Na kwa bahati mbaya baadhi ya sura na tabia hizo si tu zimekomea katika jamii. Bali kuna hatari ya kuingia katika dimbwi la kueneza maovu ambalo Mwenyezi Mungu ametutahadharisha nalo, endapo tu tutazembea na kusema kwamba mambo hayo yanaambatana na maisha ya mtu fulani au jamii fulani. Kama ambavyo itapeleka hali ya kuogopa kutenda maasi kuondoka katika nyoyo zetu, na yule ambaye atakuwa katika nafsi yake tayari kuna maradhi basi itamsukuma kuyatenda mabaya hayo. Na hivi ndivyo ambavyo itaenea taratibu mpaka kufikia hatua ambayo itakuwa ngumu tena kuweza kukabiliana na mambo au hali hizo.

Hivyo ni wajibu kwa wale watu wenye wivu na jamii zao, hasa wafuasi wa viongozi wa juu wa kidini (Marajii) si tu kuepuka mambo haya, bali kuweza kuyasafisha katika jamii kwa kutumia njia za hekima na mawaidha yaliyo bora, ikiwa ni katika kushikamana na faradhi tukufu ya kuamrisha mema na kukata za mabaya, ambayo Imamu Ally as katika kuisifia anasema “....Ni katika faradhi za juu na zenye sharafu na utukufu mkubwa...”.

Na tuweze kushikama sisi kwa sisi katika hili, ikiwa ni katika kufanyia kazi aya ya Mwenyezi Mungu aliposema

 “....Na Saidianeni katika mema na kumcha Mungu, na wala msisaidiane katika machafu na uadui...” (Surat maida aya 2).

Kama ambavyo tunatakiwa kuungana katika kutambua hizi hali chafuzi pamoja na kufikisha ujumbe huu mtukufu, ili kuweza kuizindua jamii, kuinasihi, na kuiongoza. Na pia kuweza kuwatukuza watu ambao wanafanyia kazi ujumbe huu katika kujaribu kubadili mitazamo. Mwenyezi Mungu anasema “...Na katika nyinyi kuwe na watu ambao wanalingania kuelekea mambo ya kheri,  wanaamrisha mema na kukataza mabaya...”  (Surat Al Imran aya 104)

Mambo hayo chafuzi ni pamoja na:

1.   Baadhi ya sehemu za kujirembea kina mama au hata sehemu za kibishara nyinginezo kubandika na kuweka picha au michoro ya wanawake ambao wapo katika sura ambazo haziendani na sheria.

Sasa  ni juu yetu kuweza kuwapa ushauri hawa watu kuweza kuzitoa picha hizi, au kuweka nyingine ambazo hazitapingana na heshima ya jamii kiujumla.

2.   Uwepo wa baadhi za hafla na mikusanyiko ya harusi ambayo hukusanya wanawake na wanaume, na kisha kuwepo na baadhi ya mambo ya haramu kama vile muziki na kucheza, au wanawake kuvaa nguo za nusu uchi kwa hoja ya kwamba wakati mwingine wanakuwa katika vikao mahususi vya wanawake.

Bila kujua kwamba ni katika mambo ambayo yanaweza kuleta fitina na uchochezi endapo hao hao wanawake wakaamua kuwahadihithia  waume zao kunako maumbile ambayo wanawake wenzao wanayo,  kwanza haya ni katika mambo ambayo Maasumina wamekataza kabisa.

3.   Baadhi ya vibanda vya kahawa, kumekuwa na ada za kubadilishana baadhi ya majarida au video zisizo na maadili. Au wakati mwingine huzalikana mahusiano ambayo si ya kisheria na hata kupelekea mambo ya madawa ya kulevya wakati mwingine.

4.   Jambo la baadhi ya mawalii wa mwanamke kuweka kiwango kikubwa cha mahari pale binti yao anapochumbiwa, kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa kijana mwoaji.

Pamoja na kwamba wazazi au mawalii wa binti wanakubali kwamba kijana ni mwenye adabu nzuri na mwenye uwezo wa kumfanya binti yao akawa na furaha na kuhifadhi karama zake, lakini bado unakuta wanabakia katika ada na tabia au mambo haya ambayo hayana thamani yeyote. Na jambo hili ni katika mambo ambayo k=huzuia kwa kiasi kikubwa sana utimiaji wa sunna adhimu ya ndoa, kama ambavyo pia ni upingaji wa wazi kabisa wa usia uliopokelewa kutoka kwa Maasumina as. Imepokelewa kutoka kwao wakisema :

“...Endapo mtajiwa na ambaye akili na dini yake vitawaridhisha, basi muozesheni, na kama hamtafanya hivyo basi fitina na uharibifu mkubwa utatokea katika ardhi...”

5.   Ada ya baadhi ya masayyidi (ambao nasaba zao zinafika kwa Mtume saww), Inshallah Mwenyezi Mungu azidishe utukufu wao, ambao wao katika kumchumbia mtoto wao wanaweka sharti la kwamba ni lazima na wewe uwe unatokana na kizazi cha Mtume.

Tumejaribu kubainisha kwa kirefu zaidi katika kupinga ada hii yenye nia ya kuleta dhulma, kwa maana mabinti wenye asili na nasaba ya Mtume wananyimwa haki yao ya maisha ya ndoa kwa kuweka sharti la wao kuolewa tu na wenye asili ya Kisayyidi.

Sheikh Muhammd Yaaqubiy

Ramadhani 7 mwaka 1437

Shiriki swali

Hukumu ya daktari wa Meno

Swali:

      Mtu ametoka kutibu jino lake  na ameambiwa na Daktari kwamba asile na anywe vimiminika tu, jambo ambalo linamfanya kuwa dhaifu na kushindwa kufunga, sasa je, anaweza kuachia funga?.

Jawabu:

                                  Kwa jina la Mwenyezi Mungu

             Ikiwa kufunga kwake kutamuweka katika madhara basi anaruhusiwa kufungua, ila baadae atazilipa.

 

                                 Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

 

Shiriki swali

Funga siku ya shaka

Swali:

      Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya shaka, siku ambayo hatujui kuwa inakamilisha mwezi wa Shaabani au ni tarehe mosi Ramadhani, hasa ikiwa hatuna uhakika wa kuandama kwa mwezi.

Jawabu:

             Kufunga siku kama hii kwa anuani ya kuwa ni Ramadhani si sahihi na batili, na hata kutokujua unanuia nini pia ni batili, kwani lazima ujue kuwa unafunga Shaabani ambayo ni Suna, au Ramadhani ambayo kwa hapa si sahihi. Ila unaweza kuifunga kwa anuani ya kulipiza yaliyo katika dhima yako, na hii itajitosheleza itakapokuja bainika kwamba ni kweli ilikuwa Ramadhani.

                   Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

 

Shiriki swali

Hukumu ya funga ya Ramadhani katika kipindi cha mitihani

Swali:

Salam alaykum Warahmatullah

Sisi ni wanafunzi wa kiume na kike, na Wizara ya elimu imepitisha kanuni ya kwamba mitihani ya mwaka huu itaangukia katika masiku ya Ramadhani, na kutokana na ugumu wa funga katika masiku haya ya joto, ambapo itatufanya kushindwa kurejea masomo yetu kwa ajili ya mitihani ambayo ndio itaamua mwelekeo wa maisha yetu, je, mnaturuhusu kufuturu katika masiku haya ya dharura?, na endapo hatutakuwa na ruhusa ya kufuturu na sisi kwa makusudi tukafuturu, je hukumu yetu ni ipi?

Jawabu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu (swt)

Kwa mwenye kuwa na uwezo wa kufunga na kupangilia muda wake wa masomo kiasi kwamba haitamdhuru katika masomo na mustakbali wake, kama vile aamue kusoma mchana na karibuni na alfajiri basi ni lazima afunge, kwani kwa njia hii pia wengi wamefanikiwa na kufaulu pia.

Na kama mtu atataka kufuturu ili iweze kuwa rahisi zaidi kwake, basi kuna njia ya kisheria ya kufanya hivyo, nayo ni kusafiri kila siku kwa gari masafa ya kilomita 22, ambapo ataruhusiwa kula na kisha kurejea nyumbani kwa ajili ya masomo, na kama mpo kundi pia inawezekana kukodisha gari kwa ajili ya kazi hii kama ambavyo mnakodisha kwa ajili ya kwenda na kurudi mashuleni.

Ama kufuturu kwa makusudi bila ya kuwa na udhuru haifai, ila itakapotokea amefunga kwa kudhania kuwa ataweza, lakini akajikuta imemuwia ngumu na hakuwa na uwezo wa kusafiri basi anaruhusiwa kula au kunywa kiwango hitajika tu na si kujiachia kabisa, na kisha hiyo siku atailipa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Ayatollah Muhammad Yaaqubiy

18 Jamadul Akhar 1436

Shiriki swali

Hukumu za mazungumzo ya kimitandao baina ya jinsi mbili tofauti

Swali:

 Ni ipi hukumu ya mwenye kuzungumza na binti kwa njia za simu au mitandao ya kisasa kwa lengo la kumuongoza au kujadiliana naye maswala ya kijamii yenye manufaa, hasa pale ambapo mtu huyu akawa anamchukulia binti huyu kama dada yake ambaye anaweza kusikia sauti yake na kuzungumza naye muda wowote, kama ambavyo akatoa hoja kwamba baina yao haiwezekani kukazalikana matamanio?.

 Tunaomba mwongozo wako Shekhe wetu.

Jawabu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu.

   Siku zote mahusiano  kama haya hayawi na natija nzuri, maana mara nyingi mno hupelekea kuangukia katika kutenda dhambi, na hii ni kutokana na mahusiano ya kinyoyo ambayo hupatikana, kama ambavyo tajiriba inaonyesha hivyo.

Pia haiwezekani kuainisha lengo ( kama hivyo kumuongoa kama idhaniwavyo), kwa maana hilo lengo linaweza kupatikana kupitia jinsia yake mfano kupitia  chuo cha Zahraa na vinginevyo kwa njia ambayo itawezekana kuwaweka wanawake sehemu moja.

Na ni muhimu sana kukaa mbali na vitimbi vya shetani ambaye huanzia na nukta sahihi kisha baadaye hukengeuka. “....na wala msiwe ni wenye kufuata vitimbi ya shetani...”[1]                             

                                                            Ayatollah Mohammad Yaaqubiy



[1] Surat Baqara aya 168

Shiriki swali

Hukumu ya samaki wasiokuwa na magamba

Swali:

    Je, mnaweza kutupatia sababu ya kuharamisha ulaji wa samaki wasio na magamba?.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Tuna dalili sahihi zenye kuharamisha samaki wasio na magamba, ama ukitaka kuhoji kwanini ni kwamba Mwenyezi Mungu amesema “...Haulizwi kwa afanyayo na wao ni wenye kuulizwa...”  Surat Anbiya aya 23.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

1 2 3 4 5
total: 41 | displaying: 1 - 10

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf