Mwanzo | | Maneno ya maadili | Toa zawadi
Toa zawadi

Shiriki swali

Kuenea kwa Ufukara..

“...Hakika kuenea kwa Ufukara hupelekea udhaifu wa kufanya manunuzi, kuanguka kwa gurudumu la uchumi. Kwa maana hiyo kutoa na kutimiza haki za kisheria kunapelekea watu kuwa na uwezo wa kufanya manunuzi, na hatimaye kukua kwa gurudumu la uchumi...”.

Shiriki swali

Kujizuia kutoa....

“...Mwanadamu mwenye tabia ya kujizuia kutoa au kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hujikuta anatoa sana katika njia ya kumuasi Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho atajikuta ni mwenye majuto siku ya kiyama...”

Shiriki swali

Lazima tutambue kwamba Mungu anatuona....

“....Ni juu yetu kutambua kwamba Mwenyezi Mungu anatuona na hakuna lenye kujificha kwake, iwe mbinguni au ardhini, na kuwa yu karibu nasi zaidi hata mishipa yetu ya koo, na kwamba kila mmoja wetu amewekewa malaika wenye kuorodhesha kila aina ya matendo yawe makubwa au madogo, na kwamba kuna mashahidi ambao ni viungo vyetu wenyewe. Sasa tukizingatia haya bila shaka tutakuwa makini sana katika matendo yetu, na tutajihesabu sana kabla ya kufanya maasi au kupinga amri ya Mungu. Na miongoni mwa mambo ya muhimu ni kutozuia mali na kutoa haki zake...”.

Shiriki swali

Tatizo huwa kubwa pale ambapo....

“...Ukubwa wa tatizo utajulikana pale ambapo tutatambua kwamba kutokutoa khumsi (Moja ya tano) kuna athari kubwa sana katika maisha yetu, kwa maana kila tonge ambalo halijatolewa khumsi linakuwa ni haramu na lina athari mbaya katika vizazi vyetu...”

Shiriki swali

Kila kilicho katika mikono ya watu....

“...Hakika kila aina ya mali iliyopo katika mikono ya watu ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu amewaruzuku, kiasi kwamba kama angalitaka basi asingaliwapa. Sasa vipi wao wanakuwa mabahili katika kumtii na kutekeleza amri zake katika kutoa kidogo tu ya hayo aliyowaruzuku kwa ajili ya kukidhi haja za wengine wenye kuhitajia, na ambao Mwenyezi Mungu amewapa mtihani wa kukosa na ufukara kama ambavyo wao wenyewe pia wamepewa mtihani wa kupewa na utajiri?!

“Ili tu Mwenyezi Mungu aweze kuwajaribu ni nani mwenye kutenda mema”.

total: 5 | displaying: 1 - 5

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf