Mwanzo | | Maneno ya maadili | Imamu Ali (a.s)
Imamu Ali (a.s)

Shiriki swali

Kuhuisha (kudumisha) Majalisi (vikao) za Ahlul-bayt (a.s):

 

Hakika kudumisha kumbukumbu za Ahlul-bayt (a.s) na kuzitaja sifa zao, sio historia isimuliwayo wala vitu vya kale viwekwavyo kwenye majumba ya makumbusho, bali kufanya hivyo ni chanzo na chemchemi inayokusudiwa na kila kiongozi, msuluhishi, mwanafikra, msomi, mlezi na kila msaka haki na heri. Nalo ni mwanga unaomuangazia wanadamu njia ya imani ya kweli, maadili mema na maisha ya furaha. Ahlul-bayt (a.s) hawakutuachia jambo dogo wala kubwa, isipokuwa waliliwekea kanuni sahihi, hata katika yale mambo ya kawaida maishani ambayo ni mara chache watu huyapa umuhimu, kama vile: kula, kufanya tendo la ndoa, kwenda msalani, kulala, kuingia bafuni na mfano wa hayo, ambayo sheria na kanuni za kibinadamu huyakosa na hivyo kushindwa kuikidhi mahitaji yote ya mwanadamu.

Shiriki swali

Athari za kumtawalisha Imamu Ali (a.s) katika Imani na mwenendo:

 

Hakika kumtawalisha Amirul Muuminina (a.s) si jambo la kihisia, kwa sababu ya shakhsia yake adhimu ili tutosheke na kumpenda tu, wala sio suala la kihistoria ili muambiwe: mna nini nyinyi mbona mnarudi nyuma na kuamsha ikhtilafu na tofauti za zamani? Kama ambavyo sio suala la itikadi ya nadharia, ambayo tunaishia kuiamini bila kuwa na athari ya kimatendo, bali jambo hili ni mlango ambao kila ufunguliwapo hufunguka milango elfu moja ya Imani, hukumu, na maadili, vitu ambavyo hutengeneza mfumo kamili wa Imani, na mwenendo kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

 

Shiriki swali

Upweke wa Imamu Ali (a.s):

 

Kutokana na maneno na hotuba za Amirul Muunina (a.s), idhihiri kuwa aliishi akiwa mpweke baina ya watu wake; kwa sababu ya kutofahamu kwao cheo na nafasi yake adhimu, kupenda kwao dunia iliyopambika kwa sababu ya kutanuka eneo la dola ya Kiislamu na wingi wa bidhaa zinazoingia maeneo yao, na hivyo kufuata matamanio yao. Imamu (a.s) alikuwa akiwakemea maswahaba wake na akitumia kila namna ili kuwaamsha, kuwahimiza na kuwajulisha majukumu yao ili wamtii (a.s). Amirul Muuminina (a.s) alikuwa akiongea huku akiashiria kwenye kifua chake kitukufu akisema: “Hakika hapa pana elimu nyingi, laiti ningeliipatia wakuibeba”. Lakini maswahaba wake walimpuuza, hawakufahamu thamani yake wala hawakunufaika naye. Na hivyo wakawa wamezidhulumu nafsi zao wenyewe na kumdhulumu yeye, kwani walimnyima nafasi ya kuwapatia kile alichokuwa nacho. Anasema (a.s): “Hakika jamii zimekuwa zikihofia dhulma ya watawala wao, lakini mimi nimekuwa nikihofia dhulma ya raia wangu”.

Hivyo ni wajibu wetu –sisi wafuasi wa Imamu Ali (a.s)- leo hii tusimdhulumu kama walivyomdhulumu maswahaba wake, na tusijikoseshe kumtii kama walivyofanya, kwani ingawaje alitoweka baina yetu, lakini bado yupo nasi kwa maneno yake, mawaidha yake, hotuba zake, mwenendo wake, historia yake, elimu yake, jihadi yake, usafi wa nia yake, kujitolea kwake, kuzama kwake kwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka na katika ukamilifu wake mwingine

total: 3 | displaying: 1 - 3

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf