Upweke wa Imamu Ali (a.s):

| |times read : 450
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Upweke wa Imamu Ali (a.s):

 

Kutokana na maneno na hotuba za Amirul Muunina (a.s), idhihiri kuwa aliishi akiwa mpweke baina ya watu wake; kwa sababu ya kutofahamu kwao cheo na nafasi yake adhimu, kupenda kwao dunia iliyopambika kwa sababu ya kutanuka eneo la dola ya Kiislamu na wingi wa bidhaa zinazoingia maeneo yao, na hivyo kufuata matamanio yao. Imamu (a.s) alikuwa akiwakemea maswahaba wake na akitumia kila namna ili kuwaamsha, kuwahimiza na kuwajulisha majukumu yao ili wamtii (a.s). Amirul Muuminina (a.s) alikuwa akiongea huku akiashiria kwenye kifua chake kitukufu akisema: “Hakika hapa pana elimu nyingi, laiti ningeliipatia wakuibeba”. Lakini maswahaba wake walimpuuza, hawakufahamu thamani yake wala hawakunufaika naye. Na hivyo wakawa wamezidhulumu nafsi zao wenyewe na kumdhulumu yeye, kwani walimnyima nafasi ya kuwapatia kile alichokuwa nacho. Anasema (a.s): “Hakika jamii zimekuwa zikihofia dhulma ya watawala wao, lakini mimi nimekuwa nikihofia dhulma ya raia wangu”.

Hivyo ni wajibu wetu –sisi wafuasi wa Imamu Ali (a.s)- leo hii tusimdhulumu kama walivyomdhulumu maswahaba wake, na tusijikoseshe kumtii kama walivyofanya, kwani ingawaje alitoweka baina yetu, lakini bado yupo nasi kwa maneno yake, mawaidha yake, hotuba zake, mwenendo wake, historia yake, elimu yake, jihadi yake, usafi wa nia yake, kujitolea kwake, kuzama kwake kwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka na katika ukamilifu wake mwingine