Mwanzo | | Maneno ya maadili | Mwezi wa Rajabu
Mwezi wa Rajabu

Shiriki swali

Mwanzo wa Mwaka wa Kimaanawi:

Mwaka wa kimaanawi kwa watafuta ukamilifu na wenye shauku ya radhi ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka, huanza mwanzoni mwa mwezi wa Rajabu. Mwanzo: maana yake ni kupiga hatua, kuiandaa azma, kuzidisha uchangamfu, kupitia kurasa za matendo yaliyopita, na kuweka matarajio ya kufungua kurasa mpya nyeupe.

Shiriki swali

Baraka za mwezi wa Rajabu:

Hakika utukufu wa mwezi wa Rajabu utatokana na mambo yafuatayo:

Lakwanza: Utukufu mwezi wa Rajabu wenyewe, na kiwango kikubwa kitolewacho kwa mwenyekutenda jambo ndani yake, ambacho hakilingani na kile kitolewacho katika miezi mingine ya mwaka, kwa kitendo sawa na kilekile kama ilivyopokelewa katika hadithi, mpaka ukaitwa kuwa ni (Rajabu yenye kumimina) kwa kuwa rehema za Mwenyezi Mungu ndani yake humiminwa mmimino.

Na la pili: Ni kwamba maandalizi ya ugeni, na dhifa ya Mwenyezi Mungu huanza ndani yake; kiasi kwamba waja wema wa Mwenyezi Mungu, kufurahia Idi yao ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hivyo, mwenye kutaka kupata bahati ya kushiriki ugeni huo, na kufurahia malipo ya Mwenyezi Mungu katika Idi hiyo, basi na aanze kutenda na kufanya maombi ndani ya mwezi wa Rajabu, ili ombi lake liangaliwe ndani ya mwezi wa Shabani, na kufanyiwa maamuzi na Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hii ndio njia ya kawaida ya kupata neema maalumu za Mwenyezi Mungu, ingawaje rehema za Mwenyezi Mungu ni pana zaidi ya hapo.

Shiriki swali

Kushuka neema za Mwenyezi Mungu kwa hatua:

Mwezi wa Rajabu ni mwezi wa Amirul Muunina (a.s), mwezi wa Shabani ni mwezi wa Mtume (s.a.w.w) na Mwezi wa Ramadhani ni wa Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Hivyo, maana yake ni kwamba juhudi za kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na neema zake maalumu, huanzia kwenye mwezi wa Rajabu kupitia kwa Amirul Muuminia (a.s), kwa sababu yeye ndiye mlango wa Mtume (s.a.w.w), na kumtawalisha ndio kipimo cha kukubaliwa matendo. Kisha baada ya hapo neema hizo huangaliwa ndani ya mwezi Shabani, kupitia kwa Mtuwe (s.a.w.w), kwa kuwa yeye ndiye mlango wa rehema za Mwenyezi Mungu, na ndiye njia ya kuelekea kwenye ridhaa yake. Na dalili juu ya haya ni kile kilichopokelewa katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: “Katika usiku huo hubainishwa kila jambo la hikima”, kwamba usiku huo ni usiku wa nusu ya Shabani. Baada ya hapo kadhaa ya  Mwenyezi Mungu hupita kwa kufuzisha na kufaulisha na  hatimaye kupata mwisho mwema ndani ya   mwezi wa Ramadhani baada ya utangulizi wake kutimia.

Shiriki swali

Mwezi wa Rajabu ni kituo cha  neema za Mwenyezi Mugu:

Hakika  mwezi wa Rajabu unaandaa mazingira, na sehemu muwafaka kwa ajili ya kuyapata maarifa ya kumtambua Mwenyezi Mungu aliyetakasika, kwa sababu ni moja ya vituo vya neema maalumu za Mwenyezi Mungu,vile vile ni katika sababu alizoziweka Mwenyezi Mugu, ili kuipata Ridhiwani yake (ridhaa yake). Hivyo, yeyote atakayeyatafuta hayo kwa Mwenyezi Mungu na akayafanyia juhudi, bila shaka Mwenyezi Mungu atampa, kwani hii ni ahadi yake aliyoitoa kwa mtume wake (s.a.w.w). hakika imepokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwamba, alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu alimuweka malaika anayeitwa Dai’I (muitaji) katika mbigu ya saba, basi uingiapo mwezi wa Rajabu yule malaika hunadi kila uingiapo usiku mpaka asubuhi, akisema: “Raha wanayo wenye kufanya dhikiri, raha wanayo wenye kutii, na Mwenyezi Mungu aliyetukuka anasema: Mimi ni mwenye kukaa na mwenye kukaa nae, na ni mwenye kumtii anayenitii, na ni mwenye kusamehe mwenye kuniomba msamaha, Mwezi ni wangu, na mja ni wangu, na huruma ni yangu, basi atakayeniomba ndani ya mwezi huu nitamjibu dua yake, na atakayeniomba nitampa, na atakayetaka hidaya kwangu nitamuongoza, na nimeufanya mwezi huu kuwa ni kwamba baina yangu na waja wangu, atakayeambatana nayo bila shaka atafika kwangu”.

 

Shiriki swali

 Kuchangamkia Fursa za Kheri:

Hakika umuhimu wa Mwezi wa Rajabu, sio tu unatokana na utukufu wake wenyewe na neema za Mwenyezi Mungu zinazotolewa kwa waja ndani yake, bali zaidi ya hayo, hutokana na kuwa ni mwanzo wa miezi ya ugeni na dhifa ya Mwenyezi Mungu ambayo hukamilika ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hivyo ni juu yetu tuziandae nafsi zetu kwa ajili ya kukutana na neema hizi za Mwenyezi Mungu kwa kuzidisha umuhimu, kufanya dhikiri kwa wingi na tuyatathimini mahusiano yetu na Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Tathimini hiyo inaweza kufanyika kwa namna mbalimbali, kwa mfano: matendo mema tuliyokuwa tukiyatenda, basi tudumu nayo na tuendelee kuyafanya kwa uzuri zaidi, na yale ambayo hatukuwa tukiyafanya basi na tuharakie kuyaendea, ama yale tulikuwa tukitekeleza sehemu yake, basi tuyakamilishe. Na iwapo katika ratiba za maisha yetu kutakuwa na upotezaji wa muda wenye thamani kwenye umri wetu katika mambo ambayo hayatatunufaisha Akhera, basi wakati huo ni lazima tujiepushe na jambo hilo, na kuubadilisha kuwa muda wenye manufaa na wenye tija kwa ajili ya matendo mema.

total: 5 | displaying: 1 - 5

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf