Baraka za mwezi wa Rajabu:
Baraka za mwezi wa Rajabu:
Hakika utukufu wa mwezi wa Rajabu utatokana na mambo yafuatayo:
Lakwanza: Utukufu mwezi wa Rajabu wenyewe, na kiwango kikubwa kitolewacho kwa mwenyekutenda jambo ndani yake, ambacho hakilingani na kile kitolewacho katika miezi mingine ya mwaka, kwa kitendo sawa na kilekile kama ilivyopokelewa katika hadithi, mpaka ukaitwa kuwa ni (Rajabu yenye kumimina) kwa kuwa rehema za Mwenyezi Mungu ndani yake humiminwa mmimino.
Na la pili: Ni kwamba maandalizi ya ugeni, na dhifa ya Mwenyezi Mungu huanza ndani yake; kiasi kwamba waja wema wa Mwenyezi Mungu, kufurahia Idi yao ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hivyo, mwenye kutaka kupata bahati ya kushiriki ugeni huo, na kufurahia malipo ya Mwenyezi Mungu katika Idi hiyo, basi na aanze kutenda na kufanya maombi ndani ya mwezi wa Rajabu, ili ombi lake liangaliwe ndani ya mwezi wa Shabani, na kufanyiwa maamuzi na Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hii ndio njia ya kawaida ya kupata neema maalumu za Mwenyezi Mungu, ingawaje rehema za Mwenyezi Mungu ni pana zaidi ya hapo.