Mwanzo | | Maneno ya maadili | Maneno Kwa jila la Mwenyezi Mungu
Maneno Kwa jila la Mwenyezi Mungu

Shiriki swali

Lazima tusimame kidete..

“...Ni lazima tusimame kidete bila kutetereka katika kukemea ufisadi na uharibifu wa fikra, tamaduni, itikadi, mienendo ya mtu binafsi mpaka jamii kwa ujumla....”

Shiriki swali

Hakika siasa...

“..Hakika siasa ni mfano mzuri kabisa wa swala la kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwa maana mwenye kuwepo huko anaweza kutumia nafasi yake kubadili mabaya  na machafu mengi mno, pia anaweza kukidhi haja za waumini na kutatua matatizo yao na kuwapa haki zao pamoja na kuweka uadilifu kwa raia. Na haya yote ndio maana halisi ya jukumu hili kubwa kutoka kwa Mungu  la kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwa maana haliwezi kutimia kwa maana yake pana isipokuwa kwa kuchukua jukumu ka kusimamia raia...”

Shiriki swali

Wivu juu ya dini..

“...NI lazima watu wawe na wivu na uchungu na dini yao katika kutekeleza sheria, kiamrisha mema na kukataza mabaya. Nimesikitishwa sana baada ya kusikia kwamba kulikuwa na ulaji wa wazi kabisa ndani ya mwezi wa Ramadhani uliopita katika baadhi ya vyuo, bila ya kuwepo waumini wenye kujitolea kuwakataza. Naamini kama watu wote wangesimamia hili basi wale waovu wasingepata nafasi ya kuvunja sheria za Mwenyezi Mungu ndani ya mwezi mtukufu...”

Shiriki swali

Moja kati ya majukumu ya kijamii..

“...Moja kati ya majukumu ya kijamii ambayo si haki na ni dhulma kusema ni Wajib Kifaii (Ulazima ambao endapo mmoja atasimamia basi wengine inakuwa si lazima kwao),  ni swala la kuamrisha mema na kukataza mabaya. Jambo hili limedhulumiwa katika pande zote mbili, kutolewa fatwa na hata katika kutekelezwa...”

total: 4 | displaying: 1 - 4

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf