Kuchangamkia Fursa za Kheri:

| |times read : 428
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

 Kuchangamkia Fursa za Kheri:

Hakika umuhimu wa Mwezi wa Rajabu, sio tu unatokana na utukufu wake wenyewe na neema za Mwenyezi Mungu zinazotolewa kwa waja ndani yake, bali zaidi ya hayo, hutokana na kuwa ni mwanzo wa miezi ya ugeni na dhifa ya Mwenyezi Mungu ambayo hukamilika ndani ya mwezi wa Ramadhani. Hivyo ni juu yetu tuziandae nafsi zetu kwa ajili ya kukutana na neema hizi za Mwenyezi Mungu kwa kuzidisha umuhimu, kufanya dhikiri kwa wingi na tuyatathimini mahusiano yetu na Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Tathimini hiyo inaweza kufanyika kwa namna mbalimbali, kwa mfano: matendo mema tuliyokuwa tukiyatenda, basi tudumu nayo na tuendelee kuyafanya kwa uzuri zaidi, na yale ambayo hatukuwa tukiyafanya basi na tuharakie kuyaendea, ama yale tulikuwa tukitekeleza sehemu yake, basi tuyakamilishe. Na iwapo katika ratiba za maisha yetu kutakuwa na upotezaji wa muda wenye thamani kwenye umri wetu katika mambo ambayo hayatatunufaisha Akhera, basi wakati huo ni lazima tujiepushe na jambo hilo, na kuubadilisha kuwa muda wenye manufaa na wenye tija kwa ajili ya matendo mema.