Baadhi ya sura zenye kuchafua jamii

| |times read : 777
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Baadhi ya sura zenye kuchafua jamii

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na kurehemu.

Kwa hakika jamii yetu imefikiwa na baadhi ya sura chafu zenye kupingana kabisa na mafundisho ya dini yetu tukufu, bali hata kupingana na adabu za watu wenye tabia za kibinadamu zilizokuwa bora.

Na kwa bahati mbaya baadhi ya sura na tabia hizo si tu zimekomea katika jamii. Bali kuna hatari ya kuingia katika dimbwi la kueneza maovu ambalo Mwenyezi Mungu ametutahadharisha nalo, endapo tu tutazembea na kusema kwamba mambo hayo yanaambatana na maisha ya mtu fulani au jamii fulani. Kama ambavyo itapeleka hali ya kuogopa kutenda maasi kuondoka katika nyoyo zetu, na yule ambaye atakuwa katika nafsi yake tayari kuna maradhi basi itamsukuma kuyatenda mabaya hayo. Na hivi ndivyo ambavyo itaenea taratibu mpaka kufikia hatua ambayo itakuwa ngumu tena kuweza kukabiliana na mambo au hali hizo.

Hivyo ni wajibu kwa wale watu wenye wivu na jamii zao, hasa wafuasi wa viongozi wa juu wa kidini (Marajii) si tu kuepuka mambo haya, bali kuweza kuyasafisha katika jamii kwa kutumia njia za hekima na mawaidha yaliyo bora, ikiwa ni katika kushikamana na faradhi tukufu ya kuamrisha mema na kukata za mabaya, ambayo Imamu Ally as katika kuisifia anasema “....Ni katika faradhi za juu na zenye sharafu na utukufu mkubwa...”.

Na tuweze kushikama sisi kwa sisi katika hili, ikiwa ni katika kufanyia kazi aya ya Mwenyezi Mungu aliposema

 “....Na Saidianeni katika mema na kumcha Mungu, na wala msisaidiane katika machafu na uadui...” (Surat maida aya 2).

Kama ambavyo tunatakiwa kuungana katika kutambua hizi hali chafuzi pamoja na kufikisha ujumbe huu mtukufu, ili kuweza kuizindua jamii, kuinasihi, na kuiongoza. Na pia kuweza kuwatukuza watu ambao wanafanyia kazi ujumbe huu katika kujaribu kubadili mitazamo. Mwenyezi Mungu anasema “...Na katika nyinyi kuwe na watu ambao wanalingania kuelekea mambo ya kheri,  wanaamrisha mema na kukataza mabaya...”  (Surat Al Imran aya 104)

Mambo hayo chafuzi ni pamoja na:

1.   Baadhi ya sehemu za kujirembea kina mama au hata sehemu za kibishara nyinginezo kubandika na kuweka picha au michoro ya wanawake ambao wapo katika sura ambazo haziendani na sheria.

Sasa  ni juu yetu kuweza kuwapa ushauri hawa watu kuweza kuzitoa picha hizi, au kuweka nyingine ambazo hazitapingana na heshima ya jamii kiujumla.

2.   Uwepo wa baadhi za hafla na mikusanyiko ya harusi ambayo hukusanya wanawake na wanaume, na kisha kuwepo na baadhi ya mambo ya haramu kama vile muziki na kucheza, au wanawake kuvaa nguo za nusu uchi kwa hoja ya kwamba wakati mwingine wanakuwa katika vikao mahususi vya wanawake.

Bila kujua kwamba ni katika mambo ambayo yanaweza kuleta fitina na uchochezi endapo hao hao wanawake wakaamua kuwahadihithia  waume zao kunako maumbile ambayo wanawake wenzao wanayo,  kwanza haya ni katika mambo ambayo Maasumina wamekataza kabisa.

3.   Baadhi ya vibanda vya kahawa, kumekuwa na ada za kubadilishana baadhi ya majarida au video zisizo na maadili. Au wakati mwingine huzalikana mahusiano ambayo si ya kisheria na hata kupelekea mambo ya madawa ya kulevya wakati mwingine.

4.   Jambo la baadhi ya mawalii wa mwanamke kuweka kiwango kikubwa cha mahari pale binti yao anapochumbiwa, kiasi kwamba inakuwa ngumu kwa kijana mwoaji.

Pamoja na kwamba wazazi au mawalii wa binti wanakubali kwamba kijana ni mwenye adabu nzuri na mwenye uwezo wa kumfanya binti yao akawa na furaha na kuhifadhi karama zake, lakini bado unakuta wanabakia katika ada na tabia au mambo haya ambayo hayana thamani yeyote. Na jambo hili ni katika mambo ambayo k=huzuia kwa kiasi kikubwa sana utimiaji wa sunna adhimu ya ndoa, kama ambavyo pia ni upingaji wa wazi kabisa wa usia uliopokelewa kutoka kwa Maasumina as. Imepokelewa kutoka kwao wakisema :

“...Endapo mtajiwa na ambaye akili na dini yake vitawaridhisha, basi muozesheni, na kama hamtafanya hivyo basi fitina na uharibifu mkubwa utatokea katika ardhi...”

5.   Ada ya baadhi ya masayyidi (ambao nasaba zao zinafika kwa Mtume saww), Inshallah Mwenyezi Mungu azidishe utukufu wao, ambao wao katika kumchumbia mtoto wao wanaweka sharti la kwamba ni lazima na wewe uwe unatokana na kizazi cha Mtume.

Tumejaribu kubainisha kwa kirefu zaidi katika kupinga ada hii yenye nia ya kuleta dhulma, kwa maana mabinti wenye asili na nasaba ya Mtume wananyimwa haki yao ya maisha ya ndoa kwa kuweka sharti la wao kuolewa tu na wenye asili ya Kisayyidi.

Sheikh Muhammd Yaaqubiy

Ramadhani 7 mwaka 1437