Hukumu ya funga ya Ramadhani katika kipindi cha mitihani

| |times read : 357
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Hukumu ya funga ya Ramadhani katika kipindi cha mitihani

Swali:

Salam alaykum Warahmatullah

Sisi ni wanafunzi wa kiume na kike, na Wizara ya elimu imepitisha kanuni ya kwamba mitihani ya mwaka huu itaangukia katika masiku ya Ramadhani, na kutokana na ugumu wa funga katika masiku haya ya joto, ambapo itatufanya kushindwa kurejea masomo yetu kwa ajili ya mitihani ambayo ndio itaamua mwelekeo wa maisha yetu, je, mnaturuhusu kufuturu katika masiku haya ya dharura?, na endapo hatutakuwa na ruhusa ya kufuturu na sisi kwa makusudi tukafuturu, je hukumu yetu ni ipi?

Jawabu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu (swt)

Kwa mwenye kuwa na uwezo wa kufunga na kupangilia muda wake wa masomo kiasi kwamba haitamdhuru katika masomo na mustakbali wake, kama vile aamue kusoma mchana na karibuni na alfajiri basi ni lazima afunge, kwani kwa njia hii pia wengi wamefanikiwa na kufaulu pia.

Na kama mtu atataka kufuturu ili iweze kuwa rahisi zaidi kwake, basi kuna njia ya kisheria ya kufanya hivyo, nayo ni kusafiri kila siku kwa gari masafa ya kilomita 22, ambapo ataruhusiwa kula na kisha kurejea nyumbani kwa ajili ya masomo, na kama mpo kundi pia inawezekana kukodisha gari kwa ajili ya kazi hii kama ambavyo mnakodisha kwa ajili ya kwenda na kurudi mashuleni.

Ama kufuturu kwa makusudi bila ya kuwa na udhuru haifai, ila itakapotokea amefunga kwa kudhania kuwa ataweza, lakini akajikuta imemuwia ngumu na hakuwa na uwezo wa kusafiri basi anaruhusiwa kula au kunywa kiwango hitajika tu na si kujiachia kabisa, na kisha hiyo siku atailipa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Ayatollah Muhammad Yaaqubiy

18 Jamadul Akhar 1436