Mwanzo | | Maswali ya Kisheria
Maswali ya Kisheria

Shiriki swali

Hukumu ya kula kuku katika miji isiyo ya Kiislamu

Swali:

    Ni ipi kuhumu ya kula kuku katika miji isiyo ya Kiislamu, huku nikiwa najua kabisa kwamba ninayekula kwake ni Mwislamu na ananiambia kuwa kuku huyu amechinjwa kwa njia ya Kiislamu katika mji huo, je, nijengee usahihi na uhalali wa huyu kuku au hapana?.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Kama utapata yakini kutokana na maneno yake basi hakuna shida.

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu ya kubakia katika kuwafuata Marajii waliopita, pamoja na kufanyia kazi Ihtiyat za wajibu

Swali:

    Kwako Ayatollah Sheikh Mohammad Yaaqubiy, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako.

Tunaomba fatwa yako katika hili na Mwenyezi Mungu atwalipa, Je, mnaruhusu mtu kubakia katika kumfuata Ustadh Sayyid Al Khui (ra) na maulama wengine waliopita?.

Na je inawezekana mtu kumrejea mwingine asiyekuwa wewe katika mambo ya ihtiyat za wajibu?.

                                    Kikundi cha wenye kumfuata Sayyid Al Khui (ra). 

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Sisi tunaruhusu kwa waliokuwa wakimfuata Sayyid Khui na Shahid Sadr (wote wawili) kubakia katika kutendea kazi risala zao, lakini katika maswala ambayo yanatokea zama hizi pamoja na yale ambayo yanajulikana kabisa tofauti zake basi ni lazima warejee kwangu. Na idhini hii itabakia mpaka pale tutakapotoa tamko lingine kwa uwezo wa Mungu.

Pia sisi tunamlazimisha mtu kufanyia kazi Ihtiyat za wajibu zilizotajwa katika vitabu. lakini itakapokuwa kuna tatizo na ikawa mtu anataka ufafanuzi zaidi basi aturejee, maana huenda lile ambalo tunaruhusu arejee kwa wengine ikawa ni katika mambo ambayo yanatakiwa kufuata mwenye elimu zaidi, kwani si kila mambo ya ihtiyat za wajibu inawezekana kurejea kwa mwingine.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu ya kutukana baadhi ya alama za madhehebu za Kisuni.

Swali:

 Ilikuwa ni katika siku ya kukumbuka kifo cha Imamu Muhammad Jawad (as), ambapo kundi la vijana lilitoka huku wakiwa wanatukana baadhi ya alama za ndugu zetu Masuni, ni upi msimamo wenu katika jambo hili?.

Jawabu:

Kwanza huu ni ujinga na uumbavu ambao kwa namna yeyote ile hauwezi kunasibishwa na mafunzo ya Ahlu Bayt (as), na naona kabisa kuna umuhimu wa kuwepo vikundi maalumu vyenye kuelekeza watu kama hawa uwepo wa fitina hizi. Na tumeshaashiria hapo mwanzo tulipokuwa tunazungumzia (Mbinu za kishetani tulizoandaliwa) na tukawaonya watu kunako hilo.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

                                                                      7 Dhul Hijja 1434

Shiriki swali

Hukumu ya gemu la Clash of Clans

Swali:

Katika masiku ya karibuni kumeenea sana mchezo wa simu za kisasa na kompyuta mpakato kwa jina la (Clash Of Clan), na umetokea kpoteza mno muda wa vijana na hata kupelekea baadhi yao kuuziana kwa bei za juu mno. Mchezo huu umesimamia katika kuunda majeshi na miji na kisha kushambuliana kwa ajili ya kupata pointi, na kila ambapo pointi za mji fulani zinapanda basi ndivyo ambavyo bei yake huwa juu. Na kama mnavyotambua ni kwamba michezo mingi ya sasa huwa imetengenezwa kwa lengo la kupandikiza uadui katika nyoyo za watoto na vijana, ukiongezea kutekwa na michezo hii kwa muda mrefu mno, iwe majumbani au hata maukumbi ya michezo kiasi kwamba maadili na tabia za vijana na watoto yanaathirika kwa kiwango kikubwa mno.

Je, mna ruhusu watu kucheza na kuingia katika kumbi na hii michezo?.

Tunaomba mwomgozo na Mwenyezi Mungu atawalipa.

 

Jawabu:

Baada ya kuchunguza na kufuatilia tumekuta kwamba katika mchezo huu kuna mambo mengi ambayo yanapelekea kushiriki uchezaji wake, na tuna mengi sana ambayo tumeyaongea tangu mwaka 2003 katika kuelezea hatari za michezo hii katika akili za watu, jamii, tabia, dini na hata kiuchumi, na hili peke yake linatosha kuwa kigezo cha kuzuia.

Hivyo tunawashauri wakuu na wasimamizi kuweza kuwadhibiti watoto wao na mienendo yao, kama ambavyo tunaomba wenye mamlaka husika waweze kuchukua hatua zuizi kwa hizi sehemu na kumbi za hii michezo, bila ya kuangalia kwamba zinaingiza pesa. Na hii ni kwa ajili ya kuokoa kizazi cha watoto wetu, na Mwenyezi Mungu atatusaidia.

Ayatollah Muhammad Yaaqubiy

8 Rabiul Thani 1437H

Shiriki swali

Kufanya ibada bila kuzingatia hijabu.

Swali:

 Ni miaka 15 sasa, naswali na kufunga. Ila katika muda wote huu si mwenye kuzingatia kuvaa hijabu pamoja na kuwa tangu nizaliwe nimekuwa ni mwenye mapenzi makubwa ya kuvaa na kuwa kiigizo chema kwa watoto wangu katika swala la kuvaa hijabu. Nifanye nini ili imani yangu iwe thabiti, ukizingatia mama yangu siku zote anasimamia swala la mimi kutovaa hijabu?.

Jawabu:

Kwanza kabisa itikadi yako ya kuwa hijabu  ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni hatua kubwa, kwa sababu amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu hazifai kuachwa. “...Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiichupe....”.

Na katika hilo wala si kumkosea adabu mama yako, kwa sababu ni kosa lake la kutoshikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu ya wanandoa kukubaliana kuzuia mimba.

Swali:

    Je, inafaa kwa wanandoa kukubaliana kuzuia mimba hata kama itakuwa tayari Mwenyezi Mungu ameshawabariki watoto?.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Inafaa kufanya hivyo kwa hatua ya kwanza, ila tu njia zitakazotumika ni lazima ziwe njia za halali kama vile kutomwaga mbegu ndani ya kizazi. Ama kufunga kabisa kizazi haifai kwani hiyo inahesabika ni kukatisha utendaji kazi wa kiungo cha mwili.

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu ya daktari wa Meno

Swali:

      Mtu ametoka kutibu jino lake  na ameambiwa na Daktari kwamba asile na anywe vimiminika tu, jambo ambalo linamfanya kuwa dhaifu na kushindwa kufunga, sasa je, anaweza kuachia funga?.

Jawabu:

                                  Kwa jina la Mwenyezi Mungu

             Ikiwa kufunga kwake kutamuweka katika madhara basi anaruhusiwa kufungua, ila baadae atazilipa.

 

                                 Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

Shiriki swali

Funga siku ya shaka

Swali:

      Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya shaka, siku ambayo hatujui kuwa inakamilisha mwezi wa Shaabani au ni tarehe mosi Ramadhani, hasa ikiwa hatuna uhakika wa kuandama kwa mwezi.

Jawabu:

             Kufunga siku kama hii kwa anuani ya kuwa ni Ramadhani si sahihi na batili, na hata kutokujua unanuia nini pia ni batili, kwani lazima ujue kuwa unafunga Shaabani ambayo ni Suna, au Ramadhani ambayo kwa hapa si sahihi. Ila unaweza kuifunga kwa anuani ya kulipiza yaliyo katika dhima yako, na hii itajitosheleza itakapokuja bainika kwamba ni kweli ilikuwa Ramadhani.

                   Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

Shiriki swali

Hukumu ya Mafuta yanayotumika kulainisha uso

Swali:

      Kutokana na hali ya baridi watu huwa wanatumia mafuta kwa ajili ya kulainisha ngozi zao, na hali hii huwa ni kwa wingi na endelevu, sasa vipi mtu akawa anataka kuchukua udhu huku akiwa anajua kabisa kwamba masaa machache kabla alitumia mafuta?, je achukue udhu hivyohivyo au ni lazima kwanza aondoe mafuta yote?.

Jawabu:

             Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma na mwenye kurehemu.

Ikiwa ambayo yamebakia ni mafuta ambayo hayazuii kufika kwa maji katika viungo vya udhu basi hakuna tatizo, lakini kama itakuwa yaliyobakia ni ukungu mzito basi ni lazima autoe kwanza.

                   Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

 

Shiriki swali

Hukumu ya wazazi wenye kuzuia watoto kufunga

Swali:

      Ni ipi hukumu ya wazazi ambao wanazuia  kufunga watoto wao ambao wameshafikia umri kwa kulazimikiwa na sheria, kwa hoja ya kwamba bado ni wadogo na hawataweza kufunga. Na watoto wana majukumu gani katika hili?.

Jawabu:

             Kitendo hichi cha wazazi kwanza si sahihi na ni kinyume na uchamungu, kama ambavyo pia ni kuwazembesha watoto mambo ya dini. Bali inatakiwa wazazi wawe kinyume chake, wawatie moyo na kuwapa mafunzo watoto wao kabla hata ya kubalehe, ili iwe rahisi kwao watakapofikia balehe.

Ama watoto wao ni lazima wafunge, kwani hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na ikitokea wamelazimishwa kula basi itabidi walipe baadae. Ila kama itakuwa kinachopelekea kulazimishwa kula ni jambo la kweli na lenye madhara basi hakuna ulazima wa kufunga kiasi kwamba wakaingia katika matatizo.

                   Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

1 2 3 4 5
total: 41 | displaying: 31 - 40

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf