Kufanya ibada bila kuzingatia hijabu.
Kufanya ibada bila kuzingatia hijabu.
Swali:
Ni miaka 15 sasa, naswali na kufunga. Ila katika muda wote huu si mwenye kuzingatia kuvaa hijabu pamoja na kuwa tangu nizaliwe nimekuwa ni mwenye mapenzi makubwa ya kuvaa na kuwa kiigizo chema kwa watoto wangu katika swala la kuvaa hijabu. Nifanye nini ili imani yangu iwe thabiti, ukizingatia mama yangu siku zote anasimamia swala la mimi kutovaa hijabu?.
Jawabu:
Kwanza kabisa itikadi yako ya kuwa hijabu ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni hatua kubwa, kwa sababu amri na makatazo ya Mwenyezi Mungu hazifai kuachwa. “...Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu basi msiichupe....”.
Na katika hilo wala si kumkosea adabu mama yako, kwa sababu ni kosa lake la kutoshikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu.
Ayatollah Mohammad Yaaqubiy