Kurejesha Heshima ya Umma wa Kusoma na Kalamu:

| |times read : 778
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kurejesha Heshima ya Umma wa Kusoma na Kalamu:

Ni wajibu wetu tuirejeshe heshima yetu na tuwe kweli ni Umma wa Kusoma na Kitabu. Tuliongoze gurudumu la mwamko wa kitamaduni kwa wote na tuhimize kusoma vitabu kwa namna mbalimbali na kuvipa umuhimu. Tusambaze vitabu, tuwashawishi watu kusoma na kubuni njia tofauti zitakazoinua kiwango cha utamaduni kwa watu kupitia kueneza maonyesho ya vitabu, kuvifanya vipatikane kwa bei nafuu, kuvichapisha katika maumbile yenye kuwavutia wasomaji, kurahisisha uandishi wake na kutofautisha maudhui zake. Tuvifanye kuwa ni vitabu  vyenye kuzungumzia mahitaji jamii, matatizo na matarajio yake, visaidie katika kuijenga shakhsia ya mwanadamu, na viwekwe katika ukubwa mbalimbali, kuanzia vile vyenye juzuu nyingi hadi vile vyenye juzuu moja, vijitabu, majarida na makala fupi. Ni juu yetu tuendelee kusoma ili tuwe Umma hai, wenye tamaduni na ulioendelea. Ni wajibu wa kila mtu asome ali awe mwandamu wa kweli, kama ambavyo ni lazima tusome ili kumridhisha Mwenyezi Mungu aliyetukuka na mtume wake (s.a.w.w.) na mawalii watukufu, na tunatakiwa kuitika wito wa Mwenyezi Mungu atuitapo kwenye jambo la litupalo uhai. Tusome ili tuishi maisha ya upendo, furaha na utukafu.