Walebanon na kushikamana kwao

| |times read : 699
Walebanon na kushikamana kwao
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na mwenye kurehemu

Walebanon na kushikamana kwao

Pamoja na uwepo wa mambo ambayo Wairaq wanakabiliana nayo, bado SAyatollah Sheikh Yaaqubiy hakuwa nyuma katika kuzungumzia kadhia za Walebanon ambao wanakabiliana mno na Israel adui mwenye kuungwa mkono na nchi zote za kimabavu ulimwengu, hasa ukizingatia hali ya udhaifu na unyonge inayopatikana katika nchi nyingi za Kiarabu. Adui ambao wamevamia na kuacha athari kubwa mno katika ardhi pamoja na ufisadi.

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqubiy amewaomba wananchi waumini wa Lebanon kuweza kusimamisha baadhi ya harakati zenye kuashiria mshikamano kama vile kuungana kwa pamoja katika siku ya Ijumaa ya tarehe 25 Jumadul Thani sawa na tarehe 22 mwezi wa 7 mwaka 2006 kuonyesha kuchoshwa kwao na hizi nguvu zenye kukusanyika dhidi yao,  kwa maana hii ndiyo nguvu ya mwisho kabisa kwa kila taifa lenye kudhulumiwa kama vile Lebanon, Iraq na watu wote ulimwenguni.

Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kurehemu.