NI VIPI TUTARUDI KUIHUISHA NAFASI YA QUR’ANI?

| |times read : 782
 • Post on Facebook
 • Share on WhatsApp
 • Share on Telegram
 • Twitter
 • Tumblr
 • Share on Pinterest
 • Share on Instagram
 • pdf
 • Print version
 • save

NI VIPI TUTARUDI KUIHUISHA NAFASI YA QUR’ANI?

Nirudi kwenye swali nililouliza kwamba ni vipi tutaweza kuirudisha Qur’ani kwenye maisha na na vipi tunaweza kufaidika nayo? Hakika makundi mawili ndio wanaobeba jukumu hilo: kundi la kwanza ni jamii, na kundi la pili ni hauza (vyuo vya dini) ambayo ndio alama ya ufahamu na uelewa wa Umma, ndio fikra yake na kiwango chake cha kidini. Hapo nyuma tulisema kwamba wadhifa mkubwa unaosimamiwa na Hauza katika jamii ni kuipa mafunzo ya Qur’ani, mitazamo na miono yake, maadili na Imani yake, mambo ambayo tumeashiria baadhi yake huko nyuma, kwa ufahamu sahihi na safi kama itakavyo Qur’ani, na kwa mfumo unaoendana na nafasi yake kuwa huwa hai katika maisha ya Umma, na hili kutimia kwa njia mbalimbali kama vile: mimbari za Imamu Hussain (a.s), mihadhara, mukutano, khutba za sala ya Ijumaa na Jamaa, vitabu, majarida na mfano wa hivyo.

       Isipokuwa kabla ya hayo ni lazima kuirudisha Qur’ani kwenye mitaala ya masomo kihauza, na hili litatimia kwa namna mbili:

Yakwanza: kuirudisha kwenye masomo ya awali, yaani masomo ya kiwango cha Muqadimati na Sutuhu, ambapo katika hatua hizi inabidi watoe mitaala ijayo[1]:

1.       Kuhifadhi, kusoma Qur’ani Tukufu na kuidhibiti kwa shakli kwa mujibu wa kanuni za lugha ya Kiarabu, na kuzisoma kwa umadhbuti kanuni za Tajuwidi zilizo ndani ya sheria.

2.       Tafsiri kwa ufupi ya maneno, walau kwa mfumo wa kufafanua maana za misamiati kama ilivyo katika Tafsiri ya Shibr na mfano wake, ile mwanafunzi apate fikra za ujumla kuhusu maana za Qur’ani.

3.       Kusoma Uloomul Qur’an, na kitabu bora katika hili ni (Al-Bayaan) au (Muqaddamatu Kitabil A’laaur Rahman kilichochapishwa mwanzoni mwa Tafsir Shibr.

4.       Kufanya mashindano katika elimu mbalimbali zinazohusu Qur’ani na kuandaa zawadi kwa ajili ya washindi na waliowapita wengine.

Yapili: Masomo ya juu, na hili hutimia katika hatua zifuatazo:

 1. Kufungua malango wa kubobea katika masomo ya Qur’ani, na mda muwafaka zaidi wa hilo ni baada ya kukamilisha masomo ya levo ya juu (As-Sutuhul Ulyah) kiasi kwamba mwanafunzi anayebobea huandaliwa mtaala maalumu kwa ajili yake, na inawezekana kunufaika na baadhi ya vitabu vilivyopo baada ya kufanyiwa mtihani maalumu ili kubaini uwezo wa mwanafunzi anayetaka kubobea katika sehemu hii na kutumia muda wake mwingi kwa ajili masmo haya ikiwa ni pamoja kukusanya vyanzo zinavyohusiana na taaluma ile, ili mwanafunzi huyo aje kuwa mwalimu, au mfasiri au mtafiti wa masuala ya Qur’ani.
 2. Kusoma tafsiri ya Qur’ani kwa kina, ima Qur’ani yote au baadhi ya aya na baadi ya sehemu zilizochaguliwa kwa lengo maalumu, inaweza kuchaguliwa tafsiri moja ikawa kama kitabu cha kusomea, kiasi kwamba mkufunzi hukisherehesha, hutoa maoni yake, huongeza maarifa yanayofaa kutoka kwenye vitabu vingine vya tafsiri na kutoka kwenye vyanzo vinginevyo, na kwa mtazamo wangu mvinyu naona kuwa vyanzo hivi viwili ni bora zaidi, ambavyo ni: Al-Miizan na Fii Dhilaalil Qur’an, kwa sababu kila kimojawapo kila mlengo wake maalumu katika tafsiri unaotofautiana na mlengo wa kingine, milengo ambayo haifahamu isipokuwa yule aliyevisoma vitabu hivyo.
 3. Kuwekwe mitaala ya masomo ya maarifa ya Qur’ani, miono na mitazamo ya Qur’ani, tafiti na falsafa ya Qur’ani juu ya uwepo na maisha, baada ya mwanafunzi kujifunza tafsiri kwa ufupi ya maneno ya Qur’ani na kuyasoma hapo kabla. Na yote haya hupatikana kwa kuzidurusu aya za Qur’ani kimaudhui na si kwa njia ya kusoma ya aya mojo kama ilivyozoeleka, hata kama kufanya hivyo ndio msingi wa hayo. Katika kitabu changu nilichokiita (Madkhal Ilaa Tafsiiril Qur’an) ambacho ni kitabu cha kinafaa kuwa utangulizi wa maudhui hii, nilijaribu kuilinganisha mifumo hii hii miwili.

       Katika mitaala inabidi kuzingatiwe zile maudhui za kielemu, yaani zile ambazo zina uhalizi katika maisha, sawasawa kwa upande wa Imani, au maadili au fikra. Kwa mfano ikawa na maudhui kama vile: Taquwa (Uchamungu), subira, fiqihi, tauhidi, uimamu, utawala (wilayah), shetani, siku ya marejeo, jamii ya kiislamu, mambi yanayoijenga nay ale yanayoibomoa, matarajio na matumaini, mawaidha na mazingatio, suna na kanuni za Mwenyezi Mungu kwa umati na jamii, na kuendelea, wakati huo bila shaka fikra zetu nyingi zitabadilika, kwa sababu maana za maneno ya Qur’ani zilizo zoweleka leo hii haziendani ufahamu zahihi wa Qur’ani kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa kwenye Qura’ni, na sababu yake ni mrundikano wa vumbi la taawili na kutafsiri Qur’ani kwa rai binafsi, kuyafadhilisha matamanio na kufuata chuki, lakini pia mashambulizi ya maadui wa Qur’ani na sababu nyinginezo nyingi. [1]. Mheshimiwa sheikh ameyaingiza masomo haya katika mitaala ya masomo ya Chuo Kikuu cha kidini cha Sadr anachokisimamia.