Magharibi ichukue funzo kutokana na hali ya ukosefu wa amani Ufaransa.
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na mwenye kurehemu
Magharibi ichukue funzo kutokana na hali ya ukosefu wa amani Ufaransa.
Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqubiy, amezitaka nchi za Magharibi kujifunza na kuchukua mazingatio kutokana na yanayoendelea nchini Ufaransa kwa kipindi kipatacho wiki tatu sasa, hali ambayo imepelekea mpaka nchi hiyo kutangaza hali ya hatari, jambo ambalo limezua mtafaruku mkubwa kwa raia na kudhania kwamba ni hali ya vita imeingia.
Hali hii nchini Ufaransa imeonyesha kwa kiwango kikubwa mipingano iliyopo katika jamii za kimagharibi, pamoja na matabaka, kutokuwepo kwa usawa, viongozi wa kisiasa kutofanyia kazi maneno yao katika kuwaridhisha raia, viongozi hao pia kuchukua maamuzi mabaya pasi na kuwa na sababu, mfano wake ni kitendo cha kuzuia kwao hijabu mashuleni , sasa mambo haya yote yamepelekea watu kuhifadhi hasira zao na pale ambapo inapatikana fursa ya kutekeleza yaliyo nyoyoni basi hutumia ipasavyo. Na ndio unaona jambo hili limeweza kuvuka mpaka kuelekea nchi nyingine kama vile Ujerumani, Ubelgiji, Uholanzi na Italia.
Aidha wachambuzi mbalimbali wa Kimagharibi wameonyesha hofu yao kunako nchi hizi kushindwa kutatua majanga haya ya jamii zao, na kujikuta wakitumia njia za askari bila ya kuangalia asili na chimbuko la tatizo. Jambo ambalo limepelekea mpaka baadhi ya nchi za Kimagharibi kukiri kuwa mustakabali mzuri utakuwa i kwa nchi za Kiislamu ambazo zinajipamba na misingi bora ya kijamii na adabu njema na mifano bora katika nyanja ya ubinadamu (kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu vimenukuu).
Tunamshukuru sana Mungu kwa kuweza kutuongoza katika dini yake.
· Hii imesambazwa katika jarida la Sadiqin la tarehe 28 shawwal 1426 sawa na tarehe 1 /12/2005, nambari 34 ukurasa wake wa mwanzo kabisa.