HATUA ZA KIMATENDO KATIKA ARUBAINI YA FARAJA

| |times read : 942
HATUA ZA KIMATENDO KATIKA ARUBAINI YA FARAJA
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

HATUA ZA KIMATENDO KATIKA ARUBAINI YA FARAJA

       Marjii wa Dini, Samahat Sheikh Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) amesisitiza juu ya udharura wa kufanya kila jambo linaloweza kuingiza furaha katika moyo wa Imamu Mahdi (sala na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) na linalo sababisha kuipata radhi yake na kujiweka karibu naye, na kuharakisha kudhihiri kwake na kuiandaa siku yake iliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikiwa ni kukamilisha vilio vya mamilioni ya watu wakifanya maombi na dua kwa Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri walii wake mtukufu na hoja wake kwa waja wake (roho za walimwengu ziwe fidia yake), kwakuwa mamilioni ya watu kupaza sauti zao kwa ajili ya ombi moja tena katika masiku ya Mwenyezi Mungu, ombi hilo linatarajiwa kutorejeshwa. Na katika mlengo huo Samahat Marjii ametaja nukta kadhaa:

1.  Kuweka upamoja wa kimungu:

{وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ}

(Naye yu pamoja nanyi popote mlipo) [Surat Al-Hadid:4]. Na jambo la kwanza katika umoja huo ni kujizuia na maasi ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika, na kuuhisi msaada wake, huruma yake, upole wake, ukuruba wake na mengineyo tuliyoyataja katika kuitafsiri aya hiyo1.

2. kushikamana na sala na kuitekeleza ndani ya wakati wake kwa kadiri inavyo wezekana, na inapendeza ikiswaliwa kwa jamaa katika misikiti uwezekano huo ukiwepo.

3. kuachana na ikhitilafu na migogoro na kujiepusha kutupiana kauli chafu na kushushiana heshima na kila aina ya maongezi mabaya. Na kujitahidi kutatua matatizo kwa hekima na busara kwa kufuata yamridhishayo Mwenyezi Mungu.

4. kuwatendea wema wazazi wawili, kuunga udugu, kuishi vyema na majirani na kuamiliana na watu wote kwa maadili mema.

5. kuzuia mikono na visivyo vya halali, kuhifadhi ulimi, tumbo, macho na kuyadhibiti matamanio na hisia.

6. kujifunza dini na kujumuika na makundi yenye weledi wa mambo na wasomi wa dini kwa kila namna, sawa sawa kwa kushiriki kwenye vikao vyao moja kwa moja au kwa njia za mitandao.

7. kujitahidi kukidhi haja za watu na kuingiza furaha katika nyoyo zao na kujiepusha kuwaudhi.

8. Kuwasaidia wahitaji na hasa wale wasio na uwezo, kuwatunza mayatima kimaisha, kimalezi na kielimu na kuwaozesha vijana wasio na uwezo kwa kutumia mali zijulikanazo kuwa ni “haki za kisheria” –mfano: zaka, khumsi nk- au kwa misaada.

9. kuwaelimisha watu na kuwaongoza kwenye mambo yanaijenga dunia na akhera yao, na kuwaondolea shubuhati ikiwa ni pamoja kujibu maswali yao.

10. kuwa na nia safi na ikhlasi katika kazi au wadhifa ulionao, na kuifanya kwa umakini na sio kufanya upuuzi.

11. Kujiepusha na kila aina ya upumbazo na upuuzi, na pale nafsi inapohitajia mapumziko na pumbazo, basi si viabaya kuipa kwa kiwango cha haja.

12. kuhuisha minasaba ya kidini na kushiriki katika minasaba hiyo.

13. kusoma kile kinachowezekana katika Qur’ani walau robo ya juzuu kwa siku.

14. kufanya matendo ya suna na hasa sala ya usiku (tahajudi) walau rakaa moja, kubakia katika hali ya usafi na udhu kwa muda mrefu bila kuikalisha nafsi au kuathiri majukumu mengine.

15. kumuombea dua Imamu wa zama hizi Al-hojjah (sala na amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) kwa kusoma dual-hojjah: [allahumma kun liwaliyyika...]  na dua: [ya man tuhallu bihi u’qadul- makaarihi...] na kusoma ziyaarat Ashuraa, na kutoa sadaka kwa niaba ya Imamu (amani iwe juu yake) na kuyafanya matendo yote yanayofanywa na watu binafsi, au makundi au taasisi kwa jina la Imamu ili kueneza utajo wake wenye baraka, na kukuza mahusiano ya watu kwa Imam (amani iwe juu yake).

       Samahat Marjii (Allah amhifadhi) anasema kuwa mwaka uliopita alitoa muongozo uliokuwa na anwani isemayo: (Arubaini ya faraja... kuanzia Ashuraa kuelekea kwenye Arubaini2, ambapo ilikuwa ni 08/Muharram71441H ambapo aliwataka watu kuyatumia masiku ya Arubaini ya Imamu Hussein (amani iwe juu yeke) yanayoa anzia siku ya Ashuraa mpaka ziara ya Arubaini, aliwataka wamlilie Mwenyezi Mungi Mtukufu, kunyenyekea kwake na kumtaka msaada ili aturekebishie mambo yetu yaliyoharibika kwa hali yake iliyokuwa nzuri, na kwamba Arubaini ya Imamu Husseini kuwa ni sehemu muwafaka kwa kumlilia na kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kunatokana na kuwa kadhia ya Imamu Husseini ilikuwa na mafungamano ya serikali ya uadilifu wa Mwenyezi Mungu, na kwa sababu dola ya Mwenyezi Mungu inatoa kila kheri na chanzo cha kila nguvu iwapo mikononi mwa waongofu na watenda mema. Na kutokana na maneno ya Imamu Swadiq (amani iwe juu yake):

 (فلما طال على بني إسرائيل العذاب.. ضجّوا وبكوا إلى الله أربعين صباحاً فأوحى الله إلى موسى وهارون أن يخلّصهم من فرعون فحطّ عنهم سبعين ومائة سنة، هكذا أنتم لو فعلتم لفرّج الله عنّا، فأما إذا لم تكونوا فإن الأمر ينتهي إلى منتهاه).

(Pindi adhabu ilipochukua muda mrefu kwa wana wa Israeli... walipaza sauti na wakamlilia Mwenyezi Mungu kwa muda wa siku Arubaini, basi Mwenyezi Mungu akamfunulia nabii Mussa na Haruna kwamba atawaokoa na Firiaun, na hivyo, akawapunguzia miaka mia moja na sabini. Nani ikiwa mtafanya hivyo, basi Mwenyezi Mungu atatufariji, na kama hamkufanya hivyo, basi hakika jambo litaishia kwenye ukomo wake).

       Tumuombe Mwenyezi Mungu atuwafikishe sisi na ninyi kwenye kila jambo liingizalo furaha katika moyo wa Imamu wetu Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yake) na atuwafikishe kujiepusha na yote yaingizayo huzuni na maumivu katika moyo wake mtukufu, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni msikivu wa maombi.

 

Ofisi ya Samahat Marjii wa Dini, sheikh Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi)

14/Muharram/1442H

03/09/2020

 

ـــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ

1 -https://yaqoobi.com/arabic/index.php/5/1/7418.html

2- https://yaqoobi.com/arabic/index.php/news/6978.html