FATWA KUHUSU SHARTI LA CHANJO YA CORONA KWAAJILI YA KUTEKELEZA IBADA YA HIJA

| |times read : 653
FATWA KUHUSU SHARTI LA CHANJO YA CORONA KWAAJILI YA KUTEKELEZA IBADA YA HIJA
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

FATWA KUHUSU SHARTI LA CHANJO YA CORONA KWAAJILI YA KUTEKELEZA IBADA YA HIJA

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU.

AMANI, REHEMA NA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE JUU YENU.

 

      Kulingana na maamuzi ya hivi karibuni, kila mwenye kutaka kutekeleza ibada ya Hija ni lazima achanjwe chonjo ya Corona na athibitishe kuwa amechanjwa ili aruhusiwe kutekeleza ibada ya Hija.

SWALI:

     Je? ni lazima kwa yule ambae vingezo vyote vimetimia vya kutekeleza ibada ya wajibu ya hija (kwa maana ya kwamba ndio hija yake ya kwanza na jina lake limepita katika watakao kwenda kuhiji na ni mtu mwenye uwezo) akubali chanjo, au ni mwenye hiyari kati ya kukubali chanjo ili aruhusiwe kuhiji au asikubali (hasa kutokana na kuenea shaka na wasiwasi juu ya chanjo yenyewe) na ashindwe kufanya Hija.

MWENYEZI MUNGU AKUHIFADHI, AKUSAMEHE MAKOSA YAKO NA AKUPE UMRI MREFU WENYE MANUFAA KWA WAUMINI.

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU.

AMANI, REHEMA NA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE JUU YENU.

      Chanjo dhidi ya magonjwa ya milipuko ni utangulizi wa lazima, hivyo basi ni wajibu kuitekeleza kama ilivyo kuwa wajibu kuandaa hati ya kusafiria, na kama atakuwa na hofu ya kuchwanjwa chanjo maalumu, basi na achukuwe chanjo nyingine isio kuwa na wasiwasi, lakini kama atakuwa na maradhi maalumu au siha na afya yake ni dhaifu kiasi ya kwama chanjo inamadhara makubwa kwake au kuna mlipuko wa maradhi fulani tishio msimu wa Hija (Mwenyezi Mungu atukinge na maradhi), hapo inafaa kuchelewesha Hija mwaka huo na kutokusafiri. Na kama atakuwa katika mazingira ambayo hawezi kabisa kutekeleza Hija hata katika miaka mingine ijayo, anatakiwa amtafute mtu mwingine amlipe kwaajili ya kumfanyia Hija kwa niaba yake, na kama udhuru utaondoka na itatokea mwaka mwingine akawa na uwezo; itamlazimu kutekeleza yeye mwenyewe ibada ya Hija panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

 

MUHAMMAD YAAQUBI

25 SHABANI 1442