JUKUMU LA HAUZA KATIKA KUENDESHA HARAKATI ZA QUR’ANI

| |times read : 812
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

JUKUMU LA HAUZA KATIKA KUENDESHA HARAKATI ZA QUR’ANI

       Na mimi hapa nitataja hadithi moja tu ambayo inabainisha majukumu ya hauza tukufu katika kuiamsha jamii, kuiongoza na kuirekebisha.

       Imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad (saw); ‘alihutubia akamuhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu kisha akataja makundi ya Waislamu akawasifia na akasema; kuna nini kwa watu wasiojifunza kutoka kwa majirani wao na hawafahamu wala hawaelimiki? Ninaapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, (ni lazima) wawafundishe majirani zao, wawafahamishe, wawaelimishe au (niwaombee dua) niwaharakishiwe adhabu ya duniani, kisha (Mtume) akashuka mimbari na akaingia nyumbani kwake. Masahaba wakajiuliza, Mtume alikusudia nini katika maeneo yake? Wakasema, hatujui alikusudia nini labda aliwakusudia Ashaairah (wafuasi) miongoni mwa wasomi na maulama wao, wenye majirani wajinga na wasio na elimu. Kundi miongoni mwa Ashaairah wakakusanyika wakaingia nyumbani kwa Mtume (saw) wakasema; umeitaja jamii fulani miongoni mwa Waislamu kwa kheri kisha ukatutaja sisi kwa shari, tumefanya nini? Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema; (mnatakiwa) kuwafundisha majirani zenu, muwaelimishe na muwaamrishe (mema) na muwakataze (machafu) au nikuharakishieni adhamu hapa duniani. Wakasema, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tupatie muda wa mwaka mmoja, katika muda wa mwaka mmoja, tutawaelimisha na kuwafundisha. Mtume akawapa muda wa mwaka mmoja kisha akasoma aya inayosema: (Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israel kupitia ulimi wa Nabii Daud na Issa mwana wa Maryam (a.s), hayo ni kwa kuwa waliasi na walikuwa wakikiuka sheria. Walikuwa hawakatazani mabaya waliyoyafanya, kwa hakika walikua wakifanya mabaya.)[1]

       Haya ni baadhi ya mapendekezo ambayo nayawasilisha kwa hawza (chuo) tukufu katika uwanja huu na wadhifa shirikishi kwa wote ni kuzingatia kuisoma Qur’ani na kunufaika nayo majira ya usiku na mchana na utapata kufahamu mengi kupitia hadithi tufu inayofuatia. Na wadhifa huu kwa hauza hauwahusu wao pekee, bali tumewahutubu kwa kauli hiyo kutokana udharura wake ulivyo kwao kuliko watu wengine. Lakini jamii yote ina jukumu la kufuata hatua hizi kwa kuzingatia na inavyomfaa kila mtu. (kwa mfano) watu wenye maarifa wataanza kwa kuzo tafsiri nyepesi kama vile tafsiri ya Shobar.

       Ninamnasihi kila Mwislamu kwa kuzingatia tajriba (uzoefu) niliyoitumia mimi, aanze maisha yake pamoja na Qur’ani, aisome katika msahafu wa tafsiri kama tulivyoitaja (ya Shobar), ili aweze kuenzi ufahamu wa misamiati ya aya, wakati wa kusema kwake. Na aendelee na hali hiyo kwa mahitimisho kadhaa hadi aweze kumiliki maarifa jumla ya Qur’ani, kisha anarejea tena kwenye nakala ya msahafu akisoma ndani yake; na kujiendeleza kwa kusoma vitabu vya tafsiri kubwa, kama vile tafsiri ya Al-Mizan sambamba na (kusoma) Qur’ani, huku akisoma vitabu ambavyo vimebainisha maana ya Qur’ani au ambavyo vimeifafanua Qur’ani kwa kuzingatia maudhui, ambapo atapata kuchukua mojawapo kuwa ndio anuani ya uchunguzi wake. Baadaye aitafiti Qur’ani kwa kukusanya aya zote zinazohusiana na anuani husika kisha atoe natija kwa majimui ya malengo ya Qur’ani na nadharia zake- Na mimi hapa nitaazima istilahi hizi za kifikra kwa lengo la kuziliwaza nazo akili sambamba na kuzingatia-maudhui hii ambayo inatakiwa kutatuliwe ndani yake matatizo halisi yanayoikabili jamii sawa sawa iwe tatizo ya kiitikadi, kiakhlaqi, kifikra na kadhalika.

       Na huwenda ikawa ni bora kulifuatilia hilo pamoja na baadhi ya wasomi wakubwa wa hauza tukufu, ili waweze kuwaelekeza na wajibu maswali yao, na wawaongoze kwenye mambo yenye kuwafaa, kwa kuwa jamii na hauza kila kimoja kinamkamilisha mwingine. Kwani hauza inaielekeza jamii, huku jamii nayo ikiiwekea mashinikizo hauza, ili iwe kwenye kiwango cha kubeba majukumu na kiwango cha hitajio la umma, matumaini na mazingatio ya zama ambazo unaishi ndani yake. Wakati huo itawezekana kuainishwa vipengee vya sifa stahiki za hauza, na isiyo hauza na umma utapata kujua ni upande gani ulio sahihi.

       Hakika Qur’ani haiwezi kufahamika uhalisia wa maana yake, hadi pale mwanadamu atakapoichukulia kuwa ni ujumbe ambao anairekebisha nafsi yake, pamoja na watu wanaomzunguka kwa ujumbe huo; na anaweza (kutumia ujumbe huo) kukabiliana na makosa na upotofu unaoikabili jamii ya mwanadamu. Wakati huo ataweza kuishi sawa na mazingira iliyoshuka ndani yake Qur’ani hiyo. Ni hapo ambapo kutafunguliwa milango ya siri zake na haitotosha kuisoma tu au kupata baraka zake, ingawa hayo yana fadhila isiyopingika. Ni suala la dharura (lazima) tutupie macho, moja ya masomo ya Qur’ani kwa mujibu wa historia ya kushuka aya zake, kwa kudondoa baadhi ya nukta zake, ambapo tutapata kunufaika na bahthi (tafiti) zilizo na faida nyingi katika uga wa maarifa ya hatua za Qur’ani katika kurekebisha jamii. Kwa kuzingatia kuwa ilishuka taratibu kwa mujibu wa matukio.

       Hakika ushukaji huu wa taratibu wa Qur’ani uliojiri mbadala wa kushuka mara moja tu, una nafasi yake ya moja kwa moja na taathira tendaji kwenye mazingira iliyoyatatua, kuhusiana na hilo Mwenyezi Mungu anasema: “Na Qur’ani tumeigawanya sehemu mbalimbali ili uwasomee watu kwa kituo, na tumeiteremsha kidogokidogo.” Surat Isra aya ya 106. Na kwa kuwa Qur’ani ni kitabu cha malezi, uongofu na kuhuisha mioyo, hakuna budi ila iteremke taratibu na kwa upole. Izungumzie ponyo inayofaa katika muda mwafaka na kwa uthubutu mwafaka usiopungua au usiozidi, si kabla ya wakati au baada yake. Hivyo ndivyo Qur’ani ilivyoendana na umma huu kwa upole ambapo ghafla ulijikuta (umma) baada ya vipindi virefu vya muda mrefu kwenye kilele cha ubora, ukamilifu, utukufu, izza na nguvu.[1]. Mizanu fi Tafsiril-Qur’ani juzu ya 6 ukurasa wa 84 katika tafsiri ya aya, kutoka kitabu cha Al-Durrul-Manthur.