FIQIHI NA FAQIHI KATIKA MSAMIATI WA QUR’ANI

| |times read : 948
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

FIQIHI NA FAQIHI KATIKA MSAMIATI WA QUR’ANI

Huko nyuma tumezungumzia maana ya Ujahilia katika msamiati wa Qur’ani, tukaelezea sifa za jamii ya kijahilia na njia mbadala za Mungu zilizotolewa na Qur’ani. Na huu ulikuwa ni kama mfano wa maana ya kijamii.

Na sasa nitatoa maana ya Qur’ani ya neno na msamiati wa hauza ambao ni (Fiqihi) ili uwe ni mfano mwingine.  Neno Fiqihi limezoeleka kwetu (wanahauza) kuwa ni elimu ya hukumu za kisheria, wakati masamiti huu wa kiqur’ani ndani ya Qur’ani hutambulika kwa maana ya kumtambua Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Na uhusiani uliopo baina ya maana hizo mbili upo wazi, kwamba zinakutana sehemu na sehemu nyingune hazikutani.

       Kwa mfano katika aya hii:

[فَلَوْلاَ نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوْمَهُمْ إذا رَجَعُواْ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ]

(… lakini kwa nini halitoki kundi katika kila taifa miongoni mwao kujielimisha vema dini  na kuwaonya watu wao watakapowarudia,ili wapate kujihadhari?[1]), sote tunajua kuwa tahadhari na uchamungu havitokani na kuzifahamu hukumu za kisheria, bali chanzo cha tahadhari ni cha kiroho, kinafsi na kiakili kisha ndio hupatikana uchamungu na maarifa moyoni, ambayo ndio humsukuma mtu kwenye kujifunza hukumu za kisheria na kuzifanyia kazi, mwenye unaweza kulijaribu hilo, soma vitabu vya fiqih na uzame ndani yake kuanzia mwanzo hadi mwisho, je utaviona vikiushibisha moyo moyo wako chochote au kukuongezea kuchukua tahadhari na uchamugu? Tumeona mafakihi wangapi waliofahamu maana ya fikihi kwa maana ya kwanza, lakini wamejishughulisha na dunia na wamejitenga mbali kweli na Mwenyezi Mungu?

       Qur’ani inatusimulia mfano wa faqihi huyu ikisema:

       

[وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ الَّذِيَ آتَيْنَاهُ آيَاتِنَا فَانسَلَخَ مِنْهَا فَأَتْبَعَهُ الشَّيْطَانُ فَكَانَ مِنَ الْغَاوِينَ، وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَاهُ بِهَا وَلَكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ فَمَثَلُهُ كَمَثَلِ الْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ذَّلِكَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُواْ بِآيَاتِنَا فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ]

(Na wasome khabari za yule tuliyempa aya zetu, kisha akajivua nazo, na shetani akamfuata na akawa miongoni mwa waliopotea. Na kama tungelitaka tungelimuinua kwazo, lakini yeye akagandamana kwenye ardhi na akafuata matamanio yake. Basi hali yake ni kama hali ya mbwa, ukimpigia kelele anahema au ukimwacha (pia) anahema. Hivyo ndivyo hali ya watu waliokadhibisha Aya zetu, basi simulia hadithi huwenda wakafikiri)[2].

       Na miongoni mwa dalili kwamba maana ya Fiqihi ni kumtambua Mwenyezi Mungu, ni kwamba katika aya tkufu, ameifanya mahala pake kuwa ni moyo ambao ndio sehemu ya maarifa ya kweli ya Mwenyezi Mungu, wakati hukumu za kisheria sehemu yake ni akili, anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

 

[رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ الْخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَى قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لاَ يَفْقَهُونَ]

(Wameridhia kuwa pamoja wanaobakia nyuma, nan yoyo zao zikapigwa muhuri, kwa hiyo hawafahamu)[3], na

[لَهُمْ قُلُوبٌ لاَّ يَفْقَهُونَ بِهَا]

(Nyoyo wanazo lakini hawafamu kwazo)[4], ndio maana aya ikalifanya neno fiqihi, yaana maarifa madhubuti ya Mwenyezi Mungu, na maarifa ya Muumba na siku ya marejio, kuwa ni sababu ya kuongezewa nguvu mara kumi zaidi, pale Mwenyezi Mungu aliposema:

[يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُواْ مِئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّئَةٌ يَغْلِبُواْ أَلْفاً مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لاَّ يَفْقَهُونَ]

(Ewe Nabii! Wahimie walioamini waende vitani, kama wakiwa miongini mwenu ishirini wanaosubiri, watawashinda mia mbili. Na kama wakiwa mia moja miongoni mwenu watawashinda elfu moja katika waliokufuru, kwa sababu wao ni watu wasiofahamu)[5].

Na hadithi tukufu kutoka kwa bwana mtume (s.a.w.w) anatilia mkazo maana hii, alisema:

(ألا أخبركم بالفقيه حقاً؟ من لم يقنط الناس من رحمة الله ولم يؤمنهم من عذاب الله ولم يؤيسهم من روح الله، ولم يرخص في معاصي الله ولم يترك القرآن رغبة عنه إلى غيره، ألا لا خير في علم ليس فيه تفهم، ألا لا خير في قراءة ليس فيها تدبر، ألا لا خير في عبادة ليس فيها تفقه)

(Je, nikuelezeni faqihi na mwanazuoni wa kweli? Ni yule asiyewakatisha watu tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, na wahaaminishi na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wahakatishi tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu, na haruhusu kumuasi Mwenyezi Mungu, na hamwachii mwingine Qur’ani kwa kuichukia. Tambueni kuwa hakuna kheri kwenye elimu isiyo na ufahamu ndani yake, tambueni kuwa hakuna kheri katika usomji usio na mazingatio ndani, tambueni kuwa hakuna kheri katika ibada isiyo na uelewa ndani yake)[6], hivi ndivyo ilivyo katika kitabu cha Al-Wasaail.

Na hadithi hii ina chanzo kingine[7], kama ifuatavyo:

 (فإنه إذا كان يوم القيامة نادى مناد: يا أيها الناس إن أقربكم من الله تعالى مجلساً أشدكم له خوفاً، وإن أحبكم إلى الله أحسنكم عملاً، وإن أعظمكم عند الله نصيباً أعظمكم فيما عنده رغبة، ثم يقول عز وجل: لا أجمع لكم اليوم خزي الدنيا وخزي الآخرة، فيأمر لهم بكراسي فيجلسون عليها، وأقبل عليهم الجبار بوجهه وهو راض عنهم وقد أحسن ثوابهم).

(Kwa hakika itakapokuwa siku ya Kiyama, mnadi atanadi: Enyi watu! Hakika atakayekaa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu ni mwenyekumuogopa zaidi, na hakika mpendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mwenyekutenda mema zaidi, na hakika mwenye fungu kubwa kuliko, ni yule utashi zaidi wa kile kilichoko kwake, kisha atasema Mwenyezi Mungu: Sitakupeni fedheha ya dunia wala fedheha ya Akhera, kisha ataamuru wapewe viti na wataketi juu yake, na Mwenyezi Mungu atawaelekea kwa uso wake hali ya kuwa akiwa radhi nao na akiwa amewalipa thawabu iliyo nzuri kuliko).

       Utaona kuwa sifa za faqihi ni kila kinachmuweka karibu na Mwenyezi Mungu aliyetukuka, imekuja katika hadithi kutoka kwa Amirul muunina (a.s) kuwa alisema:

(كانت الفقهاء والحكماء إذا كاتب بعضهم بعضاً كتبوا ثلاثاً ليس معهن رابعة: من كانت الآخرة همته كفاه الله همه من الدنيا، ومن أصلح سريرته أصلح الله علانيته، ومن أصلح فيما بينه وبين الله عز وجل أصلح الله فيما بينه وبين الناس)

(Wanazuoni  na watu wa hekima walikuwa wanapoandikiana wao kwa wao, huandika mambo matatu, yasiyo na la nne: Yeyote ambaye Akhera itakuwa ndio hima yake, basi Mwenyezi Mungu atamtoshelezea hima yake ya dunia, na yeyote atakayeisuluhisha na kuitakasa siri yake, basi Mwenyezi Mungu ataisulusha dhahiri yake, na mwenyekusuluhisha lile lililopo baina yake na Mwenyezi Mungu aliyetukuka, basi Mwenyezi Mungu atayasuluhisha yaliyo baina yake na watu)[8].

  Na katika hadithi ya kutoka kwa Abul Hassan (a.s) alisema:

(من علامات الفقه الحلم والعلم والصمت، إن الصمت باب من أبواب الحكمة وإن الصمت يكسب المحبة وإنه دليل على كل خير)

(Katika alama za fiqihi ni upole, elimu na ukimya, hakika ukimya ni mlango katika milango ya hekima, na hakika ukimya huleta mapenzi na ni kiashiria cha kila kheri)[9].

       Na inawezekana kuipata maana hii pia kwa kukusanya hadithi hizi mbili: katika kitabu cha Al-Khisaal kutoka kwa mtume (s.a.w.w) alisema:

(صنفان من أمتي إذا صلحا صلحت أمتي وإذا فسدا فسدت أمتي: الأمراء والفقهاء)

(Makundi katika Umma wangu wakisalimika, basi Umma wangu utasalimika, na wakiharibika, basi Umma wangi pia utaharibika: watawala na mafaqihi –wanazuoni-)[10], na katika kitabu cha Wasaail akinukuu kutoka kwenye kitabu cha Al-Amaali, ambapo badala ya wanazuoni ni wasomaji. Tukiiongezea hadithi ijayo katika sifa za wasomaji, tunapata maana iliyotajwa.

       Hivyo basi, katika ya Faqihi kwa msamiati wa Qur’ani na Faqihi kwa mujibu wa maana ya kihauza mahusiano yake ni kuwa zinakutana sehemu na kupishana sehemu nyingine, kwa sababu atu anaweza kuwa faqihi kwa mujibu wa maana ya Qur’ani lakini asiwe faqihi kwa mujibu wa maana ya kihauza,kwani wapo mawalii wengi wa Mwenyezi Mungu wenyekumtambua na wenye karama zilizoshuhuduwa licha ya kuwa walikuwa hawakufikia daraja la juu katika elimu za kihauza, na kinyume chake pia, unamkuta mtu akili yake imesheheni nadharia na fikra za Kiululi, kiakili na masilala za kifiqihi kiasi ambacho utamkuta mjuzi wa zile masiala za ndani, lakni moyo wake ukawa haujajengeka na ukumbusho wa Mwenyezi Mungu, kiasi ukimuuliza suala kidogo tu la malezi ya nafsi na mwenendo mwema wa kueleke kwa Mwenyezi Mungu, na kujisataka nafsi na kuutakasa moyo, basi hubaki amedua na akishangaa, mfano wa mtu huyu sio faqihi kwa mujibu wa maana ya Qur’ani ya neno faqih. Na faqihi aliyekamilika ni yule aliyekusanya maana zote mbili, kama ilivyo kwa wanazuoni wetu watukufu, walifikia kiwango cha juu katika Fiqhi na Usoul na wakawa ni vinara wa kumtambua Mwenyezi Mungu, bila shaka hawa ndio wale waliokusudiwa katika hadithi:

المقدسين (الفقهاء أمناء الرسل)

(Wanazuoni ni waminifu wa mitume)[11], kwa mtazamo huu wa Qur’ani ndivyo tunavyopaswa kuzifahamu hadithi pia, ili maana zake za juu zisitupotee.[1]. Surat At-Tawbah: 122.

[2]. Surat Al-Aa’raaf: 175-176.

[3]. Surat At-Tawbah: 87.

[4]. Surat Al-Aa’raaf: 179.

[5]. Surat Al-Anfaal: 65.

[6]. Biharul Anwaar: 2/49, mlango: sifaatul Ulamaa wa Asnaafuhum, hadithi: 8.

[7]. Madinatul Balaaghah: Uk: 98, kutoka kwenye kitbu cha Al-Ja’fariyaat.

[8]. Al-Khisaal: Uk: 129, mlango: 3.

[9]. Al-Ikhtisaas: 232.

[10]. Chanzo chake imekwishatajwa mwanzo wa kitabu hiki.

[11]. Biharul Anwaar: 2/36, Hadith: 38.