FATWA KUHUSU URAIBU WA MITANDAO YA KIJAMII:
FATWA KUHUSU URAIBU WA MITANDAO YA KIJAMII:
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU.
SAMAHATU AL-MARJIU DINI SHEIKH MUHAMMAD AL-YAAQUB {MUNGU AMUHIFADHI}.
AMANI, REHEMA NA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE JUU YENU.
SWALI:
Tunapo angalia utafiti wa uraibu wa mitadhao ya kijamii tunaona baadhi ya waumini wanatumia wakati mwingi katika mitandao ya kijamii tena kila siku mfululizo kiasi kwamba imefikia kiwangu cha kuchupa mipaka hali ya kuwa yeye mwenyewe halihisi hilo; Je hukumu ya kisheria inasemaje kuhusu hili kwa mujibu wa mtizamo wako?
JIBU:
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU.
AMANI, REHEMA NA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE JUU YENU.
Kwa hakika kutumia wakati mwingi atika mitandao ya kijamii pasina kuwa na udhararu wowote ule wa kiakili kunahesabiwa ni katika mchezo wa batili na upuuzi, na hakika sisi hatukuumbwa kwaajili ya upuuzi, hakima Mwenyezi Mungu ametahadharisha sana juu ya kujishughulisha na michezo ya kipuuzi na kupoteza wakati pasina kuwa na sababu ya msingi. Mwenyezi Mungu amesema: “basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo ahidiwa” suratu Zukhruf: 83, na suratu Maarij: 42. Hivyo basi ni lazima muumini atumie hii mitandao ya kijamii katika mambo yenye faida na matunda, pia anatakiwa atumie wakati wake wa faragha vizuri ili kuipumzisha nafsi yake na asiichoshe, ili aweze kupata nguvu mpya ya kutekeleza majukumu yake.
MUHAMMAD AL-YAAQUM
22 SHABANI 1442