BAADHI YA DESTURI NA SUNA ZINAZOHUSIANA NA USOMAJI WA QUR’ANI
BAADHI YA DESTURI NA SUNA ZINAZOHUSIANA NA USOMAJI WA QUR’ANI
Ninapenda hapa nitaje baadhi ya desturi, mienendo na suna zinazohusiana na usomaji wa Qur’ani kwa kutegemea riwaya tukufu:
1-Ni suna kuhitimisha Qur’ani mara moja kwa kila mwezi na isizidi miezi minne. Yaani kwamba ahitimishe kwa mwaka mmoja mara tatu, isipokuwa ziada ambazo zinatakiwa kuzidisha ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2-Usomaji uwe kwa namna ya uhitimishaji. Yaani kwamba aanze mwanzo wa Qur’ani hadi mwisho wake, na sio usomaji wa sura tofauti hata kama iwe ni kwa kuzingatia umuhimu wake. Bali apitie Qur’ani yote ili aweze kupata baraka zote kama ilivyoelezewa katika hadithi tukufu inayofuata ya: (Muhitimishaji muanzishaji …)[1]
3-Uhitimishaji usadifiane na siku ya Ijumaa na asome wakati wa kuhitimisha Qura’n dua yake maalumu nayo ipo kwenye kitabu cha Al-Sahifatus-Sajjadiyah.
4-Wakati wa kuhitimisha Qur’ani asisimame mwishoni pake, bali aiunganishe moja kwa moja kwa ufunguo wa hitimisho lake mpya angalau aanze kwa surat Al-Fatiha na mwanzo wa aya tano wa surat Al-Baqarah.
5-Awe katika hali ya tohara (usafi wa kimaanawi) na akalie msala huku akiwa ameelekea kibla.
6- Imepokelewa kuhusiana na kauli yake Mwenyezi Mungu inayosema: “Enyi mlioamini! Subirini na shindaneni kusubiri na kuweni makini na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.” Surat Aal Imran aya ya 200, kwamba miongoni mwa watu walio makini, wapo wanaotulia kwenye eneo lao la kusalia wakisubiria kutimia muda wa swala ya faradhi. Hivyo kupata fadhila za umakinifu ni muumini kupitiwa na hali hiyo, nacho ni kipindi cha kusubiria (kutimia) muda wa swala kwa kusoma Qur’ani, na malipo yake yanakuwa makubwa zadi iwapo jambo hilo litafanyika msikitini akisubiria swala ya jamaa.
7- Na imepokewa suna ya kulala ya tohara (usafi wa kimaanawi) na kusoma Qur’ani kabla ya muumini hajalala kwenye kitanda, kuhusiana na suala hilo imepokewa hadithi inayosema: “Atakayepatwa na hali ya kutokwa na udhu na akawa hakutawadha basi amenifanyia tabia mbaya. Na atakayetawadha na akawa hakusali rakaa mbili, atakuwa amenifanyia tabia mbaya na atakayesali rakaa mbili na akawa hajanisalimia, atakuwa amenifanyia tabia mbaya, na atakayenisalimia na kikakosa kumjibu, nitakuwa nimemtendea tabia mbaya na mimi si mlezi wa tabia mbaya.[2]” Na ikiongezewa juu yake suna yenye nguvu kwenye sala ya usiku, suna kujisaidia kabla ya kulala na suna ya kupiga mswaki, tutatoka na majimui ya muhimu nayo ni kwamba kabla ya muumini hajalala kwenye kitanda chake hujisaidia, kupiga (meno) mswaki kisha anatawadha na kusali swala ya usiku, yote au baadhi yake na atekeleze nyingine kabla ya kuchomoza alfajiri. Baadaye atasoma kiasi kidogo cha Qur’ani Tukufu na amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kisomo hicho (kwa ajili yake) na kwa waumini, hapo atakuwa amekusanya suna zote hizo. Ama mtu ambaye anakesha usiku akiangalia vipindi na filamu chafu ambazo zinachosha mishipa yake na kumtwisha mzigo, ataishi katika maisha magumu nay a tabu.
8-Kwa wale wanaoanza usomaji wa Qur’ani uwe kwa tafsiri ya Shobar ambayo inajumuisha faida nyingi. Kwa kuwa kuna nakala ya msahafu mtukufu na ndani yake kuna tafsiri jumla ya maala ya Qur’ani, na hayo ndio tuliyasema kwamba imejumuisha mfumo wa masomo ya awali ya Qur’ani, kama ambavyo ndani yake kuna utangulizi wa elimu za Qur’ani nalo ni somo lingine. Na humo kuna mwambata wa orodha ya matamshi ya Qur’ani kiasi kwamba kila aya utakayotaka kufahamu eneo lake, hupatikana kwa namna hiyo na eneo la neno lolote kutoka humo. Na ndani yake kuna visomo mbalimbali vya maneno ya umoja iwapo yatapatikana katika faharasi yake. Na humo kuna utaratibu wa kushuka sura , katika anuani ya kila sura inasema kuwa ilishuka baada ya sura fulani. Faida zote hizo zinapatikana katika kitabu hicho cha kuvutia.
9-Aanze kwa kutoa zadi ya hitimisho kwa kuanzia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), pili kwa Amirul-Mu’minina Ali (a.s) aendelee hivyo hadi kwa maasumina wote 14 (a.s), kwani imepokewa riwaya tukufu kuhusiana na suala hiyo kwa kuwa watukufu hao kuliko viumbe watajibu zawadi (hiyo) kwa namna inayoendana na utukufu wao siku ya Kiama.
10-Kuinua sauti kwa Qur’ani wakati wa kusoma na awe ni mwenye huzuni na azingatie maana yake na isiwe huzuni ya mmoja wenu mwishoni mwa sura kama ilivyopokelewa katika hadithi.
11-Ni suna kusoma kwenye msahafu hata kama atakuwa amehifadhi yale anayoyasoma. Na ni suna kila mtu miongoni mwa watu wa familia awe na nakala yake maalumu ya msahafu mtukufu atakuwa akiweka ndani yake alama.
12-Kunyamanza kwa ajili ya Qur’ani, kwani kuzingatia yale anayoyasikia miongoni mwa aya ni fursa bora inayotolewa kwa ajili ya kuisikiliza. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atupe maisha kwa uhai wa Qur’ani na atupe shafaa yake (uombezi) na atujaalie kuwa miongoni mwa watu wanaoongoka kwa uongozi wake (Qur’ani) na kupata mwanga kwa nuru ya elimu yake. Hakika yeye ni Kiongozi wa neema naye ni mpole kwa waja wake na kwa upole wake ametuongoza kwenye dini yake iliyonyoka na atufunike kwa kitabu chake kitukufu na Mtume wake mtakatifu na watu wa nyumba ya Mtume wake watoharifu.
(Nina Mshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuongoza kwa haya, na hatukuwa ni wenye kuongoka lau kama si Mwenyezi Mungu kutuongoza.)
Muhammad Ya’qoobi
Muharram 1422 Hijiria.
[1]. Usuulul-Kaafi Juzu ya pili ukurasa wa 605.
[2]. Wasaailush-Shia, Kitabu Al-Twaharah, Abwaabut-Twaharah, babu 11 hadithi ya 2.