Maombolezo ya kifo cha Sheikh Muhammad jawad AL Mahdawiy

| |times read : 795
Maombolezo ya kifo cha Sheikh Muhammad jawad AL Mahdawiy
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Maombolezo ya kifo cha Sheikh Muhammad jawad AL Mahdawiy

Kwa masikitiko makubwa mno, chuo cha elimu na mafunzo ya dini mjini Najaf nchini Iraq, kimempoteza mwanazuoni kati ya wanazuoni wakubwa, mjuzi aliyekuwa mashuhuri kwa juhudi na elimu kubwa, makini na mwenye kujitolea kwa ajili ya kuwanufaisha wanafunzi.

Umaarufu ambao alikuwa nao tangu kipindi cha miaka 30 iliyopita chini ya uangalifu wa mwalimu wao Almarhum Al- Sayyid Muhammad Kalantar.

    Mwanazuoni ambaye alikuwa maarufu sana kwa ufundishaji wake katika ngazi zote za elimu ya dini, kuanzia chini mpaka juu kabisa.

Watu walioishi naye walimtambua zaidi kwa unyenyekevu wake na heshima yake kwa wengine, hata kama alikuwa ni mtoto mdogo. Alikuwa ni mwenye kutatua sana shida za watu, hasa wanafunzi wa masomo ya dini. Alikuwa ni mpole na mwenye uhusiano mwema, mbali na hapo alikuwa ni mwenye kuheshimu mno wasomi wa kidini.

Kwa hakika kifo chake kimesababisha huzuni na maumivu makubwa mno kwa wenzake, wanafunzi wake, na wote wenye kuzitambua sifa zake.

Mwenyezi Mungu (swt) amgubike kwa huruma zake zisizo na mwisho, na akutane naye huku akiwa ni mwenye bashasha na furaha, na amfufue siku ya kiyama pamoja na vipenzi vyake, watu wa nyumba ya Mtume Muhammad sala na salamu ziwe juu yao.

 Muhammad Yaaqubiy

17 Rajab 1442

2/3/2021