Mwanzo | | Maswali ya Kisheria
Maswali ya Kisheria

Shiriki swali

Hukumu ya kutoa talaka kwa njia ya simu.

Swali:

    Je, inafaa kupitisha shahada ya talaka kwa njia ya simu kutokana na umbali kwa mfano?.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Ni sharti kwa mashahidi kumsikia kwa pamoja mtaliki akitamka matamshi ya talaka, sasa kama itawezekana hilo kwa njia za mawasiliano ya kisasa hakuna shida, cha muhimu tu ni kuwa na uhakika kwamba hakutakuwa na udanganyifu na mfano wake katika hilo.

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Swala na wasiokuwa Mashia

Swali:

      Imetokea tupo kwa moja ya ndugu zetu ambaye si Sunni, muda wa swala ukafikia na yeye hana udongo wa kuswalia, sasa je, inafaa kuswali katika busati?.

Jawabu:

             Kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma na mwenye kurehemu.

Ikiwa haitakuwa shida kutafuta ambavyo vinafaa kusujudia basi jitahidi utafute, kwani si lazima tu uwe ni udongo bali inaweza kuwa jani la mti, mkeka wa majani, au hata karatasi na mfano wake.

                   Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy

 

Shiriki swali

Uvaaji hijabu kwa mke wangu

Swali:

    Natarajia kufunga ndoa karibuni, je, ninaweza mruhusu mke wangu avue hijabu yake tukiwa ndani, huku nikiwa najua fika ndani naishi na familia yangu ambao ndani yake kuna kaka zangu. Na hii ni kutokana na uvaaji hijabu kwa muda mrefu unamchosha mke wangu.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Ieleweke kwamba kuruhusu au kutoruhusu si katika mikono yako, kwa sababu hukumu za kisheria ni wajibu zifanyiwe kazi. Hivyo mkeo ni lazima avae hijabu hata kama itakuwa ni mbele ya kaka wa mme wake na inabidi asubiri tu katika hilo huku wewe ukijitahidi kuandaa mazingira maalumu kwa ajili yake.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu kwenda ufukweni au katika bustani za pamoja.

Swali:

Sisi ni wenye kukufuata wewe, hivyo tunaomba hukumu ya kwenda matembezi mbugani, bustanini au ufukweni kwa ajili ya kujifurahisha.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Hakuna tatizo kama itakuwa kuna sababu za kiakili na pia kutokuwa na mambo ya haramu sehemu hizo.

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu ya ndoa baina ya Shia na Suni

Swali:

    Ni ipi hukumu ya kisheria katika kijana wa kisuni kumuoa binti wa kishia?, je hili linafaa?, na kama jibu litakuwa ndio, ni masharti gani yanatakiwa katika hilo?, kwa maana nimesikia kuwa ndoa hii ni haramu.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Ndoa hii ni sahihi, kwani Uislamu ndio sharti la kusihi kwa ndoa, na Uislamu hupatikana kwa kutamka shahada mbili.

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

Hukumu ya uvutaji sigara mchana wa mwezi wa Ramadhani

Swali:

    Kuna baadhi ya wanafunzi huvuta sigara mchana wa Ramadhani kwa madai ya kwamba kuna Fatwa kutoka kwa Shahid Thani yenye kuelezea kutofuturisha kwa sigara, ni ipi hukumu yake?.

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Hukumu yetu ni kwamba tunazuia uvutaji wa sigara, na ama kuhusu kubakia katika kumfuata Ayatollah Shahid Thani ni kwa sharti la kunirejea mimi katika mambo yenye kutofautiana.

                                                        Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

 

Hukumu ya kujitolea viungo

Swali:

   Je, inafaa mtu aliye hai kujitolea kiungo chake kwa mwingine?.

 

Jawabu:

               Kwa jina la Mwenyezi Mungu.

Haifai kujitolea kiungo kwa mwingine kwani sio mali yako, ndio, kama itakuwa katika kufanya hivyo ni kwa ajili yakuokoa maisha ya mtu pasi na kumdhuru mtoaji kwa kiasi kikubwa basi hakuna tatizo.

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy.

Shiriki swali

Hukumu ya kubakia katika kuwafuata Marajii waliopita, pamoja na kufanyia kazi Ihtiyat za wajibu

Swali:

    Kwako Ayatollah Sheikh Mohammad Yaaqubiy, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako.

Tunaomba fatwa yako katika hili na Mwenyezi Mungu atwalipa, Je, mnaruhusu mtu kubakia katika kumfuata Ustadh Sayyid Al Khui (ra) na maulama wengine waliopita?.

Na je inawezekana mtu kumrejea mwingine asiyekuwa wewe katika mambo ya ihtiyat za wajibu?.

                                    Kikundi cha wenye kumfuata Sayyid Al Khui (ra). 

 

Jawabu:

       Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Sisi tunaruhusu kwa waliokuwa wakimfuata Sayyid Khui na Shahid Sadr (wote wawili) kubakia katika kutendea kazi risala zao, lakini katika maswala ambayo yanatokea zama hizi pamoja na yale ambayo yanajulikana kabisa tofauti zake basi ni lazima warejee kwangu. Na idhini hii itabakia mpaka pale tutakapotoa tamko lingine kwa uwezo wa Mungu.

Pia sisi tunamlazimisha mtu kufanyia kazi Ihtiyat za wajibu zilizotajwa katika vitabu. lakini itakapokuwa kuna tatizo na ikawa mtu anataka ufafanuzi zaidi basi aturejee, maana huenda lile ambalo tunaruhusu arejee kwa wengine ikawa ni katika mambo ambayo yanatakiwa kufuata mwenye elimu zaidi, kwani si kila mambo ya ihtiyat za wajibu inawezekana kurejea kwa mwingine.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

Shiriki swali

 

Misingi ya kisheria katika swala la kujiremba

Swali:

   Baada ya salamu:

Je, ni ipi misingi na kigezo katika swala zima la kujiremba na kujipamba, na ni upi msimamo wa kisheria katika hilo?.

 

Jawabu:

               Kwa jina la Mwenyezi Mungu.

Swala la kujiremba leo hii lina aina nyingi, na kwa mujibu wa hizo aina hukumu za kisheria zinakuja juu yake.

    Kuna ambazo zinakuwa ni kwa ajili ya kutoa baadhi ya vitu hasa usoni, vitu ambavyo wasioelewa wakiviona hupeleka kukejeli na kudharau kwa ujinga wao, sasa katika hali kama hii ni vizuri kutoa aibu zile ili kuepuka dharau na kejeli za wajinga.

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy.

Shiriki swali

Hukumu ya kutoa mimba

Swali:

   Kuna baadhi ya wakati kunatokea mambo ambayo Daktari anashauri mimba iweze kutolewa, je, ni sahihi kutoa mimba katika hali kama hii?.

 

Jawabu:

               Kwa jina la Mwenyezi Mungu.

Kama jambo litakuwa ni la kawaida basi hauna ruhusa ya kutoa mimba ambacho ni kitendo cha kuuwa nafsi, na dia lazima itolewa kama kitafanyika kitendo hicho. Ndio, kama itakuwa ni jambo kubwa kama vile kuonekana kiumbe kilichopo hakiwezi kuitwa mwanadamu, kama vile ionekane kwamba kichwa chake i kidogo mno kuliko kawaida, basi hakuna tatizo katika hilo.

Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy.

1 2 3 4 5
total: 41 | displaying: 21 - 30

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf