Uharamu wa kutakatisha mali
Swali:
Assalamu Alaykum:
Mimi ini mwanafunzi wa ngazi ya Masters katika chuo kikuu cha Almustafa mjini Qom Iran, na nipo katika kuandika Risala yenye maudhui ya “..Utakatishaji mali, mtazamo wa fiqhi na kanuni”, nimetafuta sana katika fatwa lakini sijapata rai yeyote ya maulama wetu wa Kishia kuhusu hili, ikumbukwe ni muhimu sana kuwa na rai za maulama wetu kunako jambo hili pamoja na kutaja chimbuko la hukumu ya hili linalojulikana sasa kwa kutakatisha mali.
Jawabu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu
Utakatishaji mali ni katika mambo yenye kuharibu uchumi wa miji na kuharibu tabia na mienendo ya watu na hata kupoteza imani zao. Pia ni sababu ya kuwepo kwa mazingira ya ufisadi na jinai. Na hapo awali jambo hili lilikuwa likifanywa na makundi ya kiuhalifu, lakini kwa sasa imekuwa ni jambo la wote hasa wakubwa wa kisiasa na viongozi mbalimbali.
Na ulimwengu wa sasa umefanikiwa kutambua hatari ya jambo hili na kuamua kuweka makongamano mbalimbali yenye kulenga kuweka mikakati ya kuweza kufichua na kupambana nalo, ikiwa ni pamoja na kuweka kanuni za kupambana na wenye kufanya jambo hili.
Lakini tunaona bado hata haya makongamano hayajaweza kusimamia jambo hili kwa kiwango kikubwa, kutokana na kutokuwa na umakini mkubwa katika utendaji, au urafiki baina ya wenye kusimamia, bali inawezekana hata hao pia ndio wakawa wenye kushiriki jambo hilo, na ndio maana bado tunaona jambo hili linazidi kushamili katika jamii na nchi kwa ujumla.
Sasa tukija katika hukumu ya kisheria ni kwamba kuna mambo matatu yenye kuamuaaina ya hukumu:
1. Chenye kutakatishwa, kwa maana ya zile mali ambazo hutakatishwa, kuna wakati zinakuwa ni mali za haramu ambazo zimepatikana kwa njia ya wizi au biashara za madawa, rushwa nk. Na mara nyingi hapa hufanyika jambo la kuzitakatisha kwa kutafuta uhalali wake kwa kuziweka katika benki, sasa kama asili ya mali itakuwa ni haramu basi tendo hili lote linakuwa ni haramu.
2. Mtakatishaji, kwa maana ya mtu au upande unaotumika kutakatisha hizo mali. Kuna wakati zinakuwa zinakuwa ni njia ambazo haifai kufanya kazi kama vile vikundi vya kihalifu, kigaidi, viongozi wenye kukandamiza raia wao, madikteta nk. Hivyo inakuwa ni haramu kwa njia ya kuwapa hawa watu waweze kusimamia jambo la kutakatisha fedha, kutokana na uharamu wa kudhamini au kuwatia nguvu hawa watu, na hapa ni bila ya kuangalia kipengele cha kwanza cha kitendo.
3. Utakatishaji wenyewe, kwa maana ya zile sehemu zenyewe ambazo zinasimamia kitendo cha kutakatisha na kuzipeleka katika mabenki au mashirika ya kimali, hivyo inawezekana ikawa i haramu kwa upande wa kwamba huyu mwenye kusimamia jambo hili akawa hana kibali cha sheria au ikawa huyo msimamizi ndio fisadi.
Hivyo kwa mujibu wa haya tunaweza sema kuwa uharamu unaweza kupatikana kwa moja ya sababu hizo tatu, na pia kwa kuongezea ni kwamba kuna sababu nyinginezo ambazo zinaweza kuwa chanzo cha uharamu, nazo ni:
· Wenye akii wote wamekubali kwamba jambo hili linapelekea kuhujumu uchumi, hivyo hili ni jambo ambalo tunasema ni lenye kuhujumu na kuharibu maisha ya watu na si mtu mmoja kama vile kunywa pombe na mfano wake.
· Kama mashirika ya kiserikali yatahusika katika kutakatisha basi haifai kuzitumia isipokuwa kwa idhini ya Faqihi mwenye masharti ya kufuatwa, kama ambavyo jambo ya kutakatisha si lenye kufaa kisheria.
Naam, inawezekana kukawa na vipengele vyenye kutoka katika hukumu hii, kama ambaye atakuwa anahitajia kutoa mali kwa ajili ya kufanya upasuaji wa dharura katika nchi nyingine, na nchi yake ikawa hairuhusu kutuma kiwango kama hicho cha pesa, kiasi kwamba anatakiwa kuhamisha katika akaunti mbalimbali za watu, na jambo hili kwa asili kabisa haliingii katika anuani ya kutakatisha mali, na hata dharura pia inaipa anuani nyingine ya kwamba mali hizi ni halali.
Quran inasema “...Na mwenye kupata dharura bila yakuwa ni mwenye kutenda uovu wala uadui, basi Mwenyezi Mungu ni msamehevu na mwenye huruma...”. Na hata katika hukumu mashuhuri ni kwamba kunapokuwa na dharura yenye kukatazwa huwa halali.
Hizi ndio hali ambazo zinajulikana katika jambo la kutakatisha mali, na natumia fursa hii kwa kuuhadharisha umma kunako hali nyingine ambazo si katika utakatishaji mali kwa maana ya kiuchumi, japokuwa bado zitakuwa na maana ile ile, kama vile kuhamisha pesa kwa zaidi ya njia moja ili kuweza kufikia lengo baya.
Na katika hayo ni mfano wa hila ambazo hutumika na baadhi ya watu kwa ajili ya kuweza kupata misimamo ya Marajii ili kuweza kutimiza malengo yao. Ambapo wanatumia baadhi ya watu kwa nembo ya kupeleka mali kwa marjii kwa jina la haki za kisheria, ambapo huaminiwa na kuweza kupatiwa lile ambalo analisema kwa marjii yule.
Au ikawa mtu ana lengo la kutenganisha jamii, ikawa yeye kama yeye hawezi kufanya hivyo, hivyo anaamua kumtumia mtu ambaye hana uelewa kwa kumpatia mali za kusimamisha vikao ambavyo ndani yake kutakuwa na maudhui za kutenga watu na jamii, ambapo kwa kufanya hivi yule mwenye lengo anafanikiwa.
Na mfano wa kihistoria wa jambo hili ni pale ambapo Ubeidu Llah Bin Ziyad alitaka kujua sehemu ambayo Muslim bin Aqil alifikia mjini Kufa, ambapo alimpatia mshauri wake mali nyingi sana kwa lengo la kwenda kukaa na masahaba wa Muslim kiasi atawalaghai na kuweza uvujisha siri ya alipo Muslim, na ilijulikana fika kuwa harakati ya Muslim ilihitajia mali, na yeye akatumia vizuri fursa hii kwa kujifanya ni katika wapenzi wa Ahlu Bait mpaka pale Muslim bin Ausaja akampeleka alipo na yakatokea yaliyotokea.
Pia hapa ni vyema kuashiria utakatishaji wa aina nyingine, mfano ambao unafanywa na baadhi yao kwa kutakatisha baadhi ya magaidi ambao wameshiriki katika kuangamiza watu wa Iraq, Syria na kisha wakawa na lengo la kurejea kwao (Saudia) kwa lengo la kupata msamaha wa mfalme wao, hivyo huwarudisha kwa njia ya Indonesia na kisha kuingia Saudia baada ya kuwapa anuani ya kwamba walikuwa ni walinganiaji ambao walitoka kutimiza majukumu yao nje ya nchi. Na kwa mujibu wa ripoti ambazo nimezipata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Indonesia ni kwamba mamia mpaa sasa wamepita kwa njia hii.
Na haya yote nimeyataja ili jamii ziweze kutambua baadhi ya vitimbi vinavyolenga kuzigawa na kupenyeza chuki baina yao, ili uwanja uweze kuwa safi na mafisadi waweze kutimiza malengo yao.
Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy
13 Safar 1436
6/12/2014