Muamala wa mke kwa mume mwenye kudhihirisha maasi.
Muamala wa mke kwa mume mwenye kudhihirisha maasi.
Swali:
Mimi kama mwanamke wa Kiislamu nikiwa na familia yenye watoto, vipi nitaweza kuamiliana na mume ambaye huwezi kumsifu kuwa ni Mwislamu kwa maana yake?, kwani haswali wala hafungi na ni mwenye kudhihirisha maasi waziwazi.
Jawabu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu
Ikiwa huyo mume hatakuwa ni mwenye kuacha kuwatimizia majukumu yake ya lazima kama vile chakula na malazi, na hakuwa ni mwenye kuwalazimisha kuacha mambo ya lazima kama vile swala na funga ya Ramadhani, au kufanya vitendo vya haramu kama vile kuvua hijabu mbele ya watu basi vumilia kwanza. Mpe nasaha kwa maneno yahekima na mazuri, na usimwambie maneno ambayo yatampelekea kuwa sugu na kupinga zaidi.
Kama ambavyo ni muhimu mno pia kukaa na watoto wako na kuzungumza nao juu ya malezi sahihi na wakawa na imani na wewe zaidi. Inshallah Mwenyezi Mungu atakusaidia katika jukumu hili.
Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy