Tafsiri ya aya ya 6 katika Surat jathiya.
Tafsiri ya aya ya 6 katika Surat jathiya.
Swali:
Katika Suratu Aljathiya aya ya 6 tunasoma “.......Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake?...”. Sasa nina rafiki yangu ambaye anadai kuwa aya hii ni dalili tosha katika kuonyesha kutokuwa na haja ya Hadithi, sasa ni vipi naweza mueleza maana ya aya hii?.
Jawabu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu
Umuhimu wa hadithi umethibitishwa na Quran yenyewe, “.....Yale anayokupeni Mtume yachukueni, na anayokukatazeni basi yaacheni.....”. Pia anasema “.....Na nakuapia kuwa hawatokuamini mpaka pale utakapowahukumu kunako wenye kutofautiana.....”. pia anasema “.....Na wala hakuwa ni mwenye kutamka kwa matamanio, isipokuwa ni ujumbe alioshushiwa tu....”. Pia anasema “....Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!...”.
Pia kama kusingekuwa na haja au umuhimu wa hadithi basi kwanini Mwenyezi Mungu kamtuma Mtume wake, na kisha kuendelea kumpa Wahyi hasa kwa kuzingatia angeweza kuishia katika Quran....?”. Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy