Hukumu ya kumwangalia mwanamke unayetaka kumuoa
09/07/2020 21:21:00 |
18/Dhul-Qadah/1441|times read : 410
Hukumu ya kumwangalia mwanamke unayetaka kumuoa
Swali:
Je, inafaa mwanaume kumwangalia mwanamke ambaye anataka kumuoa bila ya hijabu na kabla ya ndoa?, na ni viungo gani vingine ambavyo mwanaume anaweza kuviangalia kwa huyo mwanamke kabla yandoa?.
Jawabu:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu
Inatosha kwake kumwangalia uso na viganja vyake tu, na kama atakuwa anataka kumwangalia zaidi basi atumie wanawake wa upande wake kumwangalia vizuri au kwa kuhofia kwamba inawezekana akawa na aibu.
Ayaotollah Mohammad Yaaqubiy