Hukumu ya wazazi wenye kuzuia watoto kufunga
Hukumu ya wazazi wenye kuzuia watoto kufunga
Swali:
Ni ipi hukumu ya wazazi ambao wanazuia kufunga watoto wao ambao wameshafikia umri kwa kulazimikiwa na sheria, kwa hoja ya kwamba bado ni wadogo na hawataweza kufunga. Na watoto wana majukumu gani katika hili?.
Jawabu:
Kitendo hichi cha wazazi kwanza si sahihi na ni kinyume na uchamungu, kama ambavyo pia ni kuwazembesha watoto mambo ya dini. Bali inatakiwa wazazi wawe kinyume chake, wawatie moyo na kuwapa mafunzo watoto wao kabla hata ya kubalehe, ili iwe rahisi kwao watakapofikia balehe.
Ama watoto wao ni lazima wafunge, kwani hakuna kumtii kiumbe katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na ikitokea wamelazimishwa kula basi itabidi walipe baadae. Ila kama itakuwa kinachopelekea kulazimishwa kula ni jambo la kweli na lenye madhara basi hakuna ulazima wa kufunga kiasi kwamba wakaingia katika matatizo.
Ayatollah Sheikh Muhammad Yaaqobiy