Hukumu ya kuchunguza maiti (baada ya kifo)

| |times read : 353
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Hukumu ya kuchunguza maiti (baada ya kifo)

Swali:

 Ni upi tazamo wenu kunako jambo hili?

     Kuchunguza maiti kutokana na amri za mahakama au vitengo vyenye kuhusika na uhakiki wa vifo, jambo ambalo husimamiwa na madaktari waliobobea katika kuchunguza mwili wa mwanadamu ili kujua sababu asili ya kifo?.

Jawabu:

Kwanza haifai kukata kiungo cha maiti kutokana na uharamu wa jambo hili, kama ambavyo ni haramu akiwa hai pia. Naam, kama kufanya hivyo itakuwa kuna maslahi kama vile kuthibitisha kutohusika mtuhumiwa, kupatikana kwa haki ya mtu mwingine, au kuweza kuamua baina ya pande mbili, au kuondoa madhara yenye kusimamia jambo hilo basi kutakuwa hakuna shida.

Lakini kuweza tu kujua sababu ya kifo haitoshi kuwa sababu ya kufanya hayo, na tumejitahidi sana kuwaelewesha wataalamu kunako umuhimu wa kushikamana na hukumu za kisheria na kubakia katika zile sehemu ambazo wameruhusiwa tu. Na kama hawatafanya hivyo basi watakuwa wametenda makosa makubwa mno (Mungu atuepushe mbali), kama ambavyo mwenye kutenda jambo hilo atatakiwa kutoa dia kwa wenye maiti, na kiwango cha dia hiyo kimetajwa katika risala.

                                                        Ayatollah Mohammad Yaaqubiy

                                                                28 Muharram 1436

                                                                         21/11/2014