Mwanzo | | Maneno ya maadili | Kukuza Utu na Uzuiaji wa Makamu
Kukuza Utu na Uzuiaji wa Makamu

Shiriki swali

Mwanadamu Muumini...

“...Hakika mwanadamu muumini i lazima ajiandae na mabalaa (mitihani) katika dunia hii...”

Shiriki swali

Hebu tujiulize...

“...Hebu kwa pamoja tujiulize swali hili, Ni kipi mwanadamu atapoteza endapo atamtii Mwenyezi Mungu katika sheria zake?. Kwa hakika hatopoteza kitu, bali kinyume chake kabisa ni kwamba ataishi maisha ambayo anayaishi mwenye kumuasi Mungu (Raha), tena hata zaidi ya hapo, kwa maana huyu atakuwa na raha za dunia na ahera kwa pamoja ambazo zinasababishwa na hii imani yake kwa Mwenyezi Mungu swt. Mwenyezi Mungu anasema “..Na hakika nyinyi mnataraji kutoka kwa Mwenyezi Mungu mambo ambayo wao (makafiri) hawataraji..”.

Shiriki swali

Hakika gao la Mwenyezi Mungu halina mipaka...

“...Kwa hakika Mwenyezi Mungu hana mipaka wala ubahili katika utoaji wake. Na mja hana jukumu zaidi ya kuandaa moyo wake kuwa nafasi stahiki ya gao hilo, kwa kuusafisha kutokana na machafu, kama ambavyo ardhi unayotaka kupanda miti ni lazima kwanza uisafishe kutokana na maada zenye kudhuru na kisha kuiandaa kupokea mbegu, hivyo ndivyo pia inatakiwa iwe kuhusu nyoyo...”

Shiriki swali

Mwenyezi Mungu hawezi kuacha....

“...NI mbali sana Mwenyezi Mungu kuacha hali ya ujinga uliopo bila ya kutuma mjumbe mwenye kusuluhisha. Mjumbe ambaye atakuwa si mtenda makosa, naye ni Imamu Muhammad bin Hassan Al Mahdi atfs....”

Shiriki swali

Kutilia mkazo kadhia ya Imamu Mahdi atfs

“...Kutilia mkazo kadhia ya Imamu Mahdi, kuitetea, kutenda katika kujiandaa kuipokea na kuinusuru ikiwa ni pamoja na kuandaa mikakati yetu kuielekea, kama vile kuendeleza minasaba ya kidini kama sala ya Ijumaa na Jamaa, Kuadhimisha maombolezo ya Imamu Hussein as, Hafla na vikao vya dua na ukumbusho, kuhudhuria misikitini kwa wingi, kufungua vikao vya masomo ya itikadi, adabu historia Mtume ni katika majukumu yetu makubwa...”

Shiriki swali

Kama mnapenda kumnusuru Imamu...

“...Kama kweli mnapenda kumnusuru Imamu basi kuweni tayari kukabiliana na magumu, kwa maana hayo ndiyo yatakayowajenga na kuwapa moyo wa kupata jambo hilo adhimu. Na endapo mtu matatizo haya ambayo si lolote yatakuwa mazito kwake, basi hatoweza pata nafasi hiyo. Imamu Ally as anasema “...Ikiwa tu mnakimbia baridi na joto, bila shaka kwenye upanga mtakimbia zaidi...”.

Shiriki swali

Siku ambayo nilikuwa naandika moja ya fatwa...

“Siku moja nilikuwa nikiandika moja ya fatwa, na katika majibu yangu nikakuta nimeandika “Hakika Uislamu unahitajia sana watu wake”. Ni neno wazi sana, ila nikahisi kabisa kwamba sikuweza kuandika hilo isipokuwa ni kwa rehema na baraka za Imamu atfs...”

Shiriki swali

Sote tunaomba...

“...Hakika sisi sote tunaomba kupata sharafu ya kumnusuru Imamu na kuwa naye katika kupambana na adui, lakini ni nani hasa mwenye kujibiwa haraka maombi yake?. Ni muumini ambaye amepitia magumu na kukabiliana nayo kwa subira na uvumilivu...”

Shiriki swali

Mwislamu anatakiwa awe…

“Mwislamu anatakiwa awe katika nafasi ambayo Imamu anaitaka, awe katika nafasi ya juu kabisa kwenye kutekeleza sheria, awe na adabu njema, awe juu katika nyanja ya itikadi sahihi..”

Shiriki swali

Kumuomba Mungu kupitia yeye

“...NI katika majukumu yetu kumuomba Mungu kupitia Imamu atfs, kama ambavyo Bi Fatima Zahra ametuhimiza hilo. Kwa maana Imamu huwa anasikia na anaitikia miito yetu..”

1 2 3
total: 24 | displaying: 1 - 10

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf