Mwanzo | | Maneno ya maadili | Dini iliyo na Mwenyezi Mungu ni Uislamu
Dini iliyo na Mwenyezi Mungu ni Uislamu

Shiriki swali

Kuenea kwa Uislamu..

“...Kwa masikitiko ni kwamba kuenea huku kwa Uislamu ni kutokana na juhudi za Waislamu, bali ni kutokana na utukufu na uimara wa misingi yake na hukumu zake. Hivyo wenyewe unajieneza, pamoja na kwamba unahitajia sana Waislamu, lakini ikitokea Waislamu wakalala basi wenyewe unajiendesha...”.

Shiriki swali

Uislamu ni mfumo kamili..

“..Uislamu ni mfumo kamili katika nyanja zote anazohitajia mwanadamu katika maisha yake, kwa maana hiyo mwanadamu ana haja ya kutafuta kutoka kwingine. Na endapo atatambua hili basi ataweza kupambana na kila aina ya kizuizi chenye kuulenga Uislamu na nyanja zake...”.

Shiriki swali

Sheria za Kiislamu...

“...Sheria za Kiislamu ni sheria sahihi, kwani zimeweka misingi sahihi katika mahusiano yeyote yale ya kijamii, kwa kiasi kwamba kama mwanadamu atashikamana nayo basi atafikia lengo lake pamoja na kupata ridhaa za Mungu. Na kama ataamua kuachana na misingi hiyo basi Mwenyezi Mungu naye atamuacha na nafsi yake yenye kuamrisha mabaya, na kisha kuangukia katika majanga ambayo hatayamfaa majuto baada yake...”.

Shiriki swali

Miongoni kwa adabu...

Miongoni mwa adabu za Kiislamu ni kwamba mtu asijigambe na kujikweza kwa ambayo Mwenyezi Mungu amempa, na wala asiyatumie katika kuminya wengine na kueneza chuki kwao...”.

Shiriki swali

Hakika dini inatilia mkazo...

“...Hakika dini inatilia sana mkazo misingi ya kibinadamu, na inataka kuiweka katika nyoyo za watu, kwa maana misingi hiyo ndio njia pekee ya kuokoa maisha ya watu kutokana na matatizo na hofu ambazo zinawatawala. Leo hii nchi za Magharibi zinakiri kwamba wameshindwa kupambana na gonjwa na Ukimwi kwa njia zao, na kwamba njia pekee ni kujaribu kuwalea watu kiroho na kuchunga misingi ya kiroho katika mahusiano ya binadamu. Ni rai sahihi kabisa, na walitakiwa kushikamana nayo tangu mwanzo..”.

Shiriki swali

Hakika Uislamu...

“...Hakika Uislamu hauishii tu katika kumwekea Mwanadamu njia za ibada katika maeneo fulani, bali una wigo mpana zaidi hata katika tamaduni, historia na mambo yao yote. Hivyo Mwislamu anatakiwa aishe humo na wala asitoke, kama ambavyo aulinde na kushikamana nao kama ambavyo watu leo hii wanashikamana na ulimwengu huu, na ajitolee kwa ajili yake...”.

Shiriki swali

Wenye kunifanyia uadui...

“...Kwa hakika wenye kunifanyia uadui na kunikosea kamwe sitawafanyia ubaya, kwa maana vyovyote vile bado ni wana familia wa Kiislamu, na Uislamu una shida na wanafamilia wake wote. Hivyo vyovyote wafanyavyo kifua changu bado  cheupe kwao, na hata wakitumia muda wao kunichafua na kunisema bado nitabakia ni mwenye kuwakumbatia daima...”.

Shiriki swali

Nchi ambazo...

“....NI haramu kuamiliana na kuwa pamoja na nchi ambazo zinapiga vita Uislamu na kuwafanyia vitimbi Waislamu, ikiwa itaonekana kama kuwa nao ni kuwasaidia katika malengo yao..”.

Shiriki swali

Kueneza mema...

“...Ni jukumu letu sisi kueneza mazuri na kuzuia mabaya na ufisadi katika jamii, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi uhakika wa Uislamu wa asili..”.

Shiriki swali

Mikono chafuzi..

“...Kwa hakika mikono chafuzi imeweza kufikia Uislamu katika nyanja zake mbalimbali, kutokana tu na chuki dhidi yake. Kwa maana katika historia Uislamu ulikuwa i pigo kubwa sana kwa watu hawa, japokuwa bado kuna umuhimu wa uhakika huu kudhihirishwa sasa, kwa maana kuficha hakuwezi kushindana na haki. Sema tu baadhi ya uongo na uzushi wa leo umefichwa sana katika umaarufu na kuenea kwake, hali ya kuwa si kila kilicho mashuhuri basi kina mashiko..”.

1 2 3
total: 21 | displaying: 1 - 10

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf