Mwanzo | | Maneno ya maadili | Dini iliyo na Mwenyezi Mungu ni Uislamu
Dini iliyo na Mwenyezi Mungu ni Uislamu

Shiriki swali

Kuchafua sura ya dini…

“...Kwa hakika kuchafua sura ya dini na kuonyesha kwamba dini ndiyo ambayo imekuja kumdhulumu mwanamke kwa mambo kama vile kuruhusu kuolewa zaidi ya mmoja, au ushahidi wa mwanamme mmoja i sawa na ushahidi wa wanawake wawili, au haki yake katika urithi na mengineyo kwa kigezo kwamba mwanamke ni mjinga kwa mtazamo wa dini, ni katika mambo ambayo yanapelekea mno mwanamke kukataa na kuwa mbali na dini, na hata hupelekea mwanamke huyu kuweka mbali kanuni za kidini kwa kuwa huaminika kwa makisio tu..”.

Shiriki swali

Uislamu unaamini...

“...Uislamu unaamini kwamba uzuri wa kweli wa mwanamke ni katika kujihifadhi kwake, aibu yake, hijabu yake na kujisitiri kwake kwa wanaume, uchamungu na kushikamana kwake na dini yake. Mwenyezi Mungu swt anasema kwamba vazi la kweli kabisa ni uchamungu...”.

Shiriki swali

Siasa katia Uislamu

“..Siasa katika Uislamu ina asili ya usafi katika malengo yake, kwa maana inajengeka katika ridhaa za Mwenyezi Mungu..”.

Shiriki swali

Kutambua utukufu wa Uislamu

“...NI lazima watu kutambua utukufu wa Uislamu, katika adabu na itikadi zake. Na kwamba ni njia pekee ya kuwanufaisha watu kwa kuwa tu ni njia ya Mwenyezi Mungu, hivyo yote yenye kuandikwa katika hili inatakiwa yawe kwa lugha nyepesi ambayo watu wote wataielewa, wawe Waislamu au hata wasiokuwa wao, kwa maana kupenyeza haya katika nyoyo zao kutawafanya wazidi kupenda Uislamu..”

Shiriki swali

Kwa hakika misikiti

:..Kwa hakika misikiti ni alama ya utukufu na nguvu ya Uislamu..”

Shiriki swali

Mrengo wa Sadr..

“Kwa hakika mrengo na msimamo wa Sadr ni moja ya mifano hai ya Uislamu hai na wenye harakati..”

Shiriki swali

Ni katika adabu za Uislamu

Ni katika adabu za Kiislamu kuheshimu nadharia za wengine, na kama kutakuwa na migongano basi atatuliwe kwa mazungumzo yenye kujenga, na kama itatoea mmoja hajatosheka na rai ya mwingine basi ana haki ya kutoungana naye lakini pasi na kuvuka mipaka ya kisheria katika kuamiliana naye...”

Shiriki swali

Subira, uvumilifu na kusaidiana

“...Ni lazima tujipambe na subira, uvumilivu na kusaidiana. Na wala tusiamiliane kwa kutumia zaidi huruma na hofu....”

Shiriki swali

Kadhia za msingi....

“...Umoja ndio jambo la msingi, hata kama kutakuwa na tofauti za misingi, hilo ni jambo la kawaida sana maadamu kuna akili zenye kufikiri na kuyafanyia kazi yenye kuifikia. Cha muhimu tu ni kuangalia hizi tofauti zetu kwa mtazamo chanya, kwa maana ya kwamba ni kuwa na aina nyingi za ala katika utendaji zenye kutumikia lengo moja ambalo i sheria iweze kufika kwa kila kona ya ulimwengu...”

Shiriki swali

Miongoni mwa tabia za Kiislamu

“..Miongoni mwa tabia na adabu za Kiislamu ni kuheshimu fikra na nadharia za wengine na matendo yao, na kama kutatokea hali ya mfarakano basi umalizwe kwa mazungumzo mazuri. Na kama itashindikana kwa hilo na mtu hakukinaika na mazungumzo ya mwingine, sawa asiungane naye, lakini asivuke mipaka yake kisheria katika kuamiliana naye. .”.

1 2 3
total: 21 | displaying: 11 - 20

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf