Mwanzo | | Maneno ya maadili | Kukuza Utu na Uzuiaji wa Makamu
Kukuza Utu na Uzuiaji wa Makamu

Shiriki swali

Kumpenda  Imamu ni njia ya…..

“...Kumpenda Imamu atfs ni katika majukumu yetu, kwa maana hiyo ni njia ya kupata baraka za Mungu, kwani katika riwaya tunaambiwa kwamba “Mwenye kuwapenda nyinyi basi huwa amempenda Mungu...”.

Shiriki swali

Jaribu kuweka nia

“...Siku zote jaribu kunuia kutomuudhi mwenzako, na kuwa sababu ya furaha yake...”

Shiriki swali

Kuwahurumia watu

“...Naimani kwamba kuwahurumia na kuwafanyia upole watu, ni katika mambo ambayo yanapelekea kujikurubisha kiroho kwa Imamu atfs...”

Shiriki swali

Kuiandaa nafsi na kuilea

“...Hakika kuiandaa na kuilea nafsi ni katika majukumu yetu ili tu kuweza kufikia katika ila nafasi ya kuwa katika wenye kumnusuru Imamu kama ambavyo kuwa katika wenye kubeba ujumbe wake na kujenga heshima ya Uislamu kwa ujumla...”

Shiriki swali

Kwa hakika Umma kuhisi uwepo wa.....

“...Kwa hakika kitendo cha umma kuhisi kuwepo kwa imamu wake, kitapelekea kujihisi yale ambayo anayahisi katika huzuni na maumivu yake, na hata yeye pia atakuwa ni mwenye kushirikiana nao katika vikao vyao, kama ambavyo atakuwa nao katika kuhakikisha anawatolea vikwazo vya dhulma na uwapa imani katika kuzichunga nafsi zao. Na mwisho kabisa ni kuwafanya kuwa ni katika jeshi lake, hasa pale ambapo Umma utatambua kuwa kuzidisha kwao kutenda mema ni katika mambo ambayo yanapelekea Imamu kudhihiri haraka....”

Shiriki swali

Kwa hakika kupinga uwepo wake...

“...Kwa hakika kupinga na kukataa uwepo wa Imamu Mahdi atfs maana yake ni kusababishia umma kukosa kiongozi na umma wenyewe pia...”

Shiriki swali

Kwa hakika jambo la Imamu Mahdi....

“...Kwa hakika kadhia ya Imamu Mahdi atfs  ni kadhia ya Kiulimwengu, na inatakiwa walimwengu wote wakinaishwe kunako yeye, kwa maana huyu ni wao. Na ndio maana kunatakiwa kuwe na lugha nyingi zenye kumuelezea yeye kwa mujibu wa yule ambaye unamuhutubia, kwa maana kumkinaisha Shia juu yake ni tofauti na mazungumzo utakayotumia kumkinaisha asiyekuwa Shia, kama ambavyo ni tofauti kabisa na utakavyotaka kumkinaisha asiyekuwa Mwislamu kabisa.....”

Shiriki swali

Jukumu la kwanza kabisa kwa Umma...

“...Na jukumu la kwanza kabisa kwa Umma juu ya Imamu wake ni kumtambua yeye, kwa maana moja ya matokeo mabaya kabisa ya kutomjua ni kupotea, kufarakiana, kugombana, kukithiri kwa wenye kujifanya yeye katika nafasi hii tukufu, kwa maana nafasi hii ni katika nafasi bora na za juu kabisa....”

Shiriki swali

Huu ndio umuhimu wa Imamu wa zama (atfs)

“..Umuhimu wa Imamu wa zama atfs unapatikana katika kusimamia mambo ambayo kwayo umma utatengemaa, ikiwa ni pamoja na kuupeleka umma katika ukamilifu na uongofu na kuyafikia yale ambayo inatakiwa kuyafikia. Na hii ndio maana ambayo Bi Fatima Zahra katika maneno yake ndani ya msikiti wa baba yake Mtume Muhammad saww alisema “..Na akajaalia Imamu wetu kuwa ni nidhamu ya umma...”.”

Shiriki swali

Kuomba kwa kupitia Imamu wa zama (atfs)

Tunatakiwa kuomba sana kwa kupitia Imamu wa zama (atfs) ili tuweze kubarikiwa kumtawalisha yeye, na kutoacha wajibu na faradhi ya aina yeyote ile.

1 2 3
total: 24 | displaying: 11 - 20

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf