Binafsi nimejifunza
Binafsi nimejifunza kila ambapo mambo yanakuwa magumu kwangu, niseme tu “...Ewe Aba Salehe, hebu nidiriki mimi..” naye hunisaidia katika kukidhi haja zangu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Binafsi nimejifunza
Binafsi nimejifunza kila ambapo mambo yanakuwa magumu kwangu, niseme tu “...Ewe Aba Salehe, hebu nidiriki mimi..” naye hunisaidia katika kukidhi haja zangu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.
Je, katika ziara zako umefikiria hili?
Je, unapokuwa unazuru ziara zako, umefikiria kuswali rakaa mbili kwa ajili ya Imamu (atfs), au kutoa sadaka maalumu kwa ajili yake?.
Kwa maana sisi ndio ambao tunamficha imamu katika mawazo yetu, pamoja na kutambua kwamba tunaishi kwa dua zake na hifadhi yake.
Kila siku tunatamani.....
Kila siku tunatamani tuwe ni katika wafuasi na wanusuru wake, hali ya kuwa bado ni madhaifu wa nafsi zetu na familia zetu, hatuna hata uwezo wa kuchukua maamuzi ya mwisho. Je, kwa udhaifu huu tutaweza kumnusuru Imamu as?, au kwa kuwa chini ya Magharibi daima tutaweza kufanikisha hilo?.
Sasa acha niseme leo kwa sauti kubwa kabisa, mnusuruni Imamu wenu na Mwenyezi Mungu atawanusuru, msiwe ni sababu ya Imamu kuchelewa kudhihiri na Mwenyezi Mungu anawanusuru, kwani kila siku Imamu wenu anaita na kunadi “..Je, kuna mwenye kuninusuru aninusuru?!...”. basi mnusuruni Imamu wenu, na andaeni silaha zenu kwa ajili yake, msiwe madhaifu na wanyonge kwa hali yeyote ile, na harakisheni sana katika kuzikomboa nafsi zenu kabala haijafika siku ambayo majuto hayatafaa kitu....ewe Mwenyezi Mungu, kwa hakika nimefikisha, kwa hakika nimefikisha....”.
Shikamaneni na Uislamu wenu...
“..Shikamaneni na Uislamu wenu, kwani ndio siri ya mafanikio yenu, dhamana ya maisha yenu yaliyobakia. Na daima hifadhini hisia hii ya kimapinduzi juu ya Uislamu, kwa maana ndio alama ya ushindi wenu. Na wala msiwape madui zenu nafasi ya kuwaondolea hima hii thabiti, na kila mnapopata nafasi katika mikutano yenu ya kidini na kijamii, basi itambulisheni hima hii kwa njia yeyote ile...”.
Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-