Mwanzo | | Maneno ya maadili | Siku ya Kusoma
Siku ya Kusoma

Shiriki swali

Wito kwa Wanazuoni na Wanafikra:

Kwa hakika ninawaita wanazuoni, wanafikra, watu wa utamaduni na waandishi warudi kuyahuisha tafiti na masomo ya kijamii na kuyangalia kwa kina na kunufaika nayo, ili tuinuwe kiwango cha jamii yetu na kuifanya iwe tayari kupokea dola ya Imamu aliyeahidiwa (a.s) na uongozi wake wenyebaraka utakaoanzia kwenye ardhii tukufu. Tafiti hizo zinapaswa ziwe wazi na zenye nia dhabiti ili ziwe ndio msingi wakuanzia, na hapo ndipo mambo mengi yaonekanayo kuwa ni sahihi utayaona yako kinyume kabisa: “Na huenda mkakichukia kitu nacho ni kheri kwenu, na huenda mkakichukia kitu nacho ni shari kwenu” surat Al-Baqarah: 216.

 

Shiriki swali

Sababu za Kuendelea Umma:

Hakika uhai wa Umma na utukufu na maendeleo yake ni kusoma na kujifunza, wakati ambao jamii ya kijahilia na uliyobaki nyumba matendo yake hayatofautiani na maisha ya wanyama. Anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: “Enyi mlioamini! Mwitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaita kwenye lile litakalowapa uhai” Surat Al-Anfaal: 24.

Shiriki swali

Umma wa Kusoma:

Ni haki yetu Sisi Umma wa Kiislamu kujifakharisha kwakuwa Sisi ni Umma Kusoma na kutafuta elimu, na kwamba neno la kwanza kuteremka kwa Mtume (s.a.w.w) pindi alipopewa ujumbe wa kiislamu lilikuwa ni (Soma), yaani amri ya kusoma, hali kadhalika kwamba muujiza wa kudumu  wa Uislamu, yaani Qur’ani ni kitabu chenyekusomwa, ambacho kimetokana na neno ‘qiraatu, yaani: kusoma.

Shiriki swali

Kurejesha Heshima ya Umma wa Kusoma na Kalamu:

Ni wajibu wetu tuirejeshe heshima yetu na tuwe kweli ni Umma wa Kusoma na Kitabu. Tuliongoze gurudumu la mwamko wa kitamaduni kwa wote na tuhimize kusoma vitabu kwa namna mbalimbali na kuvipa umuhimu. Tusambaze vitabu, tuwashawishi watu kusoma na kubuni njia tofauti zitakazoinua kiwango cha utamaduni kwa watu kupitia kueneza maonyesho ya vitabu, kuvifanya vipatikane kwa bei nafuu, kuvichapisha katika maumbile yenye kuwavutia wasomaji, kurahisisha uandishi wake na kutofautisha maudhui zake. Tuvifanye kuwa ni vitabu  vyenye kuzungumzia mahitaji jamii, matatizo na matarajio yake, visaidie katika kuijenga shakhsia ya mwanadamu, na viwekwe katika ukubwa mbalimbali, kuanzia vile vyenye juzuu nyingi hadi vile vyenye juzuu moja, vijitabu, majarida na makala fupi. Ni juu yetu tuendelee kusoma ili tuwe Umma hai, wenye tamaduni na ulioendelea. Ni wajibu wa kila mtu asome ali awe mwandamu wa kweli, kama ambavyo ni lazima tusome ili kumridhisha Mwenyezi Mungu aliyetukuka na mtume wake (s.a.w.w.) na mawalii watukufu, na tunatakiwa kuitika wito wa Mwenyezi Mungu atuitapo kwenye jambo la litupalo uhai. Tusome ili tuishi maisha ya upendo, furaha na utukafu.

total: 4 | displaying: 1 - 4

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf