Mwanzo | | Maneno ya maadili | Maombi ya utetezi wa manabii
Maombi ya utetezi wa manabii

Shiriki swali

Utukufu wa Uislamu ni...

“...Utukufu wa Uislamu ni katika umoja wa watu wake, ambao Mwenyezi Mungu anawapeda...”.

Shiriki swali

Kuzidisha kusujudu kwa kumshukuru Mungu..

“...NI muhimu sana kuzidisha kusujudu kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa neema zake ambazo hazihesabiki, au kwa ajili ya kumuomba kutukubalia dua zetu. Kwa maana hakuna muda ambao mja anakuwa karibu na Mungu kama ambavyo anakuwa katika hali ya kusujudu huku akisema mara sana “Ya Arhama Rahimiin”.

Shiriki swali

Kusoma dua za kujikurubisha...

“...Ni lazima tuzidishe sana kusoma dua za kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu na kuomba kutoka kwake kwa kuzingatia maana zake. Pia ni lazima tukutane katika nyusiku ya Ijumaa kwa ajili ya dua Kumayl, au siku ya Ijumaa kwa ajili ya dua Nudbah..”.

Shiriki swali

Kuwa karibu na Mwenyezi Mungu...

“...Inatakiwa tuwe karibu na Mwenyezi Mungu katika hali zote, daima tuwe ni kama mgonjwa ambaye hana njia nyingine zaidi..”

Shiriki swali

Alama muhimu na nembo ya kurejea...

“..Moja kati ya nembo na alama muhimu za kuonyesha kurejea kwa Mungu, ni kuimarisha misikiti kwa sala za jamaa, dua na kumtaja Mungu na kutafuta njia za kumwelekea yeye swt...”.

Shiriki swali

Bado nakariri...

“...Nilikuwa na badi naendelea sana kukariri dua hii “...Ewe Mwenyezi Mungu usituondolee mema yetu, na wala usituingize katika mabaya ambayo umeshatutoa huko..”.

Shiriki swali

Wa kabla yetu wanatuambia...

“..Wa kabla yetu wanatuambia kwamba pindi ambapo mambo yalikuwa yanawawia magumu basi walikuwa wakikutana msikitini kwa ajili ya dua na kutaja mambo ambayo yaliwatokea watu wa nyumba ya Mtume saww pamoja na kuwazuru..”.

Shiriki swali

Imepokelewa kutoka kwa Imamu Hadi as

Katika kubainisha maana ya kauli yake isemayo “...Oindi mambo yanapokuwia magumu basi sema “..Ewe ambaye hufungua vifundo vya magumu....”, imepokelewa kutoka kwa Imamu Hadi as akisema “..Hivi ndivyo ambavyo Mungu na watu wa nyumba ya Mtume saww wametufunza,...”. Sasa sisi tupo wapi na mafunzo haya ambayo yanakusudia kutunufaisha na kutusaidia?!.

Shiriki swali

Inatakiwa ....

“...Mwanadamu anatakiwa katika nyakati zake zote awe ni mwenye kumkumbuka Mungu, kumuomba amuwezeshe imani na kufanya mambo mema...”.

Shiriki swali

Nimejifunza....

Nimejifunza kwamba kila mambo yanapokuwa magumu basi niite “...Ewe Imamu Mahdi nidiriki..”. naye hunisaidia kuyapita kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu...”.

total: 10 | displaying: 1 - 10

Ofisi ya al-Marjii Wadini

Khekhe Muhammad Yaqoobi (Allah amhifadhi) - Tuma swali lako-

Najaf Ashraf