UKUMBUSHO WA FUNGA YA SIKU YA KWANZA YA MWEZI WA MUHARAM KWA AJILI KUKUBALIWA DUA NA MAOMBI

| |times read : 177
UKUMBUSHO WA FUNGA YA SIKU YA KWANZA YA MWEZI WA MUHARAM KWA AJILI KUKUBALIWA DUA NA MAOMBI
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

Kwa jina la Mwenyezi  Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu

 

UKUMBUSHO WA FUNGA YA SIKU YA KWANZA YA MWEZI WA MUHARAM KWA AJILI KUKUBALIWA DUA NA MAOMBI

 

       Shekhe Swadooq amesimulia katika kitabu cha Al-Majaalis na Uyunul Al-Khbaar kwa mapokezi kutoka kwa Al-Rayyaan bin Shabib kwamba alisema: (Niliingia kwa Imam Ridhaa (amani iwe juu yake) mwanzo mwa mwezi wa Muharam akasema: Ewe Bin Shabib! Je Wewe umefunga? Nikasema: hapana. Hapo ndipo akasema: Hakika siku hii ndio siku ambayo ndani nabii Zakaria (amani iwe juu yake) alimuomba Mola wake mlezi akisema:

{ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِنْ لَدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ}

{Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unayesikia mamombi.} [Surat Aali Imran: 38], basi Mwenyezi Mungu akamkubalia maombi yake na akawaamuru malaika wakamwita Zakaria:

{وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَى}

{Hali akiwa amesimama chumbani akisali, kwamba Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya...} [Surat Aali Imran: 38].

       Hivyo basi, mwenyekunga siku hii kisha akamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, atamkbalia maombi yake kama alivyomkubalia nabii Zakaria.) [Wasail Al-Shia: 10/469].

     Hivyo, ni matarajio yangu kwamba waumini wanawake na wanaume watafunga siku Ijumaa ya mwanzo wa mwezi Muharam na watatenda mambo yanayowakaribisha kwa Mwenyezi Mungu ili awakidhie haja zao kwa vyovyote vile zitakavyokuwa, na kwamba katika maombi yao watatanguliza kuomba faraja na kudhihiri haraka kwa kiongozi wetu wa zama hizi Imam Al-Mahdi (amani iwe juu yake), watamuombea ulinzi , nusura na usaidizi, na kumuomba Mwenyezi Mungu atujalie kuwa miongoni mwa wanusuru wake watakao mpigania kwa hali na mali. Atujalie tufaulu kwa uombezi bwana Mtume (s.a.w.w) na kizazi chake kilichohifadhika na kutenda makosa.

 

Ili kupiga kura ya kukubali mwaliko huu chagua neno (ndio) kwa kubofya linki (kiunganishi) hii hapa chini:

https://t.me/yaqoobioffice/4722

*Huisheni_Jambo letu

*Hussein ni Mwamkuko na Uelewa

*Ndondoo za Marjaiyah Tukufu

T.me/yaqoobioffice