FAIDA YA VISA KUJIKARIRI NDANI YA QUR’ANI
FAIDA YA VISA KUJIKARIRI NDANI YA QUR’ANI
- Ni kurudia na kuendeleza dozi ya matibabu na kutokutosheka na dozi moja pindi unaposimamia usahihishaji wa hali mbaya au kuziba mapungufu au kutatua tatizo liliopo katika fikra ya jamii au katika Imani yake au mwenendo wake. Kwa mfano utakuta baadhi ya visa vya mitume vijikariri zaidi ya mara kumi, lakini kila kikielezwa huwa na onjo yake, na athari yake na nafasi yake katika kulifanikisha lengo, na huacha athari tofauti na ile iliyoachwa na kilipotajwa sehemu nyingine na njia nyingine hata kama vyote madhumuni yake ni mamoja.
Tunapozungumzia suala la mwanamke kujishauwa mbele ya mwanamme, na kutojistiri na kujifanya shetani anayezuwia kumkumbuka Mwenyezi Mungu aliyetukuka; ili kimatendo awe mfano uliowazi wa kauli ya Ibilisi:
[لأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ، ثُمَّ لآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَآئِلِهِمْ وَلاَ تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ]
“Basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo Nyooka. Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala hutawakuta wengi wao wenye shukrani”[1], na hawa wanawake wahuni hutumia njia mbali za kuwapotosha wanaume na kuwadumbukiza katika maasi, kuanzia kujishauwa wawapo barabarani, kuja kujipamba wawapo vyuoni na kuonyesha viungo vya miili yao, na michezo na kwenye maonyesho ya kisanaa wakiwa watupu.
Hivyo tukitaka kuyakabili maradhi haya yenye kuangamiza katika jamii, tunaweza kuyatibu kwa kutumia vitabu vituatavyo: kitabu kuhusu hali za kijamii zilipotoka[2], kitabu kuhusu masuala ya mwanamke[3], kitabu kinachohusu athari za michezo na Sanaa katika kubomoa maadili ya jamii, kitabu kuhusu matatizo ya wanafunzi wa vyuo vikuu, wasiwasi zao na matamanio yao[4], na kitabu kingine chenye maudhui hayo hayo kuhusu vijana[5] na kitabu kinachohusu fikihi ya familia kinachozungumzia mahusiano ya kifamilia na kijamii kwa mujibu wa mafunzo ya sheria na vitabu vingineyo[6], kwani tatizo hili ni hatari na linaingia kwenye Nyanja zote zilizotajwa, na kulisoma katika Nyanja zake zote kunatoa tija tofauti na ile ambayo ingepatikana kwa kulidurusu katika uuga mmoja, na si haba kuwa vitabu hivi vinaongeza idadi ya hadhira inaowazungumzisha, na hatimaye tija inakamilika kwa kulisoma tatizo katika pande zake zote[7].
8. Kutumia njia tofauti katika kuwaongoza wanadamu. Kwa kuwa mwanadamu na aina tatu za ulimwengu ambazo ni: nafsi, akili na moyo, utaiona Qur’ani imeviandaa vyote ili kumuwezesha mwanadamu kumtii Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Haya nimeyafafanua katika masomo kwa anuwani (Hebu turudi kwenye Qur’ani[8]).
Utaikuta mara nyingi ikizungumzisha maumbile na kuyaamsha, kwani Qur’ani katika baadhi ya hadithi imeelezea sababu ya kuteremka kwake kwamba: (Ili iyaamshe maumbile yao yaliyojificha), kwa sababu maumbile ni dalili iliyozawi na yenye kusema kweli zaidi, kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kuyajadili. Msikilize Mwenyezi Mungu anavyoongea na maumbile katika kuthibitisha uwepo wa Muumba:
[أَفَرَأَيْتُم مَّا تُمْنُونَ، أَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُ أَمْ نَحْنُ الْخَالِقُونَ]،[أَفَرَأَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ، أَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُ أَمْ نَحْنُ الزَّارِعُونَ]،[أَفَرَأَيْتُمُ الْمَاء الَّذِي تَشْرَبُونَ، أَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ الْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ الْمُنزِلُونَ]،[أَفَرَأَيْتُمُ النَّارَ الَّتِي تُورُونَ، أَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَا أَمْ نَحْنُ الْمُنشِؤُونَ]
(Je, Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? Je, mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? Je, mnaona makulima mnayo yapanda? Je, Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? Je, mnayaona maji mnayo yanywa? Je, ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? Je, mnauona moto mnao uwasha? Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?[9]) na semehu nyingine Mwenyezi Mungu anasema hali yakuwa akimkemea mwanadamu muasi:
[هَلْ جَزَاء الإِحْسَانِ إِلا الإِحْسَانُ]
(Hakuna malipo ya ihsani isipokuwa ihsani[10]), bila shaka nawe unaogelea katika neema za Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
[وَإِن تَعُدُّواْ نِعْمَتَ اللّهِ لاَ تُحْصُوهَا]
(Na mkizihesabu neema za Mwenyezi Mungu hamuwezi kuzidhibiti)[11].
[1]. Surat Al-A’araaf: 16-17.
[2]. Kitabu a’n Ad-Dawahiril Al-Ijtimaai’yah Al-Munfarifah.
[3]. Kitabu a’n Qadhaayal- Al-Mar’ah.
[4]. Kitabu a’n Mashakil Al-Jaamia’t, Humuumuhum wa Tat’wallua’tuhum.
[5]. Kitabu a,n Ash-Shabaab.
[6]. Fiqihul Usrah.
[7]. Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, kumetolewa vijitabu na majarida ambavyo vinazungumzia hizi nyanja zote.
[8]. Falnarji’i Ilal Qur’ani.
[9]. Surat Al-Waaqia’h: 58-72.
[10]. Surat Ar-Rahman: 60.
[11]. Surat Ibrahim: 18.