UTAWALA GHASIBU WA KIZAYUNI NI ATHARI YA UGONJWA, BASI NYINYI TIBUNI ASILI UGONJWA
UTAWALA GHASIBU WA KIZAYUNI NI ATHARI YA UGONJWA, BASI NYINYI TIBUNI ASILI UGONJWA
Waislamu wanapolipa umuhimu suala la utawala ghasibu wa Kizayuni na wakafanya juhudi za kuuondoa, ni lazima watambue kuwa utawala huu si chochote ila ni moja athari za ugongwa ambao unaonekena kwenye mwili wa Umma wa Kiislamu ikiwa ni tija ya uwepo wa ugonjwa lililojificha ndani yake, ugonjwa ambao ndio asili na sababu ya maumivu haya. Ama ugonjwa wenyewe ni Waislamu kujitenga na mfumo na njia ya Mwenyezi Mungu maishani mwao. Hivyo, hawapaswi huyapa umuhimu maumivu na wakasahau sababu ya mauvu hayo, kwani wakifanya hivyo mfano wao utakuwa ni kama kile kinachofanyika katika uwanja wa mieleka ya ng’ombe –kama mwanafikra mmoja alivyoshabihisha[1]- kwamba ng’ombe alikasirika yeye huwa hima yake, mbio zake, hasira zake na nguvu zake anavielekeza kwenye kitambaa chekundu anamsahau mpinzani wake halisi ambaye ndio kabeba kitambaa hicho, na hivyo kumpa fursa adui yake kuzanisha visu shingoni mwake na husababisha kufa hali ya kuwa amemsahau hadi anakufa na kutoweka. Hali yetu isije ikwa kama ya yule ng’ombe! Na hapo utaona kuwa umma huwa unakaukaribia kumshinda adui yake kila unavyokaribia kuishinda nafsi yake, na kwa kadri unavyorudi na kurejea kwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka.
[1]. Naye ni sheikh Jawdah Sai’d.