MIONGONI MWA UFAHAMU WA KUPAMBANA NA MAKAFIRI NA MASHETANI
MIONGONI MWA UFAHAMU WA KUPAMBANA NA MAKAFIRI NA MASHETANI
Ufahamu huu umekusanya nyanja zote za maisha. Basi ni fikra zipi zilizotolewa na Qur’ani, ambazo tunaweza kuzitambua kuwa ni uelewa wa kupambana na makafiri? Mwenywzi Mungu anasema:
[وَلاَ تَهِنُواْ فِي ابْتِغَاء الْقَوْمِ إِن تَكُونُواْ تَأْلَمُونَ فَإِنَّهُمْ يَأْلَمُونَ كَمَا تَأْلَمونَ وَتَرْجُونَ مِنَ اللّهِ مَا لاَ يَرْجُونَ وَكَانَ اللّهُ عَلِيمًا حَكِيماً]
“Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima”[1]. Kwanini kukimbia kupambana nao wakati madhara huzipata mbande mbili? Na tofauti n kwamba nyinyi mnataji (malipo) yale yaliyopo kwa Mwenyezi Mungu siku ya Akhera wala kumna hasara, wakati wao hawaraji kwake chochote isipokuwa adhabu iumizayo. Na Mwenyezi Mungu anasema:
[وَظَنُّوا أَنَّهُم مَّانِعَتُهُمْ حُصُونُهُم مِّنَ اللَّهِ فَأَتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ حَيْثُ لَمْ يَحْتَسِبُوا وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ الرُّعْبَ يُخْرِبُونَ بُيُوتَهُم بِأَيْدِيهِمْ وَأَيْدِي الْمُؤْمِنِينَ فَاعْتَبِرُوا يَا أُولِي الأَبْصَارِ]
“Nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyezi Mungu. Lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo patazamia, na akatia woga katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya waumini. Basi zingatieni enyi wenye macho”[2]. Sehemu anasema:
[مَا كَانَ لأَهْلِ الْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ الأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُواْ عَن رَّسُولِ اللّهِ وَلاَ يَرْغَبُواْ بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ لاَ يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلاَ نَصَبٌ وَلاَ مَخْمَصَةٌ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَلاَ يَطَؤُونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ الْكُفَّارَ وَلاَ يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلاً إِلاَّ كُتِبَ لَهُم بِهِ عَمَلٌ صَالِحٌ إِنَّ اللّهَ لاَ يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ، وَلاَ يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلاَ كَبِيرَةً وَلاَ يَقْطَعُونَ وَادِياً إِلاَّ كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ اللّهُ أَحْسَنَ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ]
“Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapo waghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanao fanya mema. Wala hawatoi cha kutoa kidogo wala kikubwa, wala hawalivuki bonde, ila huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo kuwa wakiya- tenda”[3], ni kwanini kuchelea na kupuuzia kutoa kile ambacho ndani yake kuna utii wa Mwenyezi Mungu aliyetukuka, katika juhudi na mali? Na kwanini kumdhania Mwenyezi Mungu vibaya, dhana ambayo huwapata watu pindi watu wanapohitajika kutoa haki za kisheria zilizoko katika dhima yao, kama vile: khumsi, zaka nk? Aya nyingine ni:
[ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُواْ كَذَلِكَ حَقّاً عَلَيْنَا نُنجِ الْمُؤْمِنِينَ]
“Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na walio amini. Ndio kama hivyo, inatustahiki kuwaokoa Waumini”[4].
Na miongo mwa fikra za kupambana na makafiri, ni aya tukufu za surat Muhammad. Ikiwa utaweza kuhama kwa roho yako, na fikra zako na moyo wako kwenye kile kipindi cha furaha ya maisha mwanadamu, na ukajenga picha kwamba na wewe ni katika lile kundi la waumini lilimzunguka mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), kundi liliambatana naye katika wakati mgumu, mwanzo wa Uislamu, kipindi ambacho walikuwa wanyonge, wakiadhibiwa na Makuraishi adhabu kali, mpaka kufikia Washirikina walipogubikwa na hali ya kushindwa na wakakata tamaa baada ya vita ya Ahzab, kiasi kwamba mtu (s.a.w.w) alikuwa na uwezo wa kaunza mashambulizi, kisha ushindi wa Waislamu ukafululiza kuanzia ushindi wa Hudaibiya hadi kwenye ufunguzi wa Makka na ushindi wa Khaibar na Taif, kisha Yemeni na bara nzima la Arabu, jalia kwamba na wewe ulikuwepo huko unateremkiwa na maneo matakatifu ya Qur’ani tukufu iliyotoka kwa Mola wako mlezi mwendeshaji wa mambo yako na muumba mbingu na ardhi, akiongea nawe moja kwa moja ili akuambie:
[بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ] [الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ، وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَى مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ، ذَلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ كَذَلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ، فإذا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّى إذا أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنّاً بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاء حَتَّى تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ذَلِكَ وَلَوْ يَشَاء اللَّهُ لانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ، سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ، وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ، يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ، وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ، ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ، أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ دَمَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا، ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لا مَوْلَى لَهُمْ، إِنَّ اللَّهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ، وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ الَّتِي أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلا نَاصِرَ لَهُمْ، أَفَمَن كَانَ عَلَى بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ كَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءهُمْ]
Kwa Jina La Mwenyezi Mungu Mwingi Wa Rehema Mwenye Kurehemu. “Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao. Na walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyo teremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao. Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata upotovu, na walio amini wamefuata Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo wapigia watu mifano yao. Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao. Atawaongoza na awatengezee hali yao. Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha. Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao. Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao. Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo. Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walioamini[5]. Na makafiri hawana mlinzi. Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makaazi yao. Na miji mingapi iliyo kuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu ulio kutoa; nao tuliwateketeza na wala hawakuwa wa kuwanusuru. Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama aliye pambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao?[6]”
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu”[7].
Na Mwenyezi Mungu wakati huo huo anawatahadharisha na wanafiki ambao huwatosa waumini wakati wa mapambano na maadui na wakidharau udhaifu wa zana zao hali ya kuwa wameghafilika kuhusu siri ya nguvu ya waumini ambayo ni mahusiano yao na Mwenyezi Mungu aliyetukuka, na hapo ndio akaamua kuwasikilisha kauli yake:
[إِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَؤُلاء دِينُهُمْ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللّهِ فإن اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]
“ Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima”[8].
Na huingia ndani ya aya za ufamu wa mapambao na makafiri kila ahadi ya Mwenyezi Mungu ya ushindi, na kurithisha ardhi, na kwamba mwisho mwema ni waumini, na kwamba Mwenyezi Mungu yupo nao, na huwateremkiwa na malaika kwa utulivu kutoka kwa Mola wao mlezi, na kwamba atawaondolea hofu na huzuni, na mkataba alioufunga nao kwamba anazinunua nafsi na mali zao na kwamba malipo yao itakuwa ni pepo, vile vile zidisho la kumkopesha Mwenyezi Mungu na kutoa katika njia yake, na ahadi zingine nyingi ambazo hatuwezi kuzifafanua katika muhtasari huu.
Ama ukeli mkubwa unaothibitishwa na Qur’ani katika hili ni kwamba kushindwa na adui wa nje na dhahiri –makafiri- ni tawi la kushindwa na adui wa ndani ya nafsi yenyekuamrisha maovu, ambaye ni shetani. Ndio maana utaiona Qur’ani inapowaahidi waumini uongozi wa ardhi na kwamba ndio watakaoirithi na walioko juu yake, inafanya hatua ya kwanza kabisa kuwa ni kujenga na kusuluhisha mambo na kutekeleza mfumo wa Mwenyezi Mungu juu ya nafsi, anasema Mwenyezi Mungu:
[وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ، وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الأَرْضِ وَنُرِي فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ]
“Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi. Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa”[9]. Hivyo kwanza kawafanya viongozi, ambayo ina maana kuwa kuzitaka dhati zao na kuzitenga mbali na uchafu, na linalotia nguvu hilo ni kuwa hakuna thamani ya kuwashinda makafiri ikiwa ushindi huo hautambatana na kumshinda shetani na kufanya mambo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika, kwa sababu jambo lisilokuwa kwa ajili ya kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, wakati huo hakutakuwa na tofauti ya waumini na makafiri, bali wote watakuwa sawa, na wote watakuwa ni watu wa dunia na Akhera hawatakuwa na fungu lolote.
Kwa mfano: kushindwa waislamu katika vita ya Uhudi na hasara kubwa iliyowakuta, Mwenyezi Mungu anawambia:
[إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْاْ مِنكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُواْ]
“Hakika wale waliorudi nyuma miongoni mwenu siku yalipo pambana majeshi mawili, Shetani ndiye aliye watelezesha kwa sababu ya baadhi ya makosa waliyo yafanya...”[10], kwamba kushindwa na kukimbia kwao vilikuwa ni kwa sababu ya maovu waliyoyafanya, wakati mukabala wa hayo anasema:
[إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ]
“Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni”[11], na ushindi wa Mwenyezi Mungu hupatikana kwa kumtii yeye, tofauti na hivyo, Yeye si muhitaji wa walimwengu, na hali ipo hvyo hivyo katika iliyotangulia isemayo: “Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini katika nyinyi...”, na ndio maana bwana mtume (s.a.w.w) akazungumza na msafara wa wapingana jihadi waliokuwa wamerudi kutoka vitani kwa kusema: “Karibuni, mmemaliza jihadi (vita) ndogo na mmebakiwa na jihadi kubwa. Wakamuuliza: Ni ipi jihadi kubwa ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Ni jihadi ya nafsi. Mtume akajibu”[12].
[1]. Surat An-Nisaa: 104.
[2]. Surat Al-Hash’r: 2.
[3]. Surat At-Tawba: 120-121.
[4]. Surat Yunus: 103.
[5]. Aya hii ndio imebeba sura kamili ya mahujiao haya, kwamba waumini wao wana mlinzi anayesimamia ulinzi wao na malezi yao, furaha na kufaulu kwao, ambaye si mwengine isipokuwa Mwenyezi Mungu aliyetukuka, katati makafiri hawana mlinzi, bali mlinzi wao ni shetani dhaifu anayekumbia wakati wa mapigano na kuwatosa: “Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu”. Surat Al-Anfaal: 48.
[6]. Surat Muhammad: 1-14.
[7]. Surat An-Nur: 55.
[8]. Surat Al-Anfaal: 49.
[9]. Surat Al-Qasas: 5-6.
[10]. Surat Al-Imran: 155.
[11]. Surat Muhammad: 7.
[12]. Al-Kafii: 5/12, mlango wa: wojouhul-jihaad.