MASOMO TUJIFUNZAYO KUTOKANA NA NAMNA QUR’ANI INAVYOJENGA JAMII

| |times read : 536
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

MASOMO TUJIFUNZAYO KUTOKANA NA NAMNA QUR’ANI INAVYOJENGA JAMII

       Hapa inatubidi kuashiria baadhi ya masomo tunayoweza kujifunza kutokana na namna Qur’ani inavyojenga na kuongoza jamii:

1.       Umakinifu katika kutambua sababu na chanzo kuliko kujua athari wakati kutoa utatuzi wa hali maalumu, n jambo ambalo ni muhumu na ladharura. Mgonjwa aendapo kwa daktari na kumueleza hali anayo jisikia, bila shaka jambo la muhimu alifanyalo daktari huwa ni kuainisha na kugundua sababu kisha ndio hutoa matibabu yake. Ama kutosheka na matibabu ya athari za maradhi husika, kama vile: maumivu ya kichwa, au tumbo kuuma, au kupanda kiwango cha choto la mwili bila kubainisha sababu na chanzo hasa cha hizo athari, ni fikra mbovu kabisa. Ikiwa mtu atataka kutibu hali ya kutojistiri kwa akina mama, au hali ya vijana kuiga mila za kimagharibi, au watu kutotoa Khumsi au kutotekeleza ibada ya sala, au kufanya kwao machafu mfano wa kunywa pombe na kufanya ushoga, au kwa umla sema: watu kutotekeleza sheria za Mwenyezi Mungu na kufanya kwao makusudi kwenda kinyume na sheria hizo, haitoshi kuwaambia kuwa: jambo ni wajibu hivyo litekelezeni na hili ni haramu liacheni, kwa sababu wao ni Waislamu na yote haya wanayajua, hivyo ni lazima kwanza kutambua sababu ya udhaifu wa msukumo wao wa kidini, msukumo ambao ndio chachu ya kutekeleza na kutii sheria, kisha baada ya hapo ndio kutolewe tiba na suluhisho lake. Hapa utaona kwamba udhaifu wa msukumo wa kidini, chanzo chake ni udhaifu wa kimaadili na kiimani kwa jamii, ndio maana Qur’ani katika mji wa Makka -wakati ikianza kuteremka kwake- ilijikita kwenye mambo haya mawili. Qur’ani ilifafanua imani na ikaitetea kwa hoja na dalili mbalimbali, na ikatoa majibu ishikali na maswali yaliyokuwa yakielekezwa kwenye imani hiyo, na mara nyingi ilikuwa ikiyaamsha maumbile ya watu, kwa sababu maumbile salama ni hoja na dalili ya ndani kwa ndani iliyomo ndani mwa kila mwanadamu kiasi cha kutoweza kuikanusha na kuikataa. Lakini pia kwa upande wa pili, Qur’ani ililipa umuhimu suala la kuelezea matukio ya siku Kiyama, na kutaja desturi na kanuni za Mwenyezi Mungu kwa umati zilizopita, na kusimulia matukio mengi yenye mazingatio na somo, ili kuziamsha akili zao na kuzisafisha nyoyo zao, baada ya hayo ndio ikawalazimisha kutekeleza sheria nao wakakakubali kwa hiyari. Na tunatambua kuwa kipindi cha malezi ndani ya Makka kilikuwa ni kirefu kuliko kile cha sheria ndani ya Madina. Na kutokana na hayo tunafahamu ni namna gani inavyotakiwa kulipa umuhimu jambo la kuzingatia sababu kuliko athari.

2.       Kutokana na nukta ya kwanza tunahamu pia udharura wa kuijenga shakhsia ya Muislamu kimaadili na kiimani.  Na Qur’ani katika hili ilitumia njia kadhaa nilizo zitaja katika masomo yaliyojulikana kwa jina la: (Na turejee kwa Mwenyezi Mungu), kiasi kwamba nilisema huko: Qur’ani ilitumia njia ya ulimwengu tatu anazo ziishi mwanadamu (akili, moyo na roho). Kwa mfano: inahusiha baina ya mbingu kuzuia baraka zake, na ardhi kutotoa kheri zake na watu waovu kutawala na kutopokelewa dua, inataja kuwa sababu na chanzo cha vyote hivyo ni mwanadamu kujinga mbali na sheria ya Mwenyezi Mungu na kuacha kutekeleza faradhi ya kuamrisha mema na kukataza maovu, na kwamba mwenyekutaka kuepukana na matokeo haya mabaya, basi na atekeleze faradhi hii. Imekuja katika hadithi kwamba:  

(إذا تركتم الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر نزعت عنكم البركات ونزلت عليكم البليّات وسلطت عليكم شراركم ثم تدعون فلا يستجاب لكم)

         “Mtakapoacha kuamrisha mema na kukataza maovu, basi zitaondolewa kwenu baraka, na mtateremkiwa na mabalaa, na watakuwaleni waovu wenu, kisha mtaomba hamtajibiwa”[1].

       Njia muhimu zaidi katika hizo tuliiashiria hapo kabla, ambayo ni kuelezea hali nzito ya umauti na yale yaliko baada yake, na yale yatakayo kuwa siku Kiyama, na majibizano ya makafiri na waovu motoni pamoja na mashetani wao, halikadhalika kukumbusha ada ya Mwenyezi Mungu kwa wenyekuacha kumtii. Mwenyezi Mungu anasema:  

[دَمَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا]

“Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo”[2],

[فَأَخَذَهُمُ اللّهُ بِذُنُوبِهِمْ وَاللّهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa sababu ya madhabi yao, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu”[3], na kwa kutaja neema zake zisizo hisabika wala kudhibitiwa kwa waja wake, nao wakiwa nwenye kuukubali ukweli huu utokanao na maumbile yao kwaba:

[هَلْ جَزَاء الإِحْسَانِ إِلا الإِحْسَانُ]

“Hakuna malipo ya ihsani ila ni ihsani”[4], kisha ikabainishwa furaha ambayo hujenga na kuimarisha moyo wa mwanadamu, na maisha yake na jamii yake, iwapo atatekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu. Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُواْ وَاتَّقَواْ لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاء وَالأَرْضِ]

“Na lau watu wa miji wangeliamani na wakamchamugu, kwa yakini tungeliwafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi [5].

       Hakika Imani na maadili wema ndivyo ambavyo huweka malengo ambayo atayaishi wanadamu, kama ambvyo kuaisha mwelekeo wake. Kwa mfano: inapotakiwa kujitolea kwa ajili jambo la kheri au kumsaidia mtu mwenye uhitaji, ni nani ambaye atakae harakia kuliendea hilo: muumini au ambaye anatafura radhi ya Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kawa anahitaji badala kutoka kwake au yule aliye mbali na dini ambaye hima yake kubwa ni kujikusanyia vya duniani na miongoni mwa wale:

 [قَدْ يَئِسُوا مِنَ الآخِرَةِ كَمَا يَئِسَ الْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَابِ الْقُبُورِ]

“Walikwisha kata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini”[6]

Bila shaka wakwanza ndiye atakayeharakia jambo hilo. Hii ndio athari ya imani na maadili mema katika kumsukuma mwanadamu kwenye utekelezaji wa sheria, kwani lengo la muumini ni Mwenyezi Mungu aliyetukuka. Basi kuweni wana wa Akhera wa msiwe katika wana wa dunia, kwa sababu kuporomoka na kupotea kwa kila umma kulitokana na kupoteza kwake lengo ambalo ulipaswa uliishi, na hivyo, njia nyingie zikawatenga na njia ya Mwenyezi Mungu kama ilivyokuja katika Qur’ani:

 [وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيماً فَاتَّبِعُوهُ وَلاَ تَتَّبِعُواْ السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ]

“Na kwa hakika hii ndiyo njia yangu iliyonyooka. Basi ifuatani, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kumchamungu”[7].

       Hivyo hatuna namna zaidi ya kulijaza pengo hili katika akili na nyoyo za jamii ili mwelekeo wake inyooke na maisha yake yafuate nidhamu aliyoitaka Mwenyezi Mungu, lakini pia tunapaswa kuichukua njia ya Qur’ani katika kuzihuisha nyoyo na kuzilanisha, na katika kuzilea nafsi na kuzimezesha imani ya haki ambao ndio chimbuko la maadili mema. Mwenyezi Mungu anasema:

[أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ]

“Je, wakati haujafika kwa wale walioamini kwamba nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kwa mambo ya haki yaliyoteremka? Wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla yao na muda wao ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu, na wengi wao wakawa wapotovu”[8].

     Na huu ni mlengo unapaswa kuingiwa na kila mwanafikra na mwana malezi, kwani ndio njia ya Qur’ani katika kuwaidhi na kuhuisha nyoyo, na aya zote za Qur’ani kama mwenye akili angelizichunguza bila shaka  angelisahihisha mfumo wa maisha yake kama asemavyo Mwenyezi Mungu katika surat Ad-Dukhan:

[كَمْ تَرَكُوا مِن جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ، وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ، وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ، كَذَلِكَ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْماً آخَرِينَ، فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاء وَالأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنظَرِينَ]

“Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha! Na mimea na vyeo vitukufu! Na neema walizo kuwa wakijistareheshea! Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe. La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula”[9].

       Nami ninakunasihini kusoma kitabu cha Al-Qalbu As-Saliim ambacho kina juzuu mbili, juzuu ya kwanza inahusu imani na nyingine inahusu maadili ambazo zimetoka katika moyo wenye nia safi na uliotakasika.

3.       Kufuata mpangilio katika kutoa hidaya, na kusuluhisha na kuwaongoa watu kwa upole. Na mfano uliyo wazi wa hilo ni: uharamishwaji wa pombe –ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni ada na kawaida iliyo jikita katika jamii na zikanyweshwa nyoyo zao na akili zao- ambao ulifuata hatua zifuatazo:

[يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ و إثْمُهُمآ أَكْبَرُ مِنْ نَفْعِهِمَا]

“Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. Waambie: katika hayo mna uovu mkubwa na manufaa (kidogo) kwa watu, na uovu wake ni mkubwa zaidi kuliko manufaa yake”[10].

       Baadhi ya waislamu ilipoteremka aya hiyo waliesema: Hatutakunywa pombe; kwa sababu ni uovu na Mwenyezi Mungu ameharamisha mambo machafu yaonekanayo na yale yaliyofichikana na uovu, wakati wengine walisema: Tutakunywa kiasi chenye manufaa ndani yake, hapo ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha kauli yake isemayo: 

 [لاَ تَقْرَبُواْ الصَّلاَةَ وَأَنتُمْ سُكَارَى حَتَّىَ تَعْلَمُواْ مَا تَقُولُونَ]

“Msikaribie swala hali ya kuwa mmelewa mpaka mjue mnayo yasema”[11]. Baadhi yao wakajiziwia kunywa pombe, wakasema: Hatuwezi kutumia kitu kinachokwenda kinyume na swala, wakatu huu ndio ikateremka aya ya surat Al-Maidah ambayo ililipa mkazo zuwio hilo kwa kusema:

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالأَنصَابُ وَالأَزْلاَمُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ]

“Enyi mlio amini! Hakika pombe na kamari na kupiga ramli ni uchafu wa kazi ya shetani, basi jiepusheni nayo”[12].

       Na lengo ya kushuka Qur’ani kwa utaratibu kwa kipindi cha miaka (23) ilikuwa ni kutatua matatizo ya jamii hapo kwa hapo kwa kuzingatia zama, sehemu, na mazingira ya tukio. Halikadhali zilizingatiwa tofauti za kiwango cha watu na uwezo wao wa upokeaji na utekelezaji wa maamrisho na makatazo.

      Na inawezekana mpangilio wa kuremka aya ukawa katika namna mbalimbali. Kwa mfano, tunapotaka kutatua hali fulani ya kijamii iliyokita mizizi -kama vile ada za kikabila-, kwanza tunatakiwa tuanze kuweka alama za viulizo juu ya usahihi wake, malengo yake na kuitilia mashaka, kisha ndio tuanze kutoa njia mbadala na uchaguzi mwingine utakaokuwa mkabala wa ile hali. Tukiweza kuzitia mashakini nyoyo juu ile hali, na watu wakaanza kuelekea mbadala ulio bora, basi hali ya kuridhika kuibadili ile ya mwanzo itaanza, wakati huo ndio inawezekana kuishambulia ile hali ili kuiondoa, lakini kuanza kuikabili bila kufanya maandalizi maana yake ni kufeli na kushindwa vibaya, kwani maadamu bado hali hiyo imejikita na mamumbile ya watu yameumbwa ni wenye kupenda kuheshimu mila na desturi walizorithi na kuzinyenyekea, hivyo wenye mila zao wote watakuwa tayari kukabiliani na kila jaribio lenye lengo la kubadilisha ada na kawaida yao hiyo ya kijamii.

    Kwa mfano bwana mtume (s.a.w.w) alopopewa utume hakuyashambulia masanamu moja kwa moja, bali alianza kumuambudu Mwenyezi Mungu akiwa na Ali (a.s) na Bi Khadija (a.s) mbele ya Makuraishi bila kuyazungumzia masanamu yao kwa ubaya. Lakini bwana mtume (s.a.w.w) kwa kitendo hiki alifungua mlango wa maswali na viulizo vingi: kwamba watatu hawa wananya nini? Ni nani wanayemuabudu? Na ni kwanini wameamua kuachana na mila za watu wao? Lakini pia watu wana ujasiri kiasi gani na wana imani madhubuti kiasi gani katika nyoyo zao mpaka wakaweza kusimama dhidi ya watu wote kwa amani bila woga?.... Hivi viulizo vilipelekea kundi la watu kuingia kwenye Uislamu – rejea kisa cha Abdullah Bin Masoud katika vitabu vya historia- bila kushambuliwa na Makuraishi, kwa sababu bwana mtume (s.a.w.w) hakuamsha hisia zao tofauti na angeliyataja masanadu kwa ubaya mojo kwa moja.

4.       Kuyapa umuhimu na kuuelekeza umma wa Kiislamu kwenye yele mambo ya msingi ambayo ndio yanauhifadhi, hasahasa yale ambayo yanafahamika kuwa yaliachwa na kupuuzwa baada ya mtume (s.a.w.w) na ambayo alikuwa akiyahimiza sana, kama vile: kuamrisha mema na kukataza mabaya, uimamu na uongozi kwa ajili waumini, na kuwapinga makarifi na kuwapenda ndugu wa karibu, na kushikamana na Qur’ani na kizazi cha mtume (s.a.w.w), na kuchunga miskiti, na swala za jamaa na Ijuamaa, mambo ambayo baada ya kufariki kwake (s.a.w.w) Umma wa Kiislamu uliipuuzia misingi hii madhubuti yenye lengo la kuulinda Umma, na hapo ndio kasi ya kupotea ikaanza kwa haraka, hivyo kureje kwenye wema na kuerebishaji wa jamii kunategemea kuifanikisha misingi hii na kuirejesha kwenye maisha ya jamii.

5.       Kumpunguza matatizo na taabu anazokabiliana nazo yule mtu ambaye hufanya hujudi ya kurekebisha jamii na kuongoa au kama tulivyomwita huko nyuma: mbeba Qur’ani ikiwa ni ujmbe wa islahi na kurekebishaji wa jamii. Mwenyezi Mungu anasema:

[المص، كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلاَ يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ وَذِكْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ]

“Alif Lam Mym 'Saad. Kitabu kilicho teremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake, upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini”[13],

 و[فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَى إِلَيْكَ وَضَآئِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن يَقُولُواْ لَوْلاَ أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاء مَعَهُ مَلَكٌ]

“Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyo funuliwa kwako, na kifua kitaona dhiki kwa hayo, kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa khazina, au wakaja naye Malaika? Wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kila kitu”[14],

[وَاصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلاَّ بِاللّهِ وَلاَ تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلاَ تَكُ فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ، إِنَّ اللّهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَواْ وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ]

Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya MwenyeziMungu tu. Wala usiwahuzunikie; wala usiwe katika dhiki kwa hila wanazozifanya. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na watendao mema”[15],

[لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُواْ أَذىً كَثِيراً وَإِن تَصْبِرُواْ وَتَتَّقُواْ فإن ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الأُمُورِ]

“Hapana shaka yoyote mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu, na bila ya shaka yoyote mtasikia udhia mwingi kutokana na walio pewa Kitabu kabla yenu na wale walio shiriki. Na ikiwa mtasubiri na mkamchamngu basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia”[16]. Na ibara yenye upole zaidi ni kaule yake Mwenyezi Mungu:

[وَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا]

Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu”[17], macho ya uangalizi, macho ya upole, rehema, ulinzi, muongozo, muono nk.

       Na utaona sura kamili imeteremka kwa ajili ya lengo hili hili, kama vile: surat Yusuf ambao unahisi kabisa kwamba iliteremka katika kipindi kigumu alichokiishi mtume (s.a.w.w) ndani ya Makka na kabla kuhamia Madina, ambapo alimkosa msaidizi kwa kufariki dunia Abu Talib na Bi Khadija (a.s), akawa amekata tamaa ya Makuraishi kuingia katika Uislamu, lakini pia akawa amejaribu kutafuta kimbilio lingine tofauti Makka kama vile Taif, hakufanikiwa, dunia ikawa ni dhiki kwa waumini, katika kipindi hicho ndipo iliteremka surat Yusuf ikiwasimulia namna ndugu zake na Yusuf walivyopanga njama dhidi ya ndugu yao mdogo, wakamtupa kisimani, jambo ambalo kwa mazingira ya kawaida maana yake ni kifo, lakini Mwenyezi Mugu akamtumia msafara uliomuokoa, kisha akauzwa kwenye nyumba ya mfalme wa Misri, akaingia kwenye mtihani wa mke wa muheshimiwa na wanawake wengine, akafungwa miaka kadhaa, lakini Mwenyezi Mungu aliyetukuka akamuokoa na kifungo, na akamfundisha tafsiri ya ndoto, na kwa baraka za Mwenyezi Mungu akapata kile cheo cha kuaminiwa kusimamia hazina ya Misri, kisha akawa mfalme wa Misri baada ya kuzimiliki nyonyo za watu kwa maadili yake mema na usimamizi wake mzuri. Hapa ndipo walipokuja wale ndugu wapanga njama mbele yake wakiwa ni dhalili, lakini yeye kwa moyo wake wenye huruma akawasamehe huku akisema:  

[لاَ تَثْرَيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ يَغْفِرُ اللّهُ لَكُمْ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ]

“Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanao rehemu”[18], na hatima yake Mwenyezi Mungu akamkutanisha kwa mara nyingine na baba yake na kaka yake. Na bwana mtume (s.a.w.w) pia alilitumia neno lile lile lililotumiwa na Yusuf pindi Makuraishi walipofanyia kitendo kile kile cha kumfanyia njama na kutaka kumuuwa, kisha Mwenyezi Mungu akamnusuru dhidi yao na akamuwezesha juu yao ndani mji wao wa Makka, hapo ndipo bwana mtume (s.a.w.w) aliwakariria neno lile la ndugu yake Yusuf mkarimu (a.s) akasema (s.a.w.w): “Leo hakuna lawama juu. Nendeni nyinyi mpo huru”. Hayo aliyasema baada ya kuwauliza: Mnadhani nitanyaje dhidi yenu? Wakasema: “Wewe ni ndugu mwema na mwana wa ami mwema”[19], na huku ni kukiri kwa juu ya utukufu wa dhati ya bwana mtume (s.a.w.w).

6.       Kuhimiza juu utafutaji wa elimu na kujifunza kila kitachomuweka mtu karibu na Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kinamuongezea kumjua Yeye. Imesemekana kuwa ndani ya Qur’ani kuna zaidi ya aya mia tano (500) zinazihimiza juu ya elimu, na kutafakari na kuwasifu wasomi, na huku zikitia dosari ujinga na wajinga na zikieleza mwisho wao. Qur’ani imefikia hatua ya kuifanya sifa ya ujuzi na elimu na kumjua Mwenyezi Mungu kuwa ni sababu ya kuongezewa nguvu waumini dhidi ya maadui wao mara kumi zaidi, kama inavyofahamika mwishoni mwa aya ifuatayo:

[يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُواْ مِئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّئَةٌ يَغْلِبُواْ أَلْفاً مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُواْ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لاَّ يَفْقَهُونَ]

“Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja katika walio kufuru. Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu”[20], wakati subira ambayo ni katika sababu muhimu za ushindi umepewa hadhi ya kuzidisha nguvu mara moja tu:

 [الآنَ خَفَّفَ اللّهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفاً فإن يَكُن مِّنكُم مِّئَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُواْ مِئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُواْ أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللّهِ وَاللّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ]

“Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri”[21].



[1]. Tah’dhiibul Ahkaam: 6/176.

[2]. Surat Muhammad: 10.

[3]. Surat Al-Imran: 11.

[4]. Surat Ar-Rahman: 60.

[5]. Surat Al-A’araaf: 96.

[6]. Surat Al-Mumtahana:

[7]. Surat Al-An’aam: 153.

[8]. Surat Al-Hadiid: 16.

[9]. Surat Ad-Dukhan: 25-29.

[10]. Surat Al-Baqarah: 219.

[11]. Surat An-Nisaa: 43.

[12]. Surat Al-Maidah: 90.

[13]. Surat Al-A’raaf: 1-2.

[14]. Surat Hud: 12.

[15]. Surat An-Nahl: 127-128.

[16]. Surat Al-Imran: 186.

[17]. Surat At-Tur: 48.

[18]. Surat Yusuf: 92.

[19]. Tafsirun Nuur At-Taqalayn: 2/460.

[20]. Surat Al-Anfaal: 65.

[21]. Surat Al-Anfaal: 66.