QUR’ANI NI TIBA YA MARADHI YETU YAKIJAMII
QUR’ANI NI TIBA YA MARADHI YETU YAKIJAMII
Sasa umefika wakati tutumie nguvu na juhudi zetu katika kufaidika na uwezo wa Qur’ani wa kuyatibu maradhi ya kibinadamu na tunufaike na nguvu ya Qur’ani kwenye kuufikisha ubinadamu kwenye kilele cha ukamilifu, kwani Qur’ani ni ufunuo, ni yenyekudumu, na yenye kutoa muongozo mpaka siku ya Kiyama. Kudumu chwake ndio nguvu yake ya kubaini maeradhi na ndio nguvu yake ya kutoa tiba na dawa kwa kila jamii, kila zama na kila sehemu. Hivyo hatuna budi kuishaurisha Qur’ani na kuitaka itupe tiba ya mangojwa na maradhi yetu yakijamii nay a mtu mmoja mmoja.
Jamii ikikumbwa na mfarakano na mparaganyiko, basi tiba yake ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعاً وَلاَ تَفَرَّقُواْ]
“Shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu kwa pamoja wala msifarakane”[1], baada ya kutambua kuwa kamba ya Mwenyezi Mungu ni Qur’ani na Ahlul-bayt (a.s) kwa mujibu wa hadithi tukufu.
Umma ukisibiwa na woga na hofu ya kifo, basi tiba yake ni maneno ya Mwenyezi Mungu:
[أَيْنَمَا تَكُونُواْ يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ]
“Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu”[2], na kauli yake:
[قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فإنه مُلاقِيكُمْ]
“Sema: Hayo mauti mnayoyakimbia, bila ya shaka yatakukuteni”[3].
Na ikiwa jamii itapatwa na mabalaa na misiba, basi posa na tiba yake ni aya Mwenyezi Mungu:
[أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُواْ الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْاْ مِن قَبْلِكُم مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَاء وَالضَّرَّاء وَزُلْزِلُواْ حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ وَالَّذِينَ آمَنُواْ مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللّهِ أَلا إِنَّ نَصْرَ اللّهِ قَرِيبٌ]
“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu”[4].
Pindi jamii inapohisi hali ya kukata tamaa, basi itambue kuwa tiba yake ni kauli ya Mwenyezi Mungu:
[وَلاَ تَيْأَسُواْ مِن رَّوْحِ اللّهِ إِنَّهُ لاَ يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللّهِ إِلاَّ الْقَوْمُ الْكَافِرُونَ]
“Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa watu makafiri”[5],
[وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلاَّ الضَّآلُّونَ]
“Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea?”[6],
[إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الأَشْهَادُ]
“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walioamini katika uhai wa duniani na siku wataposimama Mashahidi”[7].
Na ikiwa majukumu ya kupotea na dhulma tutawabebesha wengine au tukazibebesha zama, basi natusome maneno ya Mwenyezi Mungu yasemayo:
[وَمَا أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٍ فَمِن نَّفْسِكَ]
“Na ovu liliokusibu linatokana na nafsi yako”[8],
[إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ]
“Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wao wabadili yaliyomo nafsini mwao”[9],
[وَمَا ظَلَمَهُمُ اللّهُ وَلَكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ]
“Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali wao wenyewe walidhulumu nafsi zao”[10].
Na pindi watu watakapo rejea kwenye kupenda wingi (mali na watoto) hali yao ikiwa ni sawa na msemo huu kwamba: “Kukusanyika na watu ni iddi” bila kutafakari na kufahamu, majibu ya Qur’ani kwao yatakuwa kama ifuatavyo:
[وَمَا أكثر النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ]
“Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi”[11],
[وَإِن تُطِعْ أكثر مَن فِي الأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللّهِ إِن يَتَّبِعُونَ إِلاَّ الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلاَّ يَخْرُصُونَ]
“Na ukiwatii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu”[12],
[وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُمْ بِاللّهِ إِلاَّ وَهُم مُّشْرِكُونَ]
“Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina”[13].
Na miongoni mwa maradhi ya kijamii ambayo Qur’ani imeyatolea tiba ni suala kueneza uvumi[14]. Na huu ni ugonjwa hatari sana unao isambaratisha jamii na kukutikisa uwepo wake na kuzigonganisha fikra zake. Katika kulitibu tatizo hili Qur'an’ inasema:
[وَإِذَا جَاءهُمْ أَمْرٌ مِّنَ الأَمْنِ أَوِ الْخَوْفِ أَذَاعُواْ بِهِ وَلَوْ رَدُّوهُ إِلَى الرَّسُولِ وَإِلَى أُوْلِي الأَمْرِ مِنْهُمْ لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ وَلَوْلاَ فَضْلُ اللّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لاَتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلاَّ قَلِيلاً]
“Na linapowafikia jambo lolote liliohusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu”[15], na aya zingine nyingi ambazo hutoa tiba ya maradhi yetu ya muda mrefu.
[1]. Surat Al-Imran: 103.
[2]. Surat An-Nisaa: 78.
[3]. Surat Al-Jumu’a: 8.
[4]. Surat Al-Baqarah: 214.
[5]. Surat Yusuf: 87.
[6]. Surat Al-Hijr: 56.
[7]. Surat Al-Ghaafir: 51.
[8]. Surat An-Nisaa: 79.
[9]. Surat Ar-Ra’d: 11.
[10]. Surat Al-Imran: 117.
[11]. Surat Yusuf: 103.
[12]. Surat Al-an’aam: 116.
[13]. Surat Yusuf: 106.
[14]. Baadae kilichapwa kijitabu kuhusiana mada hii, katika mfululizo ujulikanao kwa jina la: (Kuilekea Jamii Iliyosafi)
[15]. Surat An-Nisaa: 83.