SIFA ZA JAMII YA KIJAHILIA KWA MUJIBU WA QUR’ANI

| |times read : 715
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

SIFA ZA JAMII YA KIJAHILIA KWA MUJIBU WA QUR’ANI

 

       Sifa ya kwanza miongoni mwa sifa za kijahilia ni kuwaabudu watu badala ya Mwenyezi Mungu aliye tukuka. Na ibada maana yake ni kutii na kutawalisha kama ilivyo pokelewa kutoka kwa Ahlul-bayt (a.s) katika tafsiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu:

 

[اتَّخَذُواْ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَاباً مِّن دُونِ اللّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُواْ إِلَهاً وَاحِداً لاَّ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ]

Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu, na Masihi mwana wa Mariam. hali hawakuamrishwa isipokuwa wamuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo”[1]. Alisema (a.s):

(أما والله ما دعوهم إلى عبادة أنفسهم، ولو دعوهم ما أجابوهم، ولكن أحلوا لهم حراما، وحرموا عليهم حلالا فعبدوهم من حيث لا يشعرون)

“Wallah! Hawakuwaita wawaabudu wenyewe, na laiti wangeli waita kwa hilo wasingeli wakubalia, lakini waliwahalalishia haramu, na wakawaharamishia halali, wakawaabudu bila ya wenyewe kujua”[2]. Hii ni aina ya ibada ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu iliyokuwa katika jamii ile ya kijahilia, na ndio sababu sura ya kwanza ya Qur’ani iliyo teremka ilikuja kuwataka kuuacha kumtii asiyekuwa Mwenyezi Mungu: “Akome! Usimtii”[3]. Wakati ule kulikuwa na utii wa miungu wengi:

[مَا نَعْبُدُهُمْ - أي الأصنام - إِلا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّهِ زُلْفَى]

 “Hatuwaabudu -masanamu- isipokuwa wapate kutujongeza kwa Mwenyezi Mungu[4] ,

[وَلاَ يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضاً أَرْبَاباً مِّن دُونِ اللّهِ]

“Wala baadhi yetu wasiwafanye baadhi kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu”[5],

[إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلا]

 “Mola wetu! Hakika tumewatii mabwana wetu na wakubwa wetu, nao ndio walio tupoteza njia”[6],

[فَاتَّبَعُواْ أَمْرَ فِرْعَوْنَ وَمَا أَمْرُ فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ]

 “Wao wakafuata amri ya Firauni, na amri ya Firauni haikuwa yenye uongofu”[7],

 [فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيّاً]

“Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha sala, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta malipo ya ubaya”[8],

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللّهُ قَالُواْ بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لاَ يَعْقِلُونَ شَيْئاً وَلاَ يَهْتَدُونَ]

 “Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?”[9],

 [وَمِنَ النَّاسِ مَن يُجَادِلُ فِي اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَانٍ مَّرِيدٍ، كُتِبَ عَلَيْهِ أَنَّهُ مَن تَوَلاهُ فإنه يُضِلُّهُ وَيَهْدِيهِ إِلَى عَذَابِ السَّعِيرِ]

“Na miongoni mwa watu wapo wanao bishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya ilimu, na wanamfuata kila shet'ani aliye asi. Ameandikiwa kwamba anaye mfanya kuwa rafiki, basi huyo hakika atampoteza na atamwongoza kwenye adhabu ya Moto mkali”[10],

[إِذْ جَعَلَ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي قُلُوبِهِمُ الْحَمِيَّةَ حَمِيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ]

 “Wale walio kufuru walipotia nyoyoni mwao hasira, hasira za kijinga (za kijahilia)”[11].

 

       Hawa ni baadhi ya miungu wa enzi za ujahilia wa zamani waliokuwa wakiabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu aliye tukuka. Miungu ambao walikuwa ni: masanamu, wasomi wasio na nyoyo safi, watawala, matamanio ya nafsi iamrishayo maovu, Ibilisi, hasira na ada walizo zirithi kutoka kwa mababa zao. Lakini msingi wa yote hayo ulikuwa ni kufuata matamanio:

[فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءهُمْ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ لا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Na ikiwa hawakukujibu, basi jua kuwa wanajifuatia tu matamanio yao. Na nani aliyepotea zaidi kuliko yule anayefuatia matamanio yake pasipo muongozo utokao kwa Mwenyezi Mungu? Bila shaka Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu”[12].

       Lakini je hali ya watu wa leo hii imebadilika? Na hapa sikusudii wale watu wanaojiita kuwa wameendelea, kwani ni wazi kuwa wao wamezama zaidi katika dimbwi la ujahilia kuanzia kichwani kadi miguuni, bali ninakusudia wale wajiitao waislamu hali ya kuwa wamepanda jahazi la hao hao makafiri. Waislamu ambao wamezama katika kuyatii matamanio na kila kinacho amrishwa na miungu wao wapya kama vile: michezo, Sanaa na baadhi ya nadharia na kanuni zenye kupotosha. Leo hii bado amri za mabwana na wakubwa kama vile: kiongozi wa ukoo au watu wenye vyeo umekuwa unatekelezwa bila hata kuchunga mipaka ya sharia ya Mwenyezi Mungu, wamekuwa akihalalisha yale yaliyo haramishwa na Mwenyezi Munngu na kuharamisha yale aliyo yaharamisha. Hali kadhilika mila na ada za mababa na mababu zimeendelea kuheshimiwa kuliko sheria za Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba jamii iko radhi kumuasi Mwenyezi Mungu kuliko kuachana na mila na desturi hizo. Kana kwamba ndimi zao zinasema: “Moto ni mora kuliko udhalili”, kunyume kabisa na Uislamu alioudhirisha Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala, pindi aliposema:

الموت أولى من ركوب العار    والعار أولى من دخول النار

Kufa ni bora kuliko kuukubali udhalili***na udhalili ni bora kuliko kuingia motoni

      Jambo hili la kufadhilisha mida na desturi za mababa na mababu niko wazi katika mwenendo wa watu wanaoshi kimakoo na wengineo. Ama mwanamke amekuwa ni wakutii mapenzi, na kwenda kwenye maduka ya mavazi na kufuata usasa na kila kinacholetwa wamagharibi, mfano: mavazi na vipodozi hata kama vitakuwa vinaenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu. Sasa ikiwa hali ndio hii, je kuna aina yoyote ile ya ibada na utii vilivyosalia na havifanyi na jamii ya kileo? Hii ni kwa kiwango cha shirki ya wazi wazi. Na Qur’ani inatujulisha kwa miungu wote siku ya Kiyama watawakana waliowaabudu. Lakini siku hiyo majuto yao hayatawanufaisha kitu:

[وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللّهِ أَندَاداً يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللّهِ وَالَّذِينَ آمَنُواْ أَشَدُّ حُبّاً لِّلّهِ وَلَوْ يَرَى الَّذِينَ ظَلَمُواْ إِذْ يَرَوْنَ الْعَذَابَ أَنَّ الْقُوَّةَ لِلّهِ جَمِيعاً وَأَنَّ اللّهَ شَدِيدُ الْعَذَابِ، إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُواْ مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُواْ وَرَأَوُاْ الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الأَسْبَابُ، وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُواْ لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّؤُواْ مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ]

“Na miongoni mwa wako wanaowafanya miugu wasiokuwa Mwenyezi Mungu Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika na wakiwapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi. Na walio dhulumu wangelijua watakapo iona adhabu kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu na kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao”[13].

       Sehemu nyingine Qur’ani inawaelezea miungu hawa ambao huabudiwa na wanadamu kwa kuwapa mamlaka na utiifu badala ya Mwenyezi Mungu kwa musema:

[مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاء كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ]

“Mfano wa wale walio waliowafanya waungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui ajitandiaye nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti wangelijua”[14], na inasema sehemu nyingine:

 

[وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَعْمَالُهُمْ كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إذا جَاءهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئاً وَوَجَدَ اللَّهَ عِندَهُ فَوَفَّاهُ حِسَابَهُ وَاللَّهُ سَرِيعُ الْحِسَابِ]

“Na wale waliokufuru vitendo vyao ni kama mazigazi uwandani. Mwenye kiu huyadhania ni maji, hata akiyaendea hapati chochote. Na humkuta Mwenyezi Mungu hapo, naye humpa hisabu yake sawa sawa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu”[15].

       Kimsingi hii bahathi inayofaa umuhimu, kwani huwazindua wanadamu wauone upungufu wa imani na itikadi zao na kwamba waone ni namna gani walivyojitenga na tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ya kweli na kwamba utiifu wako kwa Mwenyezi Mungu umeshuka kuliko wa wanavyo watii waungu hawa mbali mbali. Bahathi hii inafaa hata tukaiita kwa jina “Masanamu ya ujahilia wa kileo”, masanamu ambayo hatari imefichikana hadi kwa waumini achilia mbali wasiokuwa wao.

      Ama tukija kwa kile kijulikanacho kama shirki iliyojificha, hapa msiba unakuwa mkubwa zaidi, kwani mara chache unaweza kuona kitendo kifanywacho kwa ikhlasi na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee hata mwenye kufanya kitendo hicho anaweza kudhania kuwa kweli kakifanya kwa ikhlasi. Kwa mfano, ni kwanini mtu aandike jina lake kwenye bango kubwa pindi anapojenga msikiti ikiwa kweli kafanya hivyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Ikiwa mtu na ikhlasi kweli ni kwanini anasimanga na kuzungumza kwa kile alichokitoa?

       Sifa ya pili miongoni mwa sifa za kijahilia ni kwamba sheria zinanadhimu mambo yao na kutatua magomvi yao siko mbali na sheria za Mwenyezi Mungu: “Je wanataka hukumu za kijahili?”[16] Kwa mujibu wa Qur’ani ni kuwa kila hukumu isiyokuwa ile aliyo iteremsha Mwenyeze Mungu basi hiyo ni hukumu ya kijahilia. Lakini kwa bahati leo tunaziona jamii nyingi ziishizo kwa mfumo wa makabila huhukumiwa na mila na desturi ambazo Mwenyezi Mungu hakuziletea uthibitisho, bali zimewekwa na watu wasijua na walioko mbali kabisa na Mwenyezi Mungu. Hilo ni kama mfano tu, lakini nawe pia unaweza kutazama makundi mengine ya kijamii ukapata mifano ya namna zinavyoishi kwa kufuata sheria isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu. Bila shaka mwenyewe unajione ni namna gani mataifa ya ulimwengu yanavyo ongozwa na kanuni na sheria zilitungwa na mwanadamu mwenye mapungu, asiye miliki kheri ya nafsi yake wala shari, na asiywezea kuona zaidi ya ncha ya pua lake. Utamuona kila siku akibadili kifungu cha sheria kwa kuongeza kupengele au kukifuta, na hugundua mapungufu mengineo kila mara na hivyo hurekebisha kasoro zake. Tukirejea kwenye hadithi tunakuta zao zikieleza kuwa kila upingaji wa sheria ya Mwenyezi Mungu au kutotenda kwa mujibu wake kuwa ni ujahilia na ujinga. Imekuja katika hadithi kuwa: “Yeyote atakaye kufa bila kutoa wasia, basi atakuwa amekufa kifo cha kijahilia”[17].

       Kwa mfano, Firauni anasema: “Sikupeni ushauri ila ile niliyoiona”[18], hali hii sio maalumu kwa ajili ya Firauni bali hali inayojirudia daima na kwa watu wengi ambao hujipa mamlaka ya kutunga sheria badala ya Mwenyezi Mungu.

       Sifa nyingine ya ujahilia ni upotovu wa imani, kama ilivyo ashiriwa katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “wanamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyokuwa ya haki, dhana ya kijahilia (kijinga/kikafiri)”[19], kwa mfano, walikuwa wakiamini kwamba vyovyote mwanadamu atakavyo tenda madhambi anaweza kuokaka na adhabu iwapo tu atatoa kafara kwa miungu! Hali hii pia unaweza kuishuhudia katika jamii yetu kutokana na makhatibu wa mimbari ya Imamu Hussein (a.s) alivyo wakaririsha watu kwamba tone moja la machozi atakalolidondosha muumini kwa ajili ya Imam Husseini (a.s) basi linamtosha kuingia peponi hata kama atakuwa katenda maovu na madhambi makubwa! Haya wameyasema kufatia hadithi isemayo:  

(من بكى على الحسين ولو مقدار جناح بعوضة وجبت له الجنة)

“Yeyote atakaye mlilia Imamu Hussein walau (chozi lake likawa) kwa kiwango cha bawa la mbu, basi Pepo itakuwa wajubu kwake”[20], lakini pia wakatumia ubeti huu wa mshairi kuwa ni hoja:

 

فإنَّ النار ليس تمس جسماً            عليه غبار زوار الحسينِ

Na hakika moto hautaugusa mwili *** wenye vumbi la mazuwari wa Hussein (a.s).

       Ni kweli kwamba hatukanush utukufu wa Imamu Hussein (a.s) kwa Mwenyezi Mungu. Bila shaka anastahiki kutukuzwa kwa namna hii, bali hata zaidi ya hivo. Lakini kutukuzwa huko inabidi kuwe ni sehemu ya sababu ambayo itakamilishwa na sehemu nyingine ambayo ni katika masharti ya kuingia peponi, ambapo sababu ya kwanza kabisa ni kumtii Mwenyezi Mungu katika maamrisho yake na makatazo yake. Qur’ani yenyewe inaeleza bayana kwamba: “Wala hawamuombei yeyote ila yule anayemridhia Mwenyezi Mungu”[21], na hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) inasema: “Mwenye kupuuza sala hataupata uombezi wetu”[22], hali kadhali madai hayo hayakinzana na aya ifuatayo:  

 

[فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْراً يَرَهُ، وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرّاً يَرَهُ]

“Basi anayetenda chembe ya wema atauona, na atakayetenda chembe ya uovu atauona”[23], isipokuwa ayadiriki matendo yake kwa kufanya toba yakweli.

       Upotovu huu wa imani madhara yake ni makubwa mno, kwani huwaweka watu mbali na dini na hupunguza ufahamu wao baada kulewa na idikadi hizi zilizo mbali kabisa na Qur’ani na wakaacha kuifanyia kazi Qur’ani.

       Katika alama za ujahilia pia ni kutojistiri, na kujishaua, na kuonyesha viongo vya uzuri, na kutojiheshimu na kuenea ausherati, anasema Mwenyezi Mungu: “Wala msijishauwe kwa mishauwo ya kijahilia ya kizamani”[24]. Na bila shaka jamii ya kileo imezipita nyumati zilizopita katika ufaiki na uovu, halikadhali katika mitindo ya ushawishi, na kupotosha, na kuwaingiza watu kwenye uchafu, na kurahisisha nyenzo za kisasa ili kueneza uchafu huo, kama ulivyokuwa ujahilia wa zamani nao pia ulikuwa ukivumbua njia na kuweka kanuni mbalimbali zinazokidhi hisia zao za kinjisia kwa mitindo mbalimbali ya kishetani. Kwa mfano: Makuraishi walipasisha kanuni ya kuharamisha kufanya tawafu kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu Makka mtu akiwa amevaa nguo yake ya zamani, kwa hoja kuwa inawezekana mwenye nayo akawa aliwahi kumuasi Mwenyezi Mungu akiwa ameivaa na kafanya madhambi, hivyo ikawa ni lazima afanye tawafu ndani ya nguo ya watu Makka, au nguo mpya au atufu akiwa uchi.

       Na wafuasi wa shetani leo hii zaidi ya kumbi za ouvu, wameanzisha njia mbali mbali za kueneza uchafu kwa jina michezo. Michezo ambayo yafanyikayo ndani yake si madogo kuliko ya yale yatendekayo kwenye kumbi za ouvu. Bali makumbi zina nafuu kuliko michezo hiyo, kwa sababu zipo ufichoni na watu wengi hawayapendi kwani huogopa kupoteza hishima zao. Lakini katika michezo maovu hufanyika hadharani na mbaya zaidi ni kuwa mwenyekufanya uovu huo hujifaharisha kwao na wote humpongeza! Bila shaka utakuwa umeona ni namna gani watu walivyofanywa midoli mikononi mwa shetani, naye huwatumia atakavyo. Hali ipo hivyo hivyo katika anuwani na majina mwengine, ukiangalia kwa mfano: matamasha kumsaka mrembo, au mauonyesho ya navazi, au sanaa nyinginezo, vyote ni ouvu, lakini kwa kutumia majina na anuwani zinazokubalika kwenye jamii kiasi kwamba haponi mtu isipokuwa yule aliyehifadhiwa na Mwenyezi Mungu. Na malengo ya hayo yote ili wanadamu waishi kinyama na katika vurugu za kijinsia huku moto wa matamanio ukiendelea kuwaka kiasi kwamba hauishi wala hausazi.

       Na miongoni mwa sifa za kijahilia ni upotovu wa fikra na mitazamo ya maisha. Kwa mfano: baadhi wa watu enzi za ujahilia wa kale, walikuwa wanakataa kuwaoza mabinti zao kwa watu wasiokuwa katika ukoo au kabila lao, kwakuwa walikuwa wakijiona kuwa wao ni wabora kuliko wengine na walijulikana kwa la ‘Humus’ ambao ni Makuraishi. Leo pia katika ujahilia wa kileo hali hiyo ipo. Kuna kundi la watu wengi, na mfano ulio wazi zaidi ni baadhi ya masayyidi (mashifu) ambao nasaba yao inanasibishwa kwa bwana mtume (s.a.w.w), wao hawawaozeshi mabinti zao isipokuwa kwa ambaye ni sayyidi kama wao, mpaka babinti hao wakuwa wakikaa mda mrefu manyumbani mwao na mwisho hukoza ndoa na kwa njia hiyo wanapoteza haki yao ya kisheria ya kufurahia familia na wao wakapata furaha ya umama. Haya yote sababu yake ni mitazo mibovo ya kijahilia. Ni mitazo duni zana unapo iangalia misingi ya Qur’ani, kwa Mwenyezi Mungu anasema:  

[خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالاً كَثِيراً وَنِسَاء]

“Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akauumba kutokana na nafsi hiyo wapili wake (mkewe). Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi”[25], vilevile ukiangalia mafunzo ya bwana Mtume (a.s.w.w) aliposema:

(إذا جاءكم من ترضون خلقه ودينه فزوجوه)

Atakapo kufikieni mtu ambaye mnairidhia dini tabia yake na dini yake, basi muozesheni”[26]. Hivyo ikiwa utukufu wao ni kwa sababu ya nasaba yao kwa bwana mtume (s.a.w.w), bila shaka utukufu wa bwana mtume ni kwa sababu ya Uislamu na kuiifu wake kwa Mwenyezi Mungu, na si kwa kuwa yeye ni Muhammad mwana wa Abdallah, anasema Mwenyezi Mungu:   

[لَئِنْ أَشرَكتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ]

“Bila shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu vitendo vyako zitaharibika na lazima utakuwa miongoni mwa wenye khasara”[27], na:

[وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الأَقَاوِيلِ، لأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ، ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ، فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ]

Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu, bila ya shaka tungelimshika kwa mkono wa kulia, kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo. Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia naye”[28], na bwana mtume (a.s) anasema: “Lau ningeliasi bila shaka ningeliporomoka”[29]. Basi wana hadhi gani hao ambao hufanya biashara kwa jina lake (s.a.w.w) ilihali wanakhalifu sheria yake?

        Vilevile katika alama za ujahilia wa kileo ni kuhitalifiana maadili na mizani ambavyo kipitia hiyo wanadamu hutofautiana kati ya ile kimungu na ile shetani. Qur’ani inaeleza wazi kwamba: 

[إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ]

“Hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni yule amchaye zaidi”[30], na:

[قُلْ بِفَضْلِ اللّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَلِكَ فَلْيَفْرَحُواْ هُوَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ]

“Sema: Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na kwa rehema zake, basi wafurahi, hiyo ni bora kuliko wanavyo vikusanya[31]”, wakati uhajilia ni kujifakharisha kwa mali, na vyeo na wingi wa watoto:

 [أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ، حَتَّى زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ]

“Kumewashughulisheni mno kutaka wingi wa mali, mpaka mmeingia makaburini”[32], na:

 [وَقَالُوا نَحْنُ أكثر أَمْوَالاً وَأَوْلاداً وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ]

“Na wakasema: Sisi tuna mali nyingi na watoto wengi na wala sisi hatukuwa wenyekuadhibiwa”[33], na mambo haya wako wazi kiasi kwamba sina haja ya kutaja mifano, na aya hizi zifuatazo zinauweka wazi ulingano huu baina ya maadili ya kimungu nay ale ya kijahilia:

[زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاء وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ذَلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَاللّهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ، قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَلِكُمْ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللّهِ وَاللّهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ]

“Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na vijana wa kiume, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi wazuri wazuri, na wanyama, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema. Sema: Je, nikwambieni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wacha Mungu ziko Bustani kwa Mola wao zipitazo mito chini yake. Watakaa humo milele na wake waliotakaswa, na wanazo radhi za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake”[34], pia anasema:

 

 [وَمَا أَمْوَالُكُمْ وَلا أَوْلادُكُم بِالَّتِي تُقَرِّبُكُمْ عِندَنَا زُلْفَى إِلا مَنْ آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحاً فَأُوْلَئِكَ لَهُمْ جَزَاء الضِّعْفِ بِمَا عَمِلُوا وَهُمْ فِي الْغُرُفَاتِ آمِنُونَ]

Na si mali zenu wala watoto wenu watakao kukaribisheni kwetu katika daraja, isipokuwa aliyeamini na kutenda mema. Basi hao watapata malipo mardufu kwa walioyafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa”[35].

        Na sifa zizazoshirikisha ujahilia wa kale na wa kileo ni kuenea maadili mabaya. Mifano iliyowazi ni kama vile: kunywa pombe, na kupunja katika mizani, na kudanganya na ushoga. Mwenyezi Mungu anasema:

[وَتَأْتُونَ فِي نَادِيكُمُ الْمُنكَرَ]

“Na manafanya maovu katika mikusanyiko yenu?[36],

[وَلاَ تَبْخَسُواْ النَّاسَ أَشْيَاءهُمْ]

“Wala msiwapunje watu vitu vyao”[37],

[وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ، الَّذِينَ إذا اكْتَالُواْ عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ، وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ]

“Ole wao wapunjao! Ambao wanapojipimia kwa watu hupokea kamili. Na wanapowapimia watu kwa kipimo au kwa mizani wao hupunguza”[38], wamefikia hadi wanamdhihaki watu wema:

[وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلاَّ أَن قَالُواْ أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ]

“Na hayakuwa majibu ya kaumu yake isipokuwa kusema: Wafukuzeni katika mji wenu, kwa sababu wao ni watu wanaojitakasa”[39], kiasi kwamba Ja’far mwana wa Abu Talib historia imesajili jina lake kuwa ni miongoni mwa watu waliojiharamishia kunywa pombe na kufanya uzinzi enzi za ujahilia. Na miongoni mwa maadili mabaya waliyokuwa nayo kipindi cha ujahilia wa kale ni mwenye nguvu kumnyonya dhaifu, na kutokuwa na tabia hata za kiubinadamu achilia mbali zile za kimungu, kwani jambo muhimu kwao yalikuwa ni manufaa binafsi. Na leo maendeleo ya yamekuwa ni kumaliza mataifa na kuteketeza mimea na viumbe kwa ajili ya masilahi ambayo kwao ndio kila kitu. Ama lengo halisi na la kweli, ambalo ni radhi za Mwenyezi Mungu na kufaulu huko Akhera, limekuwa likionekana kuwa ni kurudi nyuma na kukosa maendeleo! Anasema Mwenyezi Mungu:

 [وَطَآئِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللّهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الأَمْرِ مِن شَيْءٍ قُلْ إِنَّ الأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّهِ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لاَ يُبْدُونَ لَكَ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الأَمْرِ شَيْءٌ]

“Na kundi jingine limeshughulishwa na nafsi zao, hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyokuwa ya haki, dhana ya kijinga (kijahili na kikafiri). Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo hili? Wambie: Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyo kudhihirishia. Wanasema: Tungekuwa na lolote katika jambo hili tusingeuliwa hapa”[40], haya ndio malengo yao ambayo wanaishi kwa ajili yake kuwa: Tuna lolote katika jambo hili?

       Na katika sifa muhimu za kijahilia ambayo ndio sababu ya kubatikana kwake, ni kuacha kuamrisha mema na kukataza maovu. Na hili ni alilolohatahadharisha bwana mtume (s.a.w.w) aliposema:

(كيف بكم إذا فسدت نساؤكم وفسق شبابكم ولم تأمروا بالمعروف ولم تنهوا عن المنكر؟ فقيل له: ويكون ذلك يا رسول الله؟ فقال: نعم، وشر من ذلك، كيف بكم إذا أمرتم بالمنكر ونهيتم عن المعروف؟ فقيل له يا رسول الله ويكون ذلك؟ فقال (صلى الله عليه وآله): وشر من ذلك، كيف بكم إذا رأيتم المعروف منكراً والمنكر معروفاً)

“Mtakuwaje nyinyi pindi wanawake zenu watakapo haribika, na vijana wenu wakawa na tabia mbaya, na mema yasiamrishwe na maovu kukatazwa? Wakamuuliza: Je hilo litakuja kutokea? Akasema: Ndio, na mbaya kuliko hayo, mtakuwaje pindi mtakapo amrisha maovu na mkataza mema? Je hilo litakuja kutokea? Wakamuuliza. Akasema: Ndio, na mbaya kuliko hilo, mtakuwaje pindi mtakapo liona jambo jema kuwa uovu na ouvu kuwa ni wema”[41]. Na huku ndiko jamii za kileo zilikofikia. Na kwa mujibu wa Qur’ani ni kwamba tatizo linaanzia kwa wasomi wa dini au wanazuoni kwa sababu ya kupuuzia na kuchelewa kutekeleza wadhifa wao, na mfano mzuri wa wanazuoni ni nyinyi enyi wanafunzi na wakubwa vyuo vya kidini. Mwenyezi Mungu anasema:

[وَتَرَى كَثِيراً مِّنْهُمْ يُسَارِعُونَ فِي الإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ، لَوْلاَ يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالأَحْبَارُ عَن قَوْلِهِمُ الإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُواْ يَصْنَعُونَ]

“Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi, na uadui, na ulaji wao vya haramu. Bila shaka wayafanyayo hayo ni maovu mno. Mbona hao wanazuoni na makohani wao hawawakatazi maneno yao ya dhambi, na ulaji wao vya haramu? Bila shaka wayafanyayo ni maovu mno”[42],

 

[كَانُواْ لاَ يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ مَا كَانُواْ يَفْعَلُونَ، تَرَى كَثِيراً مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ الَّذِينَ كَفَرُواْ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ اللّهُ عَلَيْهِمْ وَفِي الْعَذَابِ هُمْ خَالِدُونَ]

Hawakuwa wenye kukataza maovu waliyokuwa wakiyafanya, bila shaka ni maovu mambo waliyokuwa wakiyafanya. Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na makafiri. Hakika ni maovu yaliyotangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia, nao watadumu katika adhabu”[43].

       Na hii ni sifa nyingine ya jamii iliyojiweka mbali na Uislamu, yaani kuwafanya makafiri marafiki. Kuhusiana na ubaya huu anasema Amirulmuunina Ali Bin Abi Talib (a.s):

(أما بعد فإنه إنما هلك من كان قبلكم حيثما عملوا من المعاصي ولم ينههم الربانيون والأحبار عن ذلك، وأنهم لما تمادوا في المعاصي نزلت بهم العقوبات فأمروا بالمعروف ونهوا عن المنكر واعملوا أن الأمر بالمعروف والنهي عن المنكر لن يقربا أجلاً ولن يقطعا رزقاً)

“Ama baada ya hayo, hakika waliokuwa kabla yenu waliangamia pindi walipotenda maasi na wanazuoni na makohani wao hawakuwakataza hayo, nao walipokithirisha maasi, basi adhabu ziliwateremkia. Basi amrisheni mema na katazeni maovu, na mtambue kuwa kuamrisha mema na kukataza maovu hakuharakishi kifo wala hakupunguzi riziki”[44].

       Ukweli ni kwamba pasina kuisimamia faradhi hii hakutabia hadhi yoyote ile kwa waumini, si kwa Mwenyezi Mungu na mtume wake (s.a.w.w) tu, bali hata kwa maadui wao, kwani baina ya Makuraishi walikuwepo waumini wanaompwekesha Mwenyezi Mungu waliojulikana maah’nafi, yaani wale walioacha kuyaabudia masanamu na wakajishughulisha na kumuabudu Mwenyezi Mungualiyetukuka, lakini hata hivyo hawakuwa na thamani mbele ya Mushirikiana, wala hawakujali uwepo wao; kwa sababu wao waliacha faradhi hii adhimu.

       Ndio maana kutekeleza wadhifa na faradhi hii ni moja ya sifa za jamii ya Kiislamu:

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ]

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu”[45], na:

[وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ، الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الأُمُورِ]

Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote”[46],

 

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ]

Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu.”[47],

[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima”[48], na aya nyingizo nyingi, hapa hatuwezi kuziorodhesha zote, kwani bahathi hii malengo yake ni kutoa ishara tu na kufungua mlango wa fikra katika masuala haya, kwa sababu kila mlango ukiufungua hufunguka milango elfu moja kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu na wingi wa rehema zake.

       Kutawaliwa na hadithi za kubuni na mabo yasiyo na uhakika ni moja ya alama za ujahilia. Kwa mfano, Warabu walikuwa wakiichulia sauti ya kunguru na bundi kuwa ni nuksi, na sasa leo hii Wamagharibi na bila sababu yoyote ile nao wanaichukuli namba (13) kuwa ni nuksi. Wakati huo watabiri na makohani walienea kila mahala na wakawa na soko nzuri. Leo hii pia tunaona mwitikio mkubwa wa watu kwenda kwa wapiga ramli na wanajimu na mfano wa hivyo vinavyo fanywa na watu wasiojua na wakawaida.

       Sifa nyingine ya kijahilia ni kuwazuwia watu na Qur’ani na kuwatenga nayo mbali kwa njia mbalimbali. Hakika Nadhri ibin Al-Harith ambaye ni miongoni mwa watu waliokwenda katika miji ya Farsi na akajifunza habari za wafalme wao, na akawa akimfuata bwana mtume (s.a.w.w) kwa nyuma, mtume anapo nyanyuka kutoka kwenye kikao, basi Nadhri naye anakaa baina yao kisha anawasimulia visa vya wafalme wa Farsi, kisha anawauliza: Ni kati yetu mwenyekusimilia vizuri kuliko mwenzake, Mimi au Muhammad? Hivyo wakawa wanaisifia Qur’ani kuwa ni viza vya kale alivyo viandikisha, anavyosomewa asubuhi na jioni, au wakisema kuwa: hadithi za kuzua, au wakati mwingine walikuwa wakipiga makofi kwa sauti ya juu pindi mtume anaposoma ili kuzuwia isisikilizike. Qur’ani inasimulia matendo yao kwa kusema:

[وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لا تَسْمَعُوا لِهَذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ]

 Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur'ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda”[49], inasema pia:

 [وَإِن يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ]

“Na wakiona ishara hugeuka upande na husema: Hu uchawi tu unazidi uendelea”[50]. Na sasa ujahilia wa kisasa pia umekuwa ukiisifu Qur’ani kwa sifa zilezile za ujahilia wa kale, kwamba Qur’ani ni maneno ya Muhammad yatokanayo na fikra za kibinadamu wala sio ufunuo na wahai utokao kwa Mwenyezi Mungu. Wamejaribu kuandika vitabu kuhusu aya walizodhania kuwa zinakinzana, lakini waliposhindwa na Qur’ani ikaendelea kuthibitisha uwepo wake waliamua -kwa kila ukhabithi, vijanja na udanganyifu- kuifanya ipoteze maana yake kivitendo, na wakaiweka mbali na maisha halisia na wakaibadili ikiwa ni mfano wa kaswida na nyimbo ambazo huibwa na wasanii na wasikilizaji wake wakawa wakionyesha furaha zao sauti za juu wakisema: Allah! Allah! Ewe shaikh! Wameifanya Qur’ani kuwa ni kinga huivaa vifuani mwao au huitundika majumbani mwazo na si vinginevyo. Njia hii kama uonavyo ni hatari kuliko ile ya Nadhiri bin Al-Harith na mfano wake, kama ambavyo ni ujanja mbaya na matokeo yake ni hatari mno.  

     Katika matendo yaliyowazi ambayo husifika nayo majahili ni kung’ang’ania mila walizo zirithi kutoka walikuwa kabila yao, na kujilazimisha kuzifanyia kazi, na kutokuwa tayari kuachana nazo hata kama ziko kinyume na haki iliyothibiti kwa hoja na dalili. Bila shaka matendo haya ni tija itokanayo na ugumu wa moyo, kutokuwa na fikra salama na kuzitawaza hisia kwamba kitu kilichofanywa na vizazi vya mababa na mababu hujipatia utukufu ambao huwa vigumu kuuvunja. Kwa hakika Qur’ani tukufu imeikariri maana hii kwa wingi kiasi kwamba tunaweza kufahamu kuwa huu ni mtihani ambao manabii wote walikabiliana nao. Anasema Mwenyezi Mungu:    

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اتَّبِعُوا مَا أَنزَلَ اللّهُ قَالُواْ بَلْ نَتَّبِعُ مَا أَلْفَيْنَا عَلَيْهِ آبَاءنَا أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لاَ يَعْقِلُونَ شَيْئاً وَلاَ يَهْتَدُونَ]

Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka?”[51],

[إِنَّهُمْ أَلْفَوْا آبَاءهُمْ ضَالِّينَ، فَهُمْ عَلَى آثَارِهِمْ يُهْرَعُونَ]

Hakika waliwakuta baba zao wamepotea, na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao”[52],

[قَالُواْ أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللّهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ]

Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli”[53],

[بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِم مُّهْتَدُونَ، وَكَذَلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءنَا عَلَى أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَى آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ، قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَى مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءكُمْ قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ]

Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao. Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote isipokuwa watu wake waliodeka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao. Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa”[54]. Na aya mbili za mwisho zinaonyesha kwamba mtihani huu mkubwa kumkabili na kumkuta kila anayetaka kuiokoa jamii yake na akafanya juhudi za kuiimarisha, kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema: “Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kabla yako isipokuwa…”, na hali hii sio maalumu kwa mitume peke yao.

       Ujahilia wa kisasa hautofautiani na ule wa kale katika hili, kwani ushahidi wa hilo ni mwingi sana. Na kwa hika jamii zetu bado zinakabiliwa na ugonjwa wa kufuata ya kale kama asemavyo mwanafikra mmoja wa kihauza.

 

      Kutomjua Imam na kiongozi wa kweli nayo ni alama ya ujagilia na ujinga:   

(من مات ولم يعرف إمام زمانه مات ميتة جاهلية)

Yeyoye yule atakayekufa bila kumtambua na kumjua Imam wa zama zake, basi mtu huyo atakufa mauti ya kijahili (yaani atakufa kifo cha ukafiri)”[55].

      Na malengo ya kumtambua sio kulijua jina lake pekee, bali ni kuyajua kikamilifu majukumu yetu kwa Imam na kuyatekeleza ipasavyo. Na bila shaka upumgufu huu kwa Imam wetu wa zama (a.s) uko wazi. Lakini pia dua iliyopokelewa inaiuelezea ujahilia huu kwa kusema:

(اللهم عرفني نفسك فإنك إن لم تعرفني نفسك لم أعرف نبيك اللهم عرفني رسولك فإنك إن لم تعرفني رسولك لم أعرف حجتك اللهم عرّفني حجّتك فإنك إن لم تعرفني حجتك ضللت عن ديني)

Ewe Mwenyezi Mungu! Nifanye nikujue wewe, kwani iwapo hautanifanya nikakujua wewe bila shaka sitaweza kumjua mtume wake. Ewe Mwenyezi Mungu! Nifanye nimjue mtume wako, kwani iwapo hautanifanya nikamjua mtume wako, bila shaka sitaweza kumjua hoja wako. Ewe Mwenyezi Mungu! Nifanye nimjue hoja wako, kwani iwapo hautanifanya kumjua hoja wake bila shaka nitapotea katika dini yako”[56], kwa sababu upotevu katika dini ndio ujahilia na ujinga wenyewe.

       Na jambo hili linahitaji kudurusiwa kwa kina na kubainisha kwanini ni lazima kuwepo Imam na Hoja wa Mwenyezi Mungu kwa kila zama, lakini pia ni nini takilifu yetu katika kipindi hiki cha ghaiba na kufichikana Imam, na upi wadhifa wetu kwa Imam wakati huu, na majibu ya viulizo vingi vya maswali na mishkeli ya kifikra inayolizunguka jambo hili la Imam, mambo amabyo yamefichikana kwa waumini wengi ukiachilia mbali waiokuwa waumini, hali ya kuwa: “maimam ndio mlango wa Mwenyezi Mungu ambao hawezi kufikiwa isipokuwa kupitia mlango huo”[57]. Ni vipi atakwenda kwa Mwenyezi Mungu yule asiyeujua mlango wa kwenda kwake? Na kipi baada ya Mwenyezi Mungu isipokuwa upotovu uliyowazi.

       Sifa nyingine ya ujahilia ni kuyakubali mambo ya kimada pekee na kuyakanusha mambo ya ghaibu na yale yasiyo ya kimada. Anasema Mwenyezi Mungu:

[وَقَالُواْ إِنْ هِيَ إِلاَّ حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ]

Sema: Mola Mlezi wangu ameamrisha uadilifu, na mumuelekeze nyuso zenu kila mnapo sujudu, na muombeni Yeye kwa kumsafia Dini. Kama alivyo kuumbeni mwanzo ndivyo mtavyo rudi”[58],

 [وَقَالُوا مَا هِيَ إِلا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا يُهْلِكُنَا إِلا الدَّهْرُ وَمَا لَهُم بِذَلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلا يَظُنُّونَ]

Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao wanadhani tu”[59]. Na hapa Qur’ani huja kuwaazishia malengo watukufu watakayoishi kwa ajili yake:

[وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالإِنسَ إِلا لِيَعْبُدُونِ]

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi”[60],

[قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُواْ اللّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَهٍ غَيْرُهُ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُواْ إِلَيْهِ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ]

Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi”[61],

[ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلاَئِفَ فِي الأَرْضِ مِن بَعْدِهِم لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ]

Kisha tukakufanyeni nyiye ndio wenye kushika mahala pao baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyotenda”[62].

Hivyo, mwanadamu hakuumbwa kwenye huu dunia ili aje kujishughulisha na matamanio yake, bali amefanywa kuwa ni khalifa na kiongozi ardhini ili aijenge na kuifanya iwe shamba kwa ajili ya akhera yake, na Muumba wake humhesabia matendo yake ili aone ni vipi atafanya. Na Mwenyezi Mungu humkemea mwanadamu anayezama katika mambo ya kimada kwa kusema:

[أَيَحْسَبُ الإنسان أَن يُتْرَكَ سُدىً، أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَى، ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّى، فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَى، أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَى]

Ati binaadamu anadhani kuwa ataachwa bure? Kwani yeye hakuwa ni tone ya manii lilioshushwa? Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. Je, huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?”[63]. Ndio, umetakasika ewe Mwenyezi Mungu. Wewe ni muweza hilo na ni muweza wa kila jambo. Ni kweli kuwa hii haimanishi kumzuwia mwanadamu kuwa na fungu lake hapa duniani maadamu hajalifanya kuwa ndio lengo lake la mwisho. Bali anaweza kuwa na fungu na akalitumia kwa ajili ya lengo lake halisi, ambalo ni radhi ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

[وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الآخِرَةَ وَلا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ وَلا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ لا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ]

Na utafute, kwa aliyokupa Mwenyezi Mungu makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyokufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi”[64], hivyo upungufu na kasoro haviko kwenye kuipata dunia, kwani imesemwa kuwa: “Dunia ni shamba la Akhera”[65] na katika hadithi nyingine imekuja kwamba: “Dunia ni sehemu ya chumo kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu”[66]. Wao hufanya biashara isiyobwaga na Mwenyezi Mungu.

       Sifa nyingine ya kijahilia ni kugawanyika na kufarakana. Anasema Mwenyezi Mungu:

[وَلا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ، مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ]

Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni Sala, na wala msiwe katika washirikina. Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho”[67]. Yote hayo ni kwa sababu ya kupoteza kwao mhimili wa msingi ambao walipaswa kuushikilia, mhimili ambao ni kumpekesha Mwenyezi Mungu aliyetukuka na Kaaba ikafanywa kuwa ni alama yake.  Ama jamii iliyo mbali na Mwenyezi Mungu kwanza: hugawangika mataifa kwa miji, kiasi leo hii idadi ya mataifa duniani imefikia zaidi ya 180. Lakini pia hugawanyika kwa jinsia na matabaka mbalimbali ndani ya nchi moja, kisha hugawanyika kifikra, utamkuta huyu ana mlengo wa kikomunisti na mwengine mlengo wake ni wakibepari hali ya kuwa wote wana utaifa mmoja na dini moja. Wanatofautiana katika mawazo hata wakiwa dini moja, bali hata ndani ya madhehebu moja, na kila kundi utaliona likiwanyika makundi tofauti tofauti na kuendelea: “kila kikundi kinafurahia kilicho nacho”[68]. Na Qur’ani imekwishaelezea kuwa mgawanyiko huu ni moja ya adhabu za kujiweka mbali na njia ya Mwenyezi Mungu na dini yake, Qur’ani inaasema:

[قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَى أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعاً وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ]

Sema: Yeye ndiye Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au kukuleteeni fujo la mfarakano, na kuwaonjesha baadhi yenu jeuri ya wenzao. Tazama vipi tunavyo zieleza aya ili wapate kufahamu”[69], kisha Uislamu ukaja kuwakusanya na kuwaweka pamoja kwa Qur’ani hii, amesma Mwenyezi Mungu:

[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ وَاذْكُرُواْ نِعْمَةَ اللّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاء فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىَ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka”[70], na katika aya nyingine anasema:

[وَإِن يُرِيدُواْ أَن يَخْدَعُوكَ فإن حَسْبَكَ اللّهُ هُوَ الَّذِيَ أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ، وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الأَرْضِ جَمِيعاً مَّا أَلَّفَتْ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَكِنَّ اللّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima. Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na waumini waliokufuata”[71].

       Katika sifa zilizowazi za kijahilia pia ni kuogopa kifo na kukiogopa kila kinacho ashiria suala la umauti. Sababu ya hilo ni kwakuwa wapeipoteza Akhera na wakayafanya malengo yao kuwa kuzishibisha hisia zao na mahitaji yao: 

 

[قُلْ إِن كَانَتْ لَكُمُ الدَّارُ الآَخِرَةُ عِندَ اللّهِ خَالِصَةً مِّن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ، وَلَن يَتَمَنَّوْهُ أَبَداً بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ وَاللّهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمينَ، وَلَتَجِدَنَّهُمْ أَحْرَصَ النَّاسِ عَلَى حَيَاةٍ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُواْ يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَمَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَن يُعَمَّرَ وَاللّهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ]

Sema: Ikiwa nyumba ya Akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti kama nyinyi mnasema kweli. Wala hawatayatamani kamwe kwa sababu ya yale yaliyo tangulizwa na mikono yao; na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwajua vyema wanao dhulumu. Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu wote kwa pupa ya kuishi, na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anatamani lau angeli pewa umri wa miaka elfu. Wala hayo ya kuzidishiwa umri hayamuondoshei adhabu; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda”[72],

[قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاء لِلَّهِ مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ، وَلا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ وَاللَّهُ عَلِيمٌ بِالظَّالِمِينَ]

Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli. Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza mikono yao. Na Mwenyezi Mungu anawajua walio dhulumu”[73]

[فَإِذَا جَاء الْخَوْفُ رَأَيْتَهُمْ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ تَدُورُ أَعْيُنُهُمْ كَالَّذِي يُغْشَى عَلَيْهِ مِنَ الْمَوْتِ]

Ikifika khofu utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye aliye zimia kwa kukaribia mauti”[74], lakini Qur’ani inazidi kuwahakikishia ukweli huu usio kuwa na makwepeo:

[قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فإنه مُلاقِيكُمْ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَى عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ]

Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda”[75],

[قُل لَّن يَنفَعَكُمُ الْفِرَارُ إِن فَرَرْتُم مِّنَ الْمَوْتِ أَوِ الْقَتْلِ وَإِذًا لا تُمَتَّعُونَ إِلا قَلِيلاً]

Sema: Kukimbia hakukufaeni kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuwawa, na hata hivyo hamtastareheshwa ila kidogo tu”[76],

[أَيْنَمَا تَكُونُواْ يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ]

Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu”[77],

[قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَى مَضَاجِعِهِمْ]

“Seme hata mngelikuwa majumbani mwenu, basi wangetoka walioandikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe”[78]. Hivyo khofu ya kifo haitoweki isipokuwa kwa kujiandaa na imamni na matendo mema na kuijenga Akhera kwa yale anayo yaridhia Mwenyezi Mungu na kwa kujikaribisha kwake.

 

Ninadhani mpaka kufikia hapa nitakuwa nimetoa ishara yenye kutosha na ninatakuwa nimefungua mlango wa fikra kwa kiwango cha kutosha kuhusiana na upande, kwa sababu hatua ya kwanza katika kuyatibu maradhi yetu ya kijamii ni kuainisha ugonjwa na maradhi kwa umakini kisha kuutolea matibabu yanayo endana na ugonjwa huo.

Na kwa maelezo hayo, mambo kadhaa yanayo ikamilisha anuwani ya Ujahilia kwa wanadamu wa leo hii yatakuwa yamebainika. Lakini pia tumeutambua upole endelevu wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake, upole ambao hauchagui baina ya kaumu na nyingine. Hivyo ujahilia wa jana hauna ubora ukilinganishwa na huu wa kisasa wala hauna sifa maalumu ambazo kwa ajili yake Mwenyezi Mungu ameiteremsha Qur’ani na akamtuma mtume, halafu akaucha ujahilia wa kisasa bure bure. Ujahilia wa kisasa ni kiwango gani hunahitajia msuluhishi ambaye ni Alhoja bin Al-Hasani (a.s), Imam Al-Mahdi. Na ni kiasi gani amabavyo tunaihitajia Qur’ani ili ituokoe kutokana na shimo hili la Ujahilia wa kisasa na kutufikisha kwenye kilele cha Uislamu.



[1]. Surat At-Tawbah: 31.

[2]. Al-Kafii” 1/53, mango wa At-Taqliid, hadithi: 1.

        Msamiati huu muhimu wa Qur’ani, yaani: (ibada) unahitaji kufafaniliwa vizuri, kwa sababu haufahamiki vyema katika vichwa vya jamii. Wamekuwa wakidhani kuwa maana ya ibada ni kusali au kusujudu tu, na sio kutii.  Ndio utawakuta hawaoni kuwa ni tatizo katika dini yao kusali na kufungu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wakati huo huo miamala na matendo yao wanavifanya kinyume na yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu. Na huu ni ufahamu hatari sana, ambapo hatuna budi kuuondoa utata huu katika jamii. Imekuja katika hadithi kutoka kwa Imamu Jawad (a.s) kwamba alisema: “Yeyote atakaye msikiliza msemaji, basi atakuwa amemuabudu, ikiwa msemaji huyo ataongea katoka kwa Mwenyezi Mungu, basi atakuwa amemuabudu Mwenyezi Mungu, na ikiwa msemaji huyo atasema kutoka kwa Ibilisi…”. Tuhaful U’quul, Uk: 336.

[3]. Surat Al-A’laq: 19.

[4]. Surat Az-Zumar: 3.

[5]. Surat Al-Imran: 64.

[6]. Surat Al-Ahzab: 67.

[7] Surat Hud: 97.

[8]. Surat Maryam: 59.

[9]. Surat Al-Baqarah: 170.

[10]. Surat Al-Hajj: 3-4.

[11]. Surat Al-Fat’hi: 26.

[12]. Surat Al-Qasas:50.

[13]. Surat Al-Baqarah: 165-166.

[14]. Surat Al-A’nkabut: 41.

[15]. Surat An-Nur: 39.

[16]. Surat Al-Maidah: 50.

[17]. Ar-Rasaailul A’sharah cha sheikh Tusi, Uk: 317.

[18]. Surat Ghaafir: 29.

[19]. Surat Al-Imran: 154.

[20]. Kamil Az-Ziyarat: Uk: 201.

[21]. Surat Al-Anbiyaa: 28.

[22]. Biharul Anwar: 76/136.

[23]. Surat Az-Zalzalah: 7-8.

[24]. Surat Al-Ahzab: 33.

[25]. Surat An-Nisaa: 1.

[26]. Wasailush- Shia: kitabun-Nikaah: abwabu muqaddimaatin-Nikaah wa aadaabihi, mlango: 28, hadithi: 1.

[27]. Surat Az-Zumar: 65.

[28]. Surat Al-Haaqah: 44-47.

[29]. Biharul Anwar: 22/467.

[30]. Surat Al-Hujuraat: 13.

[31]. Surat Yunus: 58.

[32]. Surat At-Takathur: 1-2.

[33]. Surat As-Sabai: 35.

[34].  Surat Al-Imran: 14-15.

[35]. Surat As-Sabaa: 37.

[36]. Surat Al-Ankabut: 29.

[37]. Surat Al-A’raaf: 85.

[38]. Surat Al-Mutafifiin: 1-3.

[39]. Surat Al-A’raaf: 82.

[40]. Surat Al-Imran: 154.

[41]. Al-Kafii: 5/59, mlango wa: kuamrisha mwema na kukataza maovu.

[42]. Surat Al-Maidah: 62-63.

[43]. Surat Al-Maidah: 79-80.

[44]. Nahjul-Balaghah: khutba: 27.

[45]. Surat Al-Imran: 110.

[46]. Surat Al-Hajj: 40-41.

[47]. Surat Al-Imran: 104.

[48]. Surat At-Tawbah: 71.

[49]. Surat Fussilat: 26.

[50]. Surat Al-Qamar: 2.

[51]. Surat Al-Baqarah: 170.

[52]. Surat As-Saffat: 69-70.

[53]. Surat Al-A’raaf:70.

[54]. Surat Az-Zukhruf: 22-24.

[55]. Kamalud Diini wa Tamamun Ni’mah:409.

[56]. Al-Kafii: 1/337.

[57]. Al-Kafii: 1/196.

[58]. Surat Al-An’aam: 29.

[59]. Surat Al-Jaathiyah: 24.

[60]. Surat Ath-Thaariyaat: 56.

[61]. Surat Hud: 61.

[62]. Surat Yunus: 14.

[63]. Surat Al-Qiyaamah: 36-40.

[64]. Surat Al-qasas: 77.

[65]. A’waalil Aalaali: 1/267.

[66]. Minhaajul Baraa’h fii Sharhin Nahjul Balaghah: 15/203.

[67]. Surat Ar-Rum: 31-32.

[68]. Surat Al-Muuniin: 53.

[69]. Surat Al-An’aam: 65.

[70]. Surat Al-Imran: 103.

[71]. Surat Al-Anfaal: 62-63.

[72]. Surat Al-Baqarah: 94-96.

[73]. Surat Al-Jumu’a: 6-7.

[74]. Surat Al-Ahzab: 19.

[75]. Surat Al-Jumu’a: 8.

[76]. Surat Al-Ahzab: 16.

[77]. Surat An-Nisaa: 78.

[78]. Surat Al-Imran: 154.