UJAHILIA WA KILEO
UJAHILIA WA KILEO
Wanadamu leo hii wanauishi ujahilia mpya -hata kama baadhi yao watajiiata waislamu- kwa mujibu wa maana ya ujahilia inayo tolewa na Qur’ani. Kwa sababu Qur’ani haiuhesabu ujahilia kuwa ni kipindi maalumu kilicho malizika kwa kudhihiri Uislamu, bali ujahilia kwa mtazamo wa Qur’ani, ni hali ya kijamii inayo ukumba umma na jamii ikabadilika na kusifika kwa sifa ile, kwa sababu ya kuupa na kuacha sheria ya Mwenyezi Mungu aliye takasika:
[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللّهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]
“Je wanataka hukumu ya kijahili? Na nani aliye mwema kuliko Mwenyezi Mungu katika hukumu kwa watu wenye yakini?”[1]. Hali kadhalika Qur’ani imeeleza uwepo wa ujahahilia pale iliso sema:
[وَلا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الأُولَى]
“Wala msijishauwe kwa mishauwo ya kijahilia ya kizamani”[2], kana kwamba ilikuwa ni ishara ya uwepo wa ujahilia mpya, ambao ndio huu wanao ishi wanadamu leo hii katika shari yake, na maangamizi yake na uovu wake.
Bali ujahilia wa leo umekusa mabaya yote ya ujahilia wa nyuma, mwenye nguvu amekuwa akimnyonya mnyonge, na ushoga umekuwa unatungiwa kanuni zinazo uruhusu na kujuzisha kuowana wanaume, na uzinzi unaenea kila mahali, wakati maradhi yake yaangamizayo kama vile: ukimwi na mfano wake yamesambaa ulimenguni kote, na upunjaji katika vipimo na vizani umezagaa kwa aina zake mbali mbali, kwa kiwango cha mtu mmoja mmoja bali hata kwa kiwango mataifa. Kumekuwa hakuna uadilifu katika mahusiano kati ya jamii ya kibinadamu, hadi wanafikia kuyaita mahusiano hayo kuwa ni: ‘Kibaba kwa vibaba viwili’. Na makasisi, na wamonaki na viongozi wengine wa upotovu katika mashetani, na wanadamu na majini baadhi yao wakiwafundisha wengine maneno ya kupambapamba kwa udanganyifu, wamefanywa kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu, wamekuwa wakiharamisha yale yaliyo halalishwa na wakihalalisha yale yaliyo haramishwa. Na sasa miungu ambao huabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu aliye takasika imekuwa haina idadi tena, imekuwa haishii kwenye ya mawe tu, bali kila kukicha akili za kishetani zimeendelea kuafikiana kuongeza miungu wengine. Huku mashetani watu na majini nao wakuiendelea kufundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba na wakizuwia njia ya Mwenyezi Mwenyezi iliyo nyooka:
[لأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ، ثُمَّ لآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَآئِلِهِمْ وَلاَ تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ]
“Akasema: Kwa sababu umenihukumu mpotofu, basi nitawavizia (waja wako) katika njia yako iliyo nyooka. Kisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao, na wengi katika wao hutawakuta ni wenye shukuru”[3], na:
[وَلاَ تَقْعُدُواْ بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللّهِ مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجاً](الأعراف:86)،
“Wala msikae katika kila njia kuogopesha watu, na kuwazuilia na njia ya Mwenyezi Mungu wale wenye kumuamini, na mkataka kuipotosha”[4]. Na wingi ulioje wa watu hawa wanao ziwilia na njia ya Mwenyezi Mungu wale walio amini na wanataka kuipotosha kutoka na maumbile salama, kuanzia kwa machangudoa walio tega mitego ya fitina na udanganyifu, ukija kwenye hisa za kiuchumi ambazo hadi huudondosha udenda, kisha uje kwa wasanii ambao hawana kazi zaidi ya kuharibu tabia na maadili ya kijamii nk.
Yote hayo ni katika sifa na alama za ujahili wa leo na ujahili wa kila zama na kila sehemu. Hii ni moja ya maana za Qur’ani ambazo ni lazima zifahamike na kutambuliwa.
Na hili kulifafanua hili ipasavyo, ninafanya ulinganishaji baina ya itikadi na matendo ya ujahilia wa kizamani na ujahilia wa kileo ambao tunauishi, na hapa nitabainisha mambo yafuatayo:
1. Kuchambua maana na misamiti ya Kiqur’ani na kunyambua maana zake ambazo Qur’ani ilizitaka, na kuondoa utando ulio zizunguka kwa sababu ya kughafilika na Qur’ani, na kutumia akili zetu kabla ya kuirejea.
2. Kuidiriki haja ya Qur’ani pindi tunapo fahamu kuwa wanadamu wamerudi kwenye ujahilia wao wa zamani, na hivyo wana haja ya kwenye Qur’ani ili itekeleze jukumu lake kwa mara nyingine katika kuwaleta kwenye Uislamu halisia.
3. Kukomaza fikra ya Imamu Al-Mahdi (a.s) na ili kujenga hoja ya kielemu kwenye fikra hiyo, kwa kuwa baada ya wanadamu kurudi kwenye ujahilia wao wa zamani, Qur’ani pekee ndiyo yenye uwezo wa kuwaokoa kwa kutekeleza jukumu lake. Pia ni lazima awepo masimamizi atakaye isimamia katika utekelezaji wa majukumu yake, kama vile mtume (s.a.w.w). ama katika kipindi hiki ambacho hakuna mtume, kwa sabau utume ulishia kwake (s.a.w.w), na hatuna mtu ambaye amekusanya sifa hizo isipokuwa Alhoja bin Alhasani (a.s), na sasa hizi ni alama za kudhihiri kwake na siku iliyo ahidiwa inakaribia[5]. Maelezo zaidi kumhusu Imanu Al-Mahdi (a.s) yana sehemu yake maalumu.
[1]. Surat Al-Maidah: 50.
[2]. Surat Al-Ahzaab: 33.
[3]. Surat Al-A’araaf: 16-17.
[4]. Surat Al-A’araaf: 86.
[5]. Ndio maana katika hadithi imekuja kwamba Imamu Al-Mahdi (a.s) natakuja a Uislamu mpya na Qur’ani mpya. Na hii haina maana kwamba atakuja na mafunzo yaliyo nje na Uislamu au na Qur’ani ya babu yake bwana mtume (s.a.w.w), bali kinacho kusudiwa ni kwamba ataondoa utando uliopo kwenye Qur’ani hii na kuirudisha kwenye maishani kwa mara nyingine.