MAJUKUMU YA VYUO VYA DINI KATIKA KUIRESHA QUR’ANI MAISHANI

| |times read : 571
  • Post on Facebook
  • Share on WhatsApp
  • Share on Telegram
  • Twitter
  • Tumblr
  • Share on Pinterest
  • Share on Instagram
  • pdf
  • Print version
  • save

MAJUKUMU YA VYUO VYA DINI KATIKA KUIRESHA QUR’ANI MAISHANI

        Ninaamini kuwa kundi la kwanza kabisa katika jamii lenye majukumu hayo ni hauza tukufu (vyuo vya kidini), wanafunzi wake, na wasomi wake na wakhatibu wake, kwa sababu kusalika na kuimarika kwa jamii kutategema kusalimika na kuimarika kwa hauza, na kuharibika kwa jamii kunategemea kuharibika kwa hauza pia -Mwenyezi Mungu apishe mbali-. Imekuja katika hadithi kutoka kwa bwana mtume (s.a.w.w) kwamba: “Makundi mawili katika umma wangu akiimarika umeimarika umma wangu, na yakiharibika umeharibika umma wangu”. Akaulizwa: Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Ni akina nani hao? Akasema(s.a.w.w): “Ni wanazuoni na watawala”[1].

       Hakika nimesema katika baadhi ya maandiko yangu[2] kuwa: Inahuzunisha sana kuona Qur’ani inakosa uwepo wake katika mitaala ya masomo ya hauza, kwani zimetungwa kwa namna ambayo mwanafuzi hahitaji kubobea katika Qura’ni tangu mwanzo wa masomo yake hadi anamaliza, na haipitii Qur’ani ipokuwa baadhi ishara kidogo pindi inapothibitishwa moja ya kanuni za Kinahau, au katika bahathi ya Kiusuli au katika masiala ya Kifikihi. Hivyo, mwanafunzi amekuwa ni mhanga wa mambo yanayo hitaji akili sana wakati hajapata chakula cha moyo, na roho na hajapata poza na tiba ya nafsi. Bali imefikia hatua mwanahauza anafikia kiwango cha juu katika Fikihi na Usuli hali ya kuwa hajawahi kuyaishi maisha ya Qur’ani wala hajawahi kupata tajiriba ya namna ya kuamiliana nayo na akaifahamu kama ujumbe wa isilahi na kurekebisha. Masiku, hata mawiki yanaweza kupita bila kumuona mwanafunzi akichukua Msahafu asome aya zake na kutafakari maana zake kwa sababu ya kukosekana mahusiano ya kina  ya kiroho baina yake na Qur’ani, ambapo kama angelipata ndani yake chakula inayo mtosheleza kuliko kitu kingine, bila shaka asingeli iacha. Na huu ndio msiba mkubwa wa hauza (vyuo vya dini) na jamii, kiasi kwamba imefikia hata ukawaona baadhi yao hawawezi hata kuisoma vizuri Qur’ani licha kuwa na shakli zake.

       Hivyo basi, kwa kuwa majukumu yanayo bebwa na hauza ni kurekebisha jamii na kuiweka karibu na Mwenyezi Mungu, kuifahamu Qur’ani na kupigania kuiweka katika maisha ya jamii ndio wajubu wake nambari moja. Kwani kheri ya umma haitapatikana ila kwa kushikamana na Qur’ani, na kuongoka kwa uongofu wake na kuangaza kwa nuru yake, kama ilivyo sema hadhithi mashuhuri ya Thaqalayni:

(إني تارك فيكم الثقلين كتاب الله وعترتي أهل بيتي ما إن تمسكتم بهما لن تضلوا بعدي أبداً)

“Hakika Mimi nimekuachieni viziti viwili: kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, Ahlul-bayt wangu. Iwapo mtashikamana navyo, kamwe hamtapotea baada yangu[3].



[1]. Al-Khisal: milango y ail-ithnain, hadithi: 12.

[2]. Wasia na nasaha kwa makhatibu na wanafunzi wa hauza (yamekwisha tangulia ndani ya juzuu hii)

[3]. Tumekwishaitaja huko nyumba.