UDHARURA WA KURUDI KWENYE QUR’ANI
UDHARURA WA KURUDI KWENYE QUR’ANI
Sidhani kama baada ya ufafanuzi huo tutakuwa na haja ya kuendelea kutaja sababu za ziada zinazo tusukuma kurudi kwenye Qur’ani na kuishi katika himaya yake. Kwani sidhani kama yupo ambaye hajatambua hasara mbaya iliyo tupata kwa sababu ya kuipa mgongo Qur’ani. Hivyo, sote kwa pamoja na turejee kwenye Qur’ani, tutubie na jukutia na tuiombe ili nayo ikubali kurudi kutuongoza kuelekea kwa Mwenyezi Mungu aliye tukuka. Ni juu yetu tufikirie njia itakayo kitoa kitabu hiki kwenye hali ya kutegwa tuliyo isababisha sisi wenyewe na hatimaye tuirejeshee nafasi yake katika maishani na katika jamii.
Unaweza ukasema: Mbona jambo hilo ulisemalo limeshatekelezeka! Kwani tunashuhudia vipindi mbali mbali vya kufundisha Qur’ani, kuhifadhi, kusoma tajuwidi, hata kubainisha hukumu zake na uandishi wake.
Niseme kuwa: pamoja na kuyaheshimu hayo yote, ila huko ni kuyapa umuhimu maganda wakati jambo muhimu ni kilicho ndani ya maganda hayo. Kwa sababu kama ilivyo tangulia huko nyumba kwamba, matamshi ni chombo na zana ya kufikishia maana, na ni ganda linalo hifadhi maana ambayo ndio kiini na lengo, lakini pia neno ni ala ya kuhamishia maana kwenda akilini. Sasa je tutosheke na maganda na tuache kilicho ndani yake? Kinacho tafutwa ni kuirejesha Qur’ani kwa uhalisia wake, na kwa madhumuni yake, na kwa maana zake, na fikra zake na mafunzo yake. Ndio, ni kweli kwamba hatua ya kwanza ya kuliendea hilo, ni kuisoma Qur’ani, na kufahamu maana za maneno yake na kuzitumia kanuni za lugha ya Kiarabu kwenye matokeo ya herufi zake.